MUANGALIZI: BURUDANI

Hot

Post Top Ad

Your Ad Spot
Showing posts with label BURUDANI. Show all posts
Showing posts with label BURUDANI. Show all posts

Saturday, January 27, 2018

Aslay akemea mashabiki kumfananisha na Rich Mavoko

3:50:00 AM 0
Msanii wa muziki Bongo, Aslay amesema si vizuri kufananishwa na Rich Mavoko kwani ni msanii ambaye amemtangulia katika muziki.
Muimbaji huyo amesema Rich Mavoko amekuwa akifanya vizuri kila siku, hivyo mashabiki wanaomshindanisha wanakosea.
“Huwezi kunishindanisha na Rich Mavoko, yule ni kaka yangu halafa anafanya vitu vikubwa, nimemkuta kwenye muziki na amefanya vitu vikubwa, kwa ukisema unanishindanisha na Rich Mavoko utakuwa unakosea,” Aslay ameiambia Bongo5.
Katika hatua nyingine Aslay ameeleza sababu ya yeye kuwa miongoni mwa wasanii ambao ngoma zao zinapata views zaidi katika mtandao wa YouTube.
“Ni mashabiki wangu wa kweli ndio maana unakuta hata nikitia ngoma leo kesho unakuta nina laki moja, kwa hiyo siwezi kusema labda nilikuwa nashindana au nina vitu vikubwa sana navifanya niwe na views wengi YouTube ni mashabiki zangu kunipenda kweli,” amesema.
Read More

Thursday, December 28, 2017

Moto wazidi kuwaka kati ya Zari na Hamisa

5:56:00 AM 0

Baada ya mwanamitindo Hamisa Mobetto kumtibua upya mama watoto wa Diamond, Zari The Boss Lady ikiwemo kumuita mcheza picha chafu, Zari ajibu mapigo tena.
Mobetto ambaye alikuwa nchini Uganda weekend iliyopita kwaajili ya show ya Girls Power, alimtupia dongo Zari na kumuita mcheza picha za uchi.

Alhamisi hii Zari ameamua kumtolea uvivu Mobetto kwa kuandika ujumbe mkali mfululizo kupitia mtandao wa snapchat.
“Bora mimi changudoa mzee niliye na mafanikio na bado ananipenda kuliko kijana wa miaka 20+ mama uliyeachwa solemba mara mbili na tuzo juu #MchepukoUsioNaAKili #MweweWaMwaka,” , aliandika Zari Snapchat.


“Kijana, kijana kila siku kijana, kijana na mzuri lakini huwezi kutafuta mwanaume wa kwako mwenyewe….namna chan**doa usivyojiamini, Kama unajiamini na uzuri na akili basi acha tuone mwanaume gani atakutaka baada ya drama hizi, baby daddy 3 loading ukiwa na miaka 20+ atakuwa mjinga pia,” alisema Zari kupitia ujumbe huo.
Zari akaongeza “sio wewe cha***doa uliyelia social media ukidai Lulu kakuibia bwana’ko lakini umegeuka kufanya hicho hicho ulicholilia wakati unajua inavyouma, Mungu hawezi kubariki furaha yako juu ya maumivu ya mwanamke mwingine…ng’oo!!!”
“Unaweza kupost picha zote za nyuma ukiwa nae, lakini tayari nimekwisha msamehe makosa yake yaliyopita. Siwezi kubadilisha historia….nimechukulia kawaida naendelea kujenga maisha yangu ya kesho. Uchawi wote unaisha nguvu na sasa anarudi kwa akili zake kumrudia,” amesema Zari na
Read More

Friday, March 17, 2017

Maua Sama atokwa na haya Baada ya kutoa Video yake mpya

12:52:00 AM 0
Mwanadada anayetamba na ngoma ya Main Chick, Maua Sama amesema yeye hategemei 'kiki' ili ku-'hit' bali uzuri wa kazi zake, na kuwataka wasanii wengine waache kutafuta 'kiki' ili kupata majina bali wajikite kwenye kutengeza kazi nzuri.


Akizungumza leo kwenye Planet Bongo ya East Africa Radio, Maua amesema kuwa wasanii wengi wamejikita kwenye kutafuta kiki badala ya kuwapa mashabiki ladha tofauti na kusisitiza kwamba dhana ya kiki inapaswa kufutika ili kila mtu afanye kazi nzuri.

"Ukifanya muziki mzuri lazima tu utapata jina, wala hakuna haja ya kiki, mfano mzuri mimi hapa ni msanii ambaye nimepata sapoti nzuri sana kwenye 'game' bila kuongelewa kwa mambo mabaya ya kiki, 'The real deal is good music' siyo skendo, japo mimi nina skendo ya kutoa ngoma kali siku zote". 
 Maua aliwaambia Dullah na Jay R watangazaji wa kipindi hicho.
Sama ameongeza kwamba katika muziki wapo wasanii ambao wanafanya muziki mbaya lakini wanapewa nafasi kubwa ya kusikilizwa kutokana na kiki lakini hana chuki nao kwani pia watu wa aina hiyo wana mashabiki zao wanaopenda kuwasikiliza.

"Mimi nina wivu wa maendeleo sana, lakini sina chuki na watu wanaofanya muziki mbaya kwani hata wao wana masoko yao na wanauza ila kinachotokea kwangu nikimuona mtu katoa kazi mbaya mimi naingia kutengeneza 'hits' kali ili nipate soko zaidi".  aliongeza Maua.

Hata hivyo Maua ameongeza kuwa msanii yoyote ambaye huandika nyimbo zake kipindi anapokuwa kwenye hisia yoyote ni wazi wimbo huo ukiachiwa hewani lazima uwe mkali kwa kuwa unakuwa umebeba uhalisia na hisia za kweli.


Read More

Post Top Ad

Your Ad Spot