Miss Universe Tanzania 2016 apatikana - MUANGALIZI

Hot

Post Top Ad

Your Ad Spot

Saturday, November 26, 2016

Miss Universe Tanzania 2016 apatikana

 
Aliyekuwa Mshindi wa Miss Universe Tanzania 2014 akipongezwa na baadhi ya mashabiki waliojitokeza kushuhudia mashindano hayo, Picha na Maktaba.

MLIMBWENDE Johan Dimack Kutoka arusha usiku wa kuamkia jana amefanikiwa kuibuka mshindi katika Mashindano ya Miss Universe Tanzania nakupata zaidi ya sh.mil tatu ambazo atakuwa anapewa Kwa awamu.

Mshindi wa pili katika mashindano hayo ni mwanadada Liliani Love mwenye Asili ya kimasai huku nafasi ya mshindi wa Tatu ikinyakuliwa na Liliani Felix Kutoka Ilala Dar Es Salaam ambapo pia amepata nafasi ya kuutangaza utalii Kwa maana Miss Tourism.

Akizungumza Mara baada ya kutangazwa mshindi  Dar Es Salaam jana Mlimbwende Dimack alisema kwanza anamshukuru Mungu Kwa kufika alipofika huku akikiri kuwa Mchuano ulikuwa Mkali sana Kwa maana kila mrembo alikuwa mkali.

"Kwakweli naweza kusema siamini kama mimi ndio mshindi kwani wenyewe mmeona warembo wote waliokuwa wameshiriki ni wakali lakini na mshukuru Mungu na majaji Kwa kuniona mimi ndio Mrembo."alisema mlimbwende huyo.

Aidha mwanadada huyo ambae pia aliweza kujieleza Kwa ufasaha tena wa lugha ya kiingereza baada ya kuulizwa swali na moja ya majaji hao,kwamba anadhani amekosewa kuwa mwanamke alisema anajivunua kuzaliwa mwanamke na wala hajutii.

Naye mshindi wa pili na watatu Liliani Felix alisema kuwa anaamini amefanya vizuri ukizingatia kwamba ndio mara yake anashiriki ukilinganisha na wengine ambao waliwahi kushiriki.

"Naweza kusema nimeridhika kwa kushika nafasi ya tatu kwani si haba ukizingatia ndio kwaza nashiriki mashindano haya lakini kikubwa zaidi nimepata nafasi ya kuwa Miss Tourism hivyo bado nitaitangaza nchi yangu "alisema Liliani Felix.

Kwaupande wake Mkurugenzi na Mwandaaji wa Mashindano hayo ya Miss Universe Tanzania Maria Sarungi alisema mashindano Kwa mwaka huu yamekwenda vizuri na mshindi amepatikana kihalali.

Alisema kuwa baada ya mshindi kupatikana Kazi hiyo inaaza upya Kwa maana katika kuhakikisha mshindi huyo na wezake wanakwenda kuchuana na wengine Duniani katika nchi ambayo wataambiwa mapema wiki ijayo.

"Tunashukuru Mashindano yamemalizika lakini Kwetu kama waandaaji naweza kusema ndio Kazi inaaza upya Kwa maana tunajukumu kubwa la kumwandaa mrembo wetu ili na sisi tukapambane na sio kushiriki na Hii ni Kwa wote Kwa maana hata hawa washindi wa pili na watatu pia watawakilishi nchi."alisema Maria

Aidha mbali na ushindi huo Maria alisema Mshindi wa kwaza Jihan Dimack atapewa Zawadi ya sh.mili tatu  lakini Kwa awamu kadri atakavyokuwa anashiriki,mshindi wa pili sh.mil.moja na mshindi wa tatu  sh.laki tano na atawakilishi nchi Kwenye mashindano ya Miss Tourism.

Pia aliwapongeza majaji ambao wengi wao walitoka nje ya Tanzania Kwa Kazi nzuri waliyoifanya kwani walionesha umahili mkubwa katika kazi yao.

Jumla ya walimbwende kumi Kutoka mikoa tofauti walinyukana katika mashindano hayo ya Miss Universe 2016  ambapo Jihan Dimack ndio ameibuka mshindi.

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Your Ad Spot