Msanii wa muziki Bongo, Aslay amesema si vizuri kufananishwa na Rich Mavoko kwani ni msanii ambaye amemtangulia katika muziki.
Muimbaji huyo amesema Rich Mavoko amekuwa akifanya vizuri kila siku, hivyo mashabiki wanaomshindanisha wanakosea.
“Huwezi kunishindanisha na Rich Mavoko, yule ni kaka yangu halafa anafanya vitu vikubwa, nimemkuta kwenye muziki na amefanya vitu vikubwa, kwa ukisema unanishindanisha na Rich Mavoko utakuwa unakosea,” Aslay ameiambia Bongo5.
Katika hatua nyingine Aslay ameeleza sababu ya yeye kuwa miongoni mwa wasanii ambao ngoma zao zinapata views zaidi katika mtandao wa YouTube.
“Ni mashabiki wangu wa kweli ndio maana unakuta hata nikitia ngoma leo kesho unakuta nina laki moja, kwa hiyo siwezi kusema labda nilikuwa nashindana au nina vitu vikubwa sana navifanya niwe na views wengi YouTube ni mashabiki zangu kunipenda kweli,” amesema.
No comments:
Post a Comment