Upotevu wa
mazao husababisha nchi kutokuwa na uhakika wa chakula na kipato cha wakulima
hupungua na hivyo huchangia pato la Taifa hushuka. Hata hivyo Serikali kwa
kushirikiana na wadau mbalimbali kutoka ndani na nje ya nchi imekuwa ikifanya
jitihada za kupunguza upotevu wa mazao nchini kupitia program na mipango
mbalimbali.
Mradi wa Mifuko
ya PICs ililetwa nchini Tanzania mwezi Julai mwaka 2014 na Chuo Kikuu cha
Purdue - Indiana, Marekani kwa kushirikiana na kiwanda cha PPTL kilichopo Tanga,
ambacho kina uwezo wa kuzalisha mifuko 2,400,000 kwa mwaka. Toka Julai mwaka
2014 hadi Mei 2016 mifuko 470,000 imeshatengenezwa na
kusambazwa katika maeneo mbalimbali nchini.
No comments:
Post a Comment