Kocha
wa Simba, Joseph Omog mjanja sana kwani amewaambia viongozi wa Simba
ana nafasi tatu za wachezaji ambao anataka wamuongezee nguvu kikosini.
Mmoja
wa mabosi wa Kamati ya Utendaji ya Simba ambayo ndiyo ya kwanza kuona
ripoti ya kocha, amesema kwamba, anataka wamsajilie kipa, beki na
straika mmoja.
Katika
ripoti yake, Omog ametoa sifa tu za wachezaji anaowataka huku akiacha
zoezi la kuwasajili kwa viongozi lakini akasisitiza hahitaji straika
kutoka nje ya nchi kwani atapata presha kama ilivyo kwa waliopo.
Simba
ina mastraika Laudit Mavugo raia wa Burundi na Fredrick Blagnon wa
Ivory Coast ambao bado hawajaonyesha uwezo mkubwa katika Ligi Kuu Bara
katika mechi 15 za Simba.
Kabla
ya kuiona ripoti ya Omog, baadhi ya viongozi wa Simba ambao wameona
Mavugo na Blagnon walivyochemsha, wakaanza mipango ya kumrejesha
kikosini Emmanuel Okwi kutoka SønderjyskE ya Denmark.
“Kutokana
na ripoti ya Omog, sasa hatuna tena mpango wa kumsajili Okwi kwani
itakuwa kinyume na matakwa ya kocha hivyo tunaendelea na mambo mengine
kwa kufuata anachotaka yeye (Omog).
“Tulidhani
Okwi akija atafanya vizuri moja kwa moja kwani anaijua ligi yetu,
lakini kocha ameshikilia msimamo wake wa kutaka straika kutoka ndani ya
nchi, hatuna jinsi tunafuata kile alichosema,” alisema bosi huyo.
Licha
ya viongozi wake kutokuwa tayari kuweka wazi kuhusu usajili wa straika
mzawa, gazeti hili linafahamu Simba inamfukuzia Victor Hangaya wa
Prisons ili iweze kumsajili.
SOURCE: CHAMPIONI
No comments:
Post a Comment