Aboutrika atajwa orodha ya magaidi Misri - MUANGALIZI

Hot

Post Top Ad

Your Ad Spot

Thursday, January 19, 2017

Aboutrika atajwa orodha ya magaidi Misri

Msahambuliaji wa zamani wa Misri, Mohamed Aboutrika
MAMLAKA za usalama za Nchi ya Misri zimemweka mchezaji wa zamani wa soka wa timu ya taifa ya nchi hiyo pamoja na Al Ahly, Mohamed Aboutrika katika orodha ya magaidi baada ya kuhusishwa na kikundi cha waislam wa Brotherhood.

Aboutrika anashutumiwa kuwasaidia kifedha kikundi cha  Brotherhood, ambacho mamlaka za Misri kimewaweka kwenye kundi la magaidi kutokana na matukio mbalimbali wanayoyafanya.

Mnamo mwaka 2012, Aboutrika alimpigia kampeni ya urais, Rais wa zamani wa nchi hiyo Mohamed Morsi, ambaye ni mwanachama wa Brotherhood.

Kwa mujibu wa sheria mbalimbali za Misri, mtu yoyote anayewekwa kwenye listi ya ugaidi, hufungiwa kusafiri na passport yake pamoja na mali zake hushikiliwa.

Kwa upande wake Mwanasheria wa Aboutrika, Mohamed Osman, alisema mteja wake hajatiwa hatiani wala hajapewa taarifa rasmi juu ya mashtaka wanayomtuhumu juu yake.

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Your Ad Spot