MUANGALIZI: UDAKU

Hot

Post Top Ad

Your Ad Spot
Showing posts with label UDAKU. Show all posts
Showing posts with label UDAKU. Show all posts

Saturday, January 27, 2018

Aslay akemea mashabiki kumfananisha na Rich Mavoko

3:50:00 AM 0
Msanii wa muziki Bongo, Aslay amesema si vizuri kufananishwa na Rich Mavoko kwani ni msanii ambaye amemtangulia katika muziki.
Muimbaji huyo amesema Rich Mavoko amekuwa akifanya vizuri kila siku, hivyo mashabiki wanaomshindanisha wanakosea.
“Huwezi kunishindanisha na Rich Mavoko, yule ni kaka yangu halafa anafanya vitu vikubwa, nimemkuta kwenye muziki na amefanya vitu vikubwa, kwa ukisema unanishindanisha na Rich Mavoko utakuwa unakosea,” Aslay ameiambia Bongo5.
Katika hatua nyingine Aslay ameeleza sababu ya yeye kuwa miongoni mwa wasanii ambao ngoma zao zinapata views zaidi katika mtandao wa YouTube.
“Ni mashabiki wangu wa kweli ndio maana unakuta hata nikitia ngoma leo kesho unakuta nina laki moja, kwa hiyo siwezi kusema labda nilikuwa nashindana au nina vitu vikubwa sana navifanya niwe na views wengi YouTube ni mashabiki zangu kunipenda kweli,” amesema.
Read More

Ruby, Clouds Media Bifu limekwisha

2:53:00 AM 0

Msanii wa muziki Bongo, Ruby amemaliza tofauti baina yake na Clouds Media Group. 

Muimbaji huyo ametumia kipindi cha XXL kuwaomba radhi wale wote aliowakwaza katika chombo hicho cha habari.

“Yeyote, awe ni mwanakamati wa Clouds, team Clouds au awe ni shabiki wa nje I like to apologize guy to say sorry to my country, sorry to this management Clouds, I love them so much all I need is support mimi naamini kwamba ukiwa mjinga kwenye kila kitu utapata kujua vitu vingi sana,”
amesema Ruby.

“Nilikaa nikamuomba Boss wangu Ruge samahani, mimi ni mdogo wewe ni mkubwa, of course kwa chochote kile mimi ndio nakosea,” amesema.

Clouds Media Group walikuwa wamesitisha kucheza nyimbo za msanii huyo kutokana na tofauti zao, hivyo sasa nyimbo zake zinachezwa na inaelezwa tangu November mwaka jana ilitolewa ruhusu kwa ngoma zake kuchezwa.
Read More

Thursday, January 25, 2018

Mke Kumtaka wema aolewe na Nabii Tito

1:27:00 AM 0
African Sweetheart, Wema Sepetu
 Katika hali isiyotarajiwa, imeelezwa kuwa msanii nyota wa filamu za Kibongo, Wema Sepetu, amemlipua mke wa ‘Nabii’ Tito baada ya mwanamke huyo kumshawishi kupitia mitandaoni aolewe na nabii huyo.

Chanzo makini kilisema kuwa, msanii huyo amekasirishwa na kitendo cha mke huyo kumshawishi kuolewa na mumewe anayeitwa Onesmo Machija ‘Nabii Tito’ (44).

“Wema Sepetu nakupenda sana hata Nabii Tito anakupenda sana, kwanza mzuri, una shepu nzuri hata katika mambo ya Kiafrika unaongoza kwa uzuri.

“Nabii Tito huyo kwa watu wasiomfahamu wanasema sio nabii lakini kwa mimi ninayemfahamu na kuishi naye naona mambo ya kinabii anayofanya, nakuomba ukubali hata mimi nakupenda sana, kwanza una shepu nzuri.

“Uwe mke mwenzangu, ukubali kuwa mke wa Nabii Tito. Sikia kilio cha mke wa nabii,” amesikika kwenye video mke huyo wa Nabii Tito akimbembeleza Wema.

Naye Nabii Tito kwenye video hiyohiyo amechombeza kwa kubembeleza kwamba Wema akubali kuwa mkewe ili kanisa lao likuwe.

Alipotafutwa Wema na kuulizwa kuhusiana na video hiyo alisema, ameiona na amekasirishwa na kile walichokifanya nabii huyo na mkewe.

“Kiukweli wameniudhi sana kwa kunidhalilisha. Nawasiliana na mwanasheria wangu ili nimburuze mahakamani mwanamke huyo,” alisema Wema.

Hata hivyo, Jeshi la Polisi mkoani Dodoma, mapema wiki hii lilimkamata nabii huyo na kumfanyia mahojiano kutokana na mahubiri ya kidini anayoyafanya na limesema mtu huyo ana matatizo ya akili.

Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Dodoma, SACP Gillesi Muroto amesema Juni 23, 2014, mtu huyo aliwahi kulazwa Hospitali ya Taifa ya Muhimbili kwa ajili ya matibabu ya akili chini ya daktari aliyejulikana kwa jina moja la Dk. William ambapo aliporuhusiwa alitakiwa kurejea hospitalini hapo Julai 9 mwaka huohuo lakini hakurejea.

Kamanda Muroto aliendelea kusema kwamba, baada ya hapo Machija ambaye kanisa lake halijasajiliwa popote, aliibukia mkoani Dodoma katika Kijiji cha Nong’ona kilicho karibu na Chuo Kikuu cha Dodoma (Udom) akifanya mahubiri ya kidini yaliyodaiwa kuwa hayakuwa na maadili ya kidini.

“Kwa msingi huo, jeshi la polisi limempeleka Hospitali ya Rufaa ya Milembe iliyoko mkoani Dodoma kwa ajili ya kumpima tena matatizo hayo ya akili na baada ya majibu kutolewa, Dk. Dixon Philipo aliyemshughulikia alithibitisha kwamba bado ana matatizo hayo ya akili,” alisema kamanda Muroto juzi na kusisitiza kuwa wanaendelea kumshikilia kutokana na matendo yake aliyoyafanya ili kufanya uchunguzi zaidi.


Nabii Tito na mkewe pamoja na mfanyakazi wake wa ndani.
Read More

Bifu zito Kati ya Stamina na Edu boy

1:06:00 AM 0

Msanii wa bongo fleva anaejulikana kwa jina la edu boy, alieachia jiwe lake jipya siku chache zilizopita amejikuta kuingia kwenye bifu zitto na msanii stamina ambae alifanya nae remix ya ngoma yake ya Naiee, baada ya kutoa ngoma mpya inayoitwa TUNASAFISHA ambapo ndani ya ngoma hiyo amewapita wasanii wengi kwa kuwachana akiwemo Diamond, alikiba dogo janja stamina na wengine wengi.

Bifu hili kati ya stamina na Edu boy limesababishwa na ngoma hiyo baada ya kuibwa kuwa stamina anaimba kwa kusafiria nyota za wasanii wenzake, Edu boy. katika mahojiano aliofanyiwa edu boy na times fm ameeleza uwa kabl hajatoa ngoma hiyo alimshirikisha stamina na alijibiwa kuwa kama kamchana nae atamjibu na baadae kilichotokea  baada ya ngoma kutoka alishangaa kuona amefungiwa (BLOCK) na stamina kwenye kila njia ya mawasiliano

Vile vile edu alieleza kuwa kama ni bifu, liwe la kimuziki nae aingie studio amjibu na ikiwezekana waingie ulingoni ili zaidi ya menzake ajulikane na kusisitiza kuwa hata stamina akiiingia ulingozi hataweza kwani atamuaibisha.
Read More

Thursday, December 28, 2017

Moto wazidi kuwaka kati ya Zari na Hamisa

5:56:00 AM 0

Baada ya mwanamitindo Hamisa Mobetto kumtibua upya mama watoto wa Diamond, Zari The Boss Lady ikiwemo kumuita mcheza picha chafu, Zari ajibu mapigo tena.
Mobetto ambaye alikuwa nchini Uganda weekend iliyopita kwaajili ya show ya Girls Power, alimtupia dongo Zari na kumuita mcheza picha za uchi.

Alhamisi hii Zari ameamua kumtolea uvivu Mobetto kwa kuandika ujumbe mkali mfululizo kupitia mtandao wa snapchat.
“Bora mimi changudoa mzee niliye na mafanikio na bado ananipenda kuliko kijana wa miaka 20+ mama uliyeachwa solemba mara mbili na tuzo juu #MchepukoUsioNaAKili #MweweWaMwaka,” , aliandika Zari Snapchat.


“Kijana, kijana kila siku kijana, kijana na mzuri lakini huwezi kutafuta mwanaume wa kwako mwenyewe….namna chan**doa usivyojiamini, Kama unajiamini na uzuri na akili basi acha tuone mwanaume gani atakutaka baada ya drama hizi, baby daddy 3 loading ukiwa na miaka 20+ atakuwa mjinga pia,” alisema Zari kupitia ujumbe huo.
Zari akaongeza “sio wewe cha***doa uliyelia social media ukidai Lulu kakuibia bwana’ko lakini umegeuka kufanya hicho hicho ulicholilia wakati unajua inavyouma, Mungu hawezi kubariki furaha yako juu ya maumivu ya mwanamke mwingine…ng’oo!!!”
“Unaweza kupost picha zote za nyuma ukiwa nae, lakini tayari nimekwisha msamehe makosa yake yaliyopita. Siwezi kubadilisha historia….nimechukulia kawaida naendelea kujenga maisha yangu ya kesho. Uchawi wote unaisha nguvu na sasa anarudi kwa akili zake kumrudia,” amesema Zari na
Read More

Tuesday, February 7, 2017

Uongozi wa Yanga wavunja ukimya malipo ya Kocha wao

7:25:00 AM 0

Katibu wa Yanga, Boniface Mkwasa

HATIMAYE Uongozi wa Klabu ya Yanga, umefunguka na kusema wapo katika mchakato wa mwisho wa kukamilisha malipo ya deni la aliyekuwa Kocha Mkuu wa timu hiyo, Ernest Brandts aliyevunjiwa mkataba wa kuifundisha timu hiyo miaka miwili iliyopita.

Yanga imetakiwa kulipa dola 11,000 za Marekani kama ambavyo iliamriwa Juni 30, 2015 na Kamati ya Hadhi ya Wachezaji ya FIFA, jambo ambalo lilipuuzwa na klabu hiyo kwa muda mrefu kabla ya FIFA kuibuka na kutishia kuishusha daraja Yanga endapo wasipolipa deni hilo.

Katibu Mkuu wa Klabu ya Yanga, Charles Mkwasa amesema suala hilo lilikuwa ni la muda mrefu na walikuwa wakilifanyia kazi lakini kutokana na kupewa maagizo kwa uzito mkubwa wameamua kulifanyia kazi kwa haraka ili kulimaliza suala hilo kabla ya Kamati ya Nidhamu ya FIFA haijakaa kwenye vikao vyake vinavyotarajiwa kukaa siku yoyote.

Amesema Uongozi wa klabu hiyo unatambua kwamba wanadaiwa kiasi hicho cha fedha kilichoelezwa na FIFA wiki iliyopita na kuwataka mashabiki wa klabu hiyo kuondoa hofu ya timu yao kushushwa daraja kwa kuwa uwezo walionao kwa ajili ya kulipa deni hilo ni mkubwa.

"Suala hili tulianza kulijadili toka mwaka 2014 mara baada tu ya kuvunja mkataba na Brandits, lakini kulikuwa na baadhi ya mambo mbalimbali yaliyoingiliana hapa katikati na kukwamisha kutekeleza mpango ambao tulijiwekea,"

"Lakini hata kama FIFA isingetupa hili agizo ni lazima tungelimaliza hili suala haraka kwa sababu tulikuwa tunatambua mchango mkubwa aliouonesha Brandts katika kuhakikisha Yanga inakuwa bora kwa wakati wake ule aliokuwa akiifundisha timu yetu," alisema Mkwasa.

Kitendo cha Yanga kutolipa deni hilo kwa wakati, imetafsiriwa kwamba imevunja Kanuni ya 64 inayozungumzia Nidhamu katika FIFA yaani FDC (FIFA Disciplinary Committee).

Ikumbukwe FIFA iliieleza klabu ya Yanga siku chache zilizopita kama watashindwa kumlipa Brandts fedha zake hizo kabla ya kamati kuketi na kufanya vikao vyake watakua wamekiuka sheria na kanuni mbalimbali za soka na adhabu mbalimbali zinaweza kuwakumba ikiwemo Kukatwa pointi katika michezi ya Ligi ya Vodacom inayoendelea nchini au kushushwa daraja.

Wakati huo huo, Mkwasa amewataka mashabiki wa Yanga kuwa na imani na timu yao inayotarajia kusafiri jumamosi kuelekea nchini Comoro wanakwokwenda kucheza mchezo wa ligi ya mabigwa dhidi ya Ngaya Fc.

Amedai kuwa kocha wa timu hiyo, George Lwandamina kwa ushirikiano na benchi lake la ufundi wataweza kuwatoa kimasomaso mashabiki wa timu hiyo kutokana na wao kama uongozi kuwapatia vitu vyote vya muhimu vinavyohitajika katika mashindano hayo.

Amesema hawezi kuzungumzia zaidi mchezo wao dhidi ya Ngaya kwa kuwa tathmini hiyo inapaswa kutolewa na kocha wa timu hiyo ambaye anatambua uimara na udhaifu wa wachezaji wake wanaounda timu yake.

"Mimi kwa sasa sipendi kusema mchezo huo utakuwa ni mgumu au sio mgumu kwa sababu mimi sipo kwenye benchi la ufundi la Yanga kwa hiyo kazi hiyo tumwachie kocha na benchi lake, lakini kama kiongozi wa Yanga nikiangalia mahitaji tuliyowatimizia hawa wachezaji na makocha wetu basi watafanikiwa tu kwenye mechi zao," aliongeza Mkwasa.

Katika mchezo huo utakaopigwa Februari 12 huko nchini Comoro Klabu ya Yanga itamkosa beki wake, Andrew Vicent 'Dante' kutokana na mchezaji huyo kupata kadi nyekundu katika mchezo wa Kombe la shirikisho uliofanyika mwaka jana dhidi ya Timu ya TP Mazembe ya DR Congo.
Read More

Thursday, January 19, 2017

Aboutrika atajwa orodha ya magaidi Misri

7:28:00 AM 0
Msahambuliaji wa zamani wa Misri, Mohamed Aboutrika
MAMLAKA za usalama za Nchi ya Misri zimemweka mchezaji wa zamani wa soka wa timu ya taifa ya nchi hiyo pamoja na Al Ahly, Mohamed Aboutrika katika orodha ya magaidi baada ya kuhusishwa na kikundi cha waislam wa Brotherhood.

Aboutrika anashutumiwa kuwasaidia kifedha kikundi cha  Brotherhood, ambacho mamlaka za Misri kimewaweka kwenye kundi la magaidi kutokana na matukio mbalimbali wanayoyafanya.

Mnamo mwaka 2012, Aboutrika alimpigia kampeni ya urais, Rais wa zamani wa nchi hiyo Mohamed Morsi, ambaye ni mwanachama wa Brotherhood.

Kwa mujibu wa sheria mbalimbali za Misri, mtu yoyote anayewekwa kwenye listi ya ugaidi, hufungiwa kusafiri na passport yake pamoja na mali zake hushikiliwa.

Kwa upande wake Mwanasheria wa Aboutrika, Mohamed Osman, alisema mteja wake hajatiwa hatiani wala hajapewa taarifa rasmi juu ya mashtaka wanayomtuhumu juu yake.
Read More

Madrid Yakung'utwa Tena

7:27:00 AM 0
Kocha wa Real Madrid Zinedine Zidane
MIAMBA ya Soka Nchini Hispania,Real Madrid wameshindwa kuonesha ubabe wao kwenye soka mara baada ya kukubali kichapo cha bao 2-1 dhidi ya klabu ya Celta Vigo katika mechi ya mkondo wa kwanza wa robo fainali ya Kombe la Mfalme, Copa del Rey iliyopigwa kunako uwanja wa Santiago Bernabeu.

Miamba hao wa soka waliocheza mechi 40 bila kufungwa wameingia katika rekodi nyingine ya kufungwa michezo miwili mfululizo huku wa kwanza wakifungwa na Sevilla katika mchezo wao uliopigwa jumapili iliyopita.

Celta Vigo ndio walikuwa wa kwanza kupata goli kupitia kwa mshambuliaji wa zamani wa Liverpool Lago Aspas mnamo dakika ya 16 huku madrid wakisawazisha bao lao kupitia Marcelo Vieira kabla ya kuongezwa dakika chache baadae.

Katika mchezo huo uliokuwa wa ushindani mkubwa Mfaransa Karim Benzema alipoteza nafasi nzuri mara baada ya kombora lake kupaa juu ya goli zikiwa zimesalia dakika nane mechi hiyo kumalizika.

Mechi ya marudiano kati ya Madrid na Celta Vigo inatarajiwa kuchezwa Galicia Jumatano wiki ijayo.
Read More

Man U yaipiku Madrid kwa Utajiri

7:24:00 AM 0

HATIMAYE Klabu ya Manchester United imerudi kileleni mwa orodha ya klabu zenye vipato vikubwa duniani  kwa msimu uliopita mara baada ya kuwapiku miamba ya Soka Nchini Hispania, Real Madrid.

Kwa Mujibu wa taarifa zilizochapishwa na kampuni kubwa ya ukaguzi wa hesabu Duniani, Deloitte zinaonesha mapato ya Man U yameongezeka kutoka Euro Mil.519.5 kwa msimu wa 2014-15 hadi 689 kwa msimu wa 2015-16.
Viongozi wa Klabu ya Manchester United

Hii ni mara ya kwanza kwa Man U kushika nafasi hiyo tangu walipoiachia mwaka 2003-4 na kuchukuliwa na Madrid waliofanya vizuri kwa kipindi cha miaka 11 mfululizo kwa kutengeneza kiasi cha Euro mil. 577 kiasi ambacho hakikufikiwa na klabu nyingine yoyote duniani.

Ripoti ya Shirika la Deloitte inaonesha ukijumlisha mapato ya timu ishirini bora kwa msimu wa 2015-16 vimeongezeka kwa asilimia 12% na kufikia jumla ya Euro. Bilioni 7.4.

Madrid iliyokuwa kinara kwa miaka 11 imeangukia nafasi ya tatu wakiwa wanajumla ya Euro Mil. 620.1 huku nafasi ya pili ikienda kwa wapinzani wao wakubwa Barcelona wenye Eiro Mil. 620.2 na nafasi ya nne ikidondokea kwa Klabu ya Bayern Munich yenye kiasi cha Euro Mil. 592.

Hata hivyo Ripoti hiyo inaonesha timu za uingereza zimefanikiwa kushika nafasi kubwa zaidi kuliko klabu zote duniani kutokana na kuingiza timu tano katika orodha ya timu kumi zenye mapato makubwa huku Manchester City ikishika nafi ya Tano jambo ambalo halijawahi kutokea.

Mwishooooooooo
Read More

Monday, December 19, 2016

MUONE HAPO MISS DUNIA 2016

6:13:00 AM 0


Picha za juuzinaonesha namna Puerto Rico alivyovalishwa taji la miss Dunia,Picha nyingine  akiwa katika pozi mara baada ya kuvaishwa taji la miss Dunia 2016.

Walimbwende mbalimbali wakiwa katika picha ya pamoja kabla ya kutangazwa kwa mshindi wa taji la mlimbwende bora wa dunia.
Read More

Saturday, November 26, 2016

ETI OKWI KUINGIA MSIMBAZI! SIJUI

5:46:00 AM 0
 
Mchezaji wa Zamani wa Klabu ya Simba, Mganda Emmanuel Okwi, Piacha na Maktaba.
Kocha wa Simba, Joseph Omog mjanja sana kwani amewaambia viongozi wa Simba ana nafasi tatu za wachezaji ambao anataka wamuongezee nguvu kikosini.

Mmoja wa mabosi wa Kamati ya Utendaji ya Simba ambayo ndiyo ya kwanza kuona ripoti ya kocha, amesema kwamba, anataka wamsajilie kipa, beki na straika mmoja.

Katika ripoti yake, Omog ametoa sifa tu za wachezaji anaowataka huku akiacha zoezi la kuwasajili kwa viongozi lakini akasisitiza hahitaji straika kutoka nje ya nchi kwani atapata presha kama ilivyo kwa waliopo.

Simba ina mastraika Laudit Mavugo raia wa Burundi na Fredrick Blagnon wa Ivory Coast ambao bado hawajaonyesha uwezo mkubwa katika Ligi Kuu Bara katika mechi 15 za Simba.

Kabla ya kuiona ripoti ya Omog, baadhi ya viongozi wa Simba ambao wameona Mavugo na Blagnon walivyochemsha, wakaanza mipango ya kumrejesha kikosini Emmanuel Okwi kutoka SønderjyskE ya Denmark.

“Kutokana na ripoti ya Omog, sasa hatuna tena mpango wa kumsajili Okwi kwani itakuwa kinyume na matakwa ya kocha hivyo tunaendelea na mambo mengine kwa kufuata anachotaka yeye (Omog).

“Tulidhani Okwi akija atafanya vizuri moja kwa moja kwani anaijua ligi yetu, lakini kocha ameshikilia msimamo wake wa kutaka straika kutoka ndani ya nchi, hatuna jinsi tunafuata kile alichosema,” alisema bosi huyo.


Licha ya viongozi wake kutokuwa tayari kuweka wazi kuhusu usajili wa straika mzawa, gazeti hili linafahamu Simba inamfukuzia Victor Hangaya wa Prisons ili iweze kumsajili.

SOURCE: CHAMPIONI
Read More

Wacheza Karate nchini watahadharisha

5:29:00 AM 0

Mkuu wa Wilaya ya Temeke, Felix Lyaniva, Picha na Maktaba.
MKUU wa Wilaya ya Temeke, Felix Lyaniva amewataka vijana wenye taaluma ya karate nchini kuyatumia vyema mafunzo hayo katika kujihami na kulinda usalama wa Ttaifa badala ya kujikita katika kutenda vitendo vibaya vinavyopelekea uvunjifu wa amani.

Akizungumza na Wadau mbalimbali waliojitokeza kuchangia damu katika viwanja vya Mwembe Yanga Temeke jana, Lyaniva amesema vijana hao wanapaswa kuitumia vyema taaluma hiyo na kuacha kujiingiza kwenye makundi mabaya ikiwemo Panya Road ambao wamekuwa wakihatarisha usalama wa raia pamoja na mali zao.

"Nimeona mambo mazuri yaliyooneshwa na hawa vijana wetu wa karate na ni imani yangu watatumia taaluma waliyonayo katika kuhakikisha ulinzi wetu unaimarika lakini kama watakuwa wanatumia vibaya nguvu zao nahakika hawataweza kuishi kwa muda mrefu kwa kuwa sasa hivi Serikali hatutaki kuona mambo ya uhalifu yakiendelea zaidi," alisema Lyaniva.

Amesema wataalamu wa karate ndio watu wanaotegemewa katika kuimarisha ulinzi lakini wao wamekuwa ndio watu wa kwanza katika kufanya vitu visivyopendeza kwa kuwatendea wasio na nguvu vitendo vya kinyama vyenye dalili zote za uzalilishaji.

Katika hatua nyingine Lyaniva amewaahidi waendesha baiskeli wa jumuiya hiyo kuwafungulia akaunti kila mmoja wao katika benki ya Amana ili kuwawezesha kufanikisha safari yao ya kwenda nchini Saudi Arabia ambako walipanga kutumia usafiri huo kutoka Tanzania mpaka Maka ambako ndio huenda kuhiji.

Amesema anatambua umuhimu wa waendesha baiskeli hao na yeye kama kiongozi wa Serikali ameguswa na madereva hao na kuahidi kushughulikia akaunti zao ili waweze kupatiwa mikopo isiyo na riba itakayowasaidia kwa kupata nauli pamoja na fedha za mahitaji mengine watakayoyahitaji pindi watakapokuwa huko nchini Saudi Arabia.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa waendesha Baiskeli wa JAI, Ibrahim Minja amesema wameamua kufanya matembezi ya baiskeli katika maeneo mbalimbali ya nchi ili kuweza kuwahamasisha watu kujitokeza katika kuchangia damu na kumaliza tatizo hilo ambalo linaonekana kuumiza serikali kwa sasa.

Amesema Matembezi hayo yamehusisha zaidi ya madereva 18 kutoka mikoa mbalimbali nchini ikiwemo Tanga, Moshi pamoja na Lindi na kushirikisha waendesha baiskeli wenye umri tofauti tofauti huku wengi wao wakiwa ni watu wazima wenye umri zaidi ya miaka 40.

Akizungumzia msaada walioupata kutoka kwa Mkuu wa wilaya, Minja amesema kuwa wanayofuraha ya kumpata kiongozi ambae amekuwa makini na kutambua mahitaji ya wananchi kwa wakati jambo linaloongeza utayari kwa wao kufanya kazi nzuri zaidi ya hiyo waliyoifanya.

"Kwa mambo haya ambayo Lyaniva ametufanyia tunaahidi kuhamasisha zaidi watu wengi katika kuchangia damu ili tuweze kwenda kumaliza matatizo yanazisumbua hospitali zetu kwa sasa hasa kwenye hili janga la damu kwani tunaona uhitaji umekuwa ni mkubwa zaidi ya hivi tunavyofanya sisi," alisema Minja.
Read More

Miss Universe Tanzania 2016 apatikana

5:19:00 AM 0
 
Aliyekuwa Mshindi wa Miss Universe Tanzania 2014 akipongezwa na baadhi ya mashabiki waliojitokeza kushuhudia mashindano hayo, Picha na Maktaba.

MLIMBWENDE Johan Dimack Kutoka arusha usiku wa kuamkia jana amefanikiwa kuibuka mshindi katika Mashindano ya Miss Universe Tanzania nakupata zaidi ya sh.mil tatu ambazo atakuwa anapewa Kwa awamu.

Mshindi wa pili katika mashindano hayo ni mwanadada Liliani Love mwenye Asili ya kimasai huku nafasi ya mshindi wa Tatu ikinyakuliwa na Liliani Felix Kutoka Ilala Dar Es Salaam ambapo pia amepata nafasi ya kuutangaza utalii Kwa maana Miss Tourism.

Akizungumza Mara baada ya kutangazwa mshindi  Dar Es Salaam jana Mlimbwende Dimack alisema kwanza anamshukuru Mungu Kwa kufika alipofika huku akikiri kuwa Mchuano ulikuwa Mkali sana Kwa maana kila mrembo alikuwa mkali.

"Kwakweli naweza kusema siamini kama mimi ndio mshindi kwani wenyewe mmeona warembo wote waliokuwa wameshiriki ni wakali lakini na mshukuru Mungu na majaji Kwa kuniona mimi ndio Mrembo."alisema mlimbwende huyo.

Aidha mwanadada huyo ambae pia aliweza kujieleza Kwa ufasaha tena wa lugha ya kiingereza baada ya kuulizwa swali na moja ya majaji hao,kwamba anadhani amekosewa kuwa mwanamke alisema anajivunua kuzaliwa mwanamke na wala hajutii.

Naye mshindi wa pili na watatu Liliani Felix alisema kuwa anaamini amefanya vizuri ukizingatia kwamba ndio mara yake anashiriki ukilinganisha na wengine ambao waliwahi kushiriki.

"Naweza kusema nimeridhika kwa kushika nafasi ya tatu kwani si haba ukizingatia ndio kwaza nashiriki mashindano haya lakini kikubwa zaidi nimepata nafasi ya kuwa Miss Tourism hivyo bado nitaitangaza nchi yangu "alisema Liliani Felix.

Kwaupande wake Mkurugenzi na Mwandaaji wa Mashindano hayo ya Miss Universe Tanzania Maria Sarungi alisema mashindano Kwa mwaka huu yamekwenda vizuri na mshindi amepatikana kihalali.

Alisema kuwa baada ya mshindi kupatikana Kazi hiyo inaaza upya Kwa maana katika kuhakikisha mshindi huyo na wezake wanakwenda kuchuana na wengine Duniani katika nchi ambayo wataambiwa mapema wiki ijayo.

"Tunashukuru Mashindano yamemalizika lakini Kwetu kama waandaaji naweza kusema ndio Kazi inaaza upya Kwa maana tunajukumu kubwa la kumwandaa mrembo wetu ili na sisi tukapambane na sio kushiriki na Hii ni Kwa wote Kwa maana hata hawa washindi wa pili na watatu pia watawakilishi nchi."alisema Maria

Aidha mbali na ushindi huo Maria alisema Mshindi wa kwaza Jihan Dimack atapewa Zawadi ya sh.mili tatu  lakini Kwa awamu kadri atakavyokuwa anashiriki,mshindi wa pili sh.mil.moja na mshindi wa tatu  sh.laki tano na atawakilishi nchi Kwenye mashindano ya Miss Tourism.

Pia aliwapongeza majaji ambao wengi wao walitoka nje ya Tanzania Kwa Kazi nzuri waliyoifanya kwani walionesha umahili mkubwa katika kazi yao.

Jumla ya walimbwende kumi Kutoka mikoa tofauti walinyukana katika mashindano hayo ya Miss Universe 2016  ambapo Jihan Dimack ndio ameibuka mshindi.
Read More

Friday, September 2, 2016

Povu limetoka Irene Uwoya baada ya mtoto kusemekana sio wa Ndikumana

10:24:00 AM 0
povu zito limemtoka mcheza bongo muvi wanadada mrembo Irene Uwoya bbada ya shirika la wambea shilawadu kupekenyua ya ndani na kukuta mtoto sio wa Ndikumana inasemekana lakini
 Angalia video hiyo alichokisema..
 
Read More

Sunday, July 24, 2016

Wavulana wavaa sketi shuleni Nchini Uingereza

5:41:00 AM 0
Wavulana wanne wakiwa wamevaa sketi kama unifom za shule huko nchini uingereza

Na Mwandishi Wetu

Wavulana wanne katika shule moja nchini Uingereza wameeenda shuleni wakiwa wamevaa sketi kulalamikia hatua ya mwalimu kuwaadhibu kwa kuvalia kaptura siku yenye joto kali zaidi nchini humo.

Wanafunzi hao wa darasa la mwaka wa tisa katika shule yaLonghill eneo la Rottingdean, Sussex Mashariki, walikuwa miongoni mwa wanafunzi 20 wavulana waliovalia kaptura za kuvaliwa wakati wa mazoezi badala ya suruali ndefu.

Baadhi walifukuzwa shuleni Jumanne na wengine kutengwa hadi siku iliyofuata. Waliokubali kuvua kaptura hizo na kuvalia suruali ndefu hawakuadhibiwa.

Lakini badala ya kuvalia sare kamili ya wakati wa masomo, kama walivyokuwa wameagizwa, wanafunzi wanne walirejea shuleni Alhamisi wakiwa wamevalia sketi.

Michael Parker, mmoja wa wanafunzi, akiwa na kaptura na akiwa na sketi
Watatu waliambia wavue sketi hizo lakini wote kwa pamoja wakakataa na ndipo wakaruhusiwa kuendelea kukaa shuleni.

Mwalimu mkuu Kate Williams aliwaambia wanaweza kuvalia mavazi yoyote, mradi yawe ni sehemu ya sare iliyokubalika shuleni.

Wanafunzi hao walivaa sketi kwa siku mbili mfululizo ikiwa ni kujirisha kwa kile walichokiona kuwa ni sahihi.
Read More

Ujumbe wa Zitto Kabwe kwa Rais Magufuli baada ya kuwa Mwenyekiti wa CCM

5:13:00 AM 0
 
Kiongozi Mkuu wa Chama cha ACT-Wazalendo na Mbunge wa Kigoma Mjini, Zitto Kabwe
Na Mwandishi wetu.
 
Baada ya Rais Magufuli kutangazwa kuwa ameshinda na kuwa ndiye Mwenyekiti wa tano wa CCM Taifa akichukua nafasi iliyokuwa inashikiliwa na Rais wa awamu ya nne, Dkt Jakaya Kikwete, Mbunge wa Kigoma Mjini na Kiongozi Mkuu wa ACT- Wazalendo ameandika haya kwenye ukurasa wake wa Facebook;-
 
“Napenda kumpongeza Rais John Magufuli kwa kuchaguliwa kwake kuwa Kiongozi wa Chama chake cha CCM akiwa Mwenyekiti wa Tano chama hicho. CCM imeendelea kudumisha utamaduni wa kukabidhiana Uongozi kila baada ya muda.
 
Jambo ambalo ni la kujifunza hasa kwa vyama vya Siasa nchini na barani Afrika. Nataraji kwamba Rais na Mwenyekiti mpya wa CCM ataona umuhimu wa Vyama vya Siasa kuendelea kufanya Siasa bila vikwazo na kwa mujibu wa Sheria za Nchi yetu.
 
 Demokrasia inaimarisha Amani kwa kupaza sauti za HAKI. Karibu kwenye changamoto za kuongoza Vyama vya Siasa ndugu Rais.” 

Pia alisema hivi
"Zanzibar sasa iwe ajenda ya kudumu kwa Vyama vyote vya Siasa vinavyosimamia HAKI. Rais Magufuli hawezi kukwepa tena suala la Zanzibar kwani sasa ni Mwenyekiti wa Chama chake. Hana excuse tena. Suala la Zanzibar sio la CUF peke yao, ni suala letu sote. Shime wana demokrasia"



Read More

ROMA povu la mtoka baada ya kukataliwa kwa kina ALIKIBA....

Post Top Ad

Your Ad Spot