![]() |
Kocha wa Real Madrid Zinedine Zidane |
Miamba hao wa soka waliocheza mechi 40 bila kufungwa wameingia katika rekodi nyingine ya kufungwa michezo miwili mfululizo huku wa kwanza wakifungwa na Sevilla katika mchezo wao uliopigwa jumapili iliyopita.
Celta Vigo ndio walikuwa wa kwanza kupata goli kupitia kwa mshambuliaji wa zamani wa Liverpool Lago Aspas mnamo dakika ya 16 huku madrid wakisawazisha bao lao kupitia Marcelo Vieira kabla ya kuongezwa dakika chache baadae.
Katika mchezo huo uliokuwa wa ushindani mkubwa Mfaransa Karim Benzema alipoteza nafasi nzuri mara baada ya kombora lake kupaa juu ya goli zikiwa zimesalia dakika nane mechi hiyo kumalizika.
Mechi ya marudiano kati ya Madrid na Celta Vigo inatarajiwa kuchezwa Galicia Jumatano wiki ijayo.
No comments:
Post a Comment