MUANGALIZI: KITAIFA

Hot

Post Top Ad

Your Ad Spot
Showing posts with label KITAIFA. Show all posts
Showing posts with label KITAIFA. Show all posts

Thursday, March 1, 2018

Dk Shein awaapisha mawaziri, wakuu wa wilaya

3:00:00 AM 0
 
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dk Ali Mohamed Shein leo Machi 1, 2018 amewaapisha viongozi aliowateua jana Februari 28, 2018 kushika nyadhifa mbalimbali katika Serikali ya Mapinduzi Zanzibar (SMZ).
Taarifa iliyotolewa na Ikulu Zanzibar leo, inaeleza kuwa hafla hiyo imefanyika Ikulu mjini Zanzibar na kuhudhuriwa na viongozi mbalimbali wa Serikali.
Baadhi ya viongozi hao ni Makamu wa Pili wa Rais, Balozi Seif Ali Idd; Spika wa Baraza la Wawakilishi,  Zubeir Ali Maulid; Jaji Mkuu wa Zanzibar, Omar Othman Makungu; Mwanasheria Mkuu wa Zanzibar,  Said Hassan Said; mawaziri, naibu mawaziri na wakuu wa mikoa.
Walioapishwa ni Waziri wa Biashara na Viwanda Balozi, Amina Salum Ali;  Waziri wa Vijana, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Balozi Ali Abeid Karume; Waziri wa Ujenzi, Mawasiliano na Usafirishaji na Dk Sira Ubwa Mamboya.
Wengine ni Waziri wa Afya, Hamad Rashid Mohamed; Waziri wa Kilimo, Maliasili, Mifugo na Uvuvi,  Rashid Ali Juma; Waziri wa Ardhi, Nyumba, Maji na Nishati, Salama Aboud Talib; Waziri wa Habari, Utalii na Mambo ya Kale, Mahmoud Thabit Kombo pamoja Waziri wa Kazi, Uwezeshaji, Wazee, Wanawake na Watoto, Maudline Cyrus Castico.
Pia wamo Naibu Waziri wa Ardhi, Nyumba, Maji na Nishati, Juma Makungu Juma;  Naibu Waziri wa Habari, Utalii na Mambo ya Kale, Choum Kombo Khamis; Naibu Waziri wa Kazi, Uwezeshaji, Wazee, Wanawake na Watoto, Shadia Mohamed Suleiman; Naibu Waziri wa Kilimo, Maliasili, Mifugo na Uvuvi, Dk Makame Ali Ussi na  Naibu Waziri wa Biashara na Viwanda, Hassan Khamis Hafidh.
Pia, Dk. Shein amewaapisha wakuu wa wilaya aliowateua ambao ni  Issa Juma Ali (Mkoani-Pemba) na Rajab Ali Rajab wa Kaskazini B, Unguja.
Viongozi walioapishwa wameahidi kuendelea kumsaidia Rais Dk. Shein katika kuhakikisha Zanzibar inazidi kupata maendeleo, kuimarisha ushirikiano na kuwatumikia wananchi.
Pia, wameahidi kuleta mabadiliko na kufanya kazi kwa vitendo sambamba na kuendelea kusimamia amani na utulivu uliopo nchini.
Jana, Dk Shein alifanya mabadiliko madogo katika Baraza la Mapinduzi kwa kuongeza wizara moja zaidi na kuwabadilisha wizara baadhi ya Mawaziri.
Kufuatia mabadiliko hayo, shughuli za vijana zimehamishiwa katika Wizara mpya ya Vijana, Utamaduni, Sanaa na Michezo shughuli za mazingira zimehamishiwa katika Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais na shughuli za Wakala wa Serikali wa Uchapaji zimehamishiwa Wizara mpya ya Habari, Utalii na Mambo ya Kale.
Aidha, amewateua naibu mawaziri wapya wawili na kumbadilisha wizara naibu waziri mmoja ambapo kufuatia mabadiliko hayo, SMZ hivi sasa ina wizara 14.
Read More

Tuesday, January 30, 2018

LIVE VIDEO: JPM Azindua Hati za Kusafiria

10:42:00 PM 0
Tazama hapa chini Video Rais John Magufuli Akizindua hati za kusafiria.


Read More

Saturday, January 27, 2018

Thursday, January 25, 2018

Afariki dunia Baada ya Kutoa Sadaka

12:49:00 AM 0

WAUMINI wa Kigango cha Muze, Parokia ya Zimba Kanisa Katoliki Jimbo la Sumbawanga waliofurika kanisani kwa ibada ya misa ya Jumapili walipatwa na taharuki kubwa huku ibada ikisimama kwa muda baada ya mwanakwaya kupoteza fahamu muda mfupi baada kutoa sadaka.

Mwanakwaya huyo akiwa na ujauzito wa miezi mitano aitwaye Flora Nandi (25) akiwa mwanakwaya wa Kwaya ya Mtakatifu Cecilia alifariki dunia akiwa anakimbizwa kupatiwa huduma katika zahanati iliyopo katika kijiji cha Muze katika Bonde la Ziwa Rukwa wilayani Sumbawanga.


Mkasa unaofanana na huu ulitokea miezi sita iliyopita pale mkazi wa Mtaa wa Makanyagio katika Manispaa ya Mpanda mkoani Katavi, Beatrice Kangu (48) alifikwa na umauti muda mfupi baada ya kutoa sadaka katika ibada ya Jumapili iliyofanyika katika Kigango cha Kanisa Katoliki Jimbo la Mpanda kilichopo katika Mtaa wa Makanyagio B.
source: Tanzania Today
Read More

Daktari wa Olympic ahukumiwa Miaka 175 Jela

12:42:00 AM 0

Aliyekuwa Daktari wa timu ya taifa ya akina dada ya michezo ya kuruka hewani nchini Marekani Larry Nasser, amehukumiwa kifungo cha miaka 175 jela. Nasser mwenye umri wa miaka 54, amepewa adhabu hiyo baada ya kupatikana na makosa 10 ya kuwanyanyasa kimapenzi mamia ya wanamichezo wa kike, ambao walijitokeza kutoa ushahidi.
Wasichana na wanawake 160, walijitokeza kutoa ushahidi dhidi ya daktari huyo ambaye juhudi zake za kuomba radhi hazikuzaa matunda.

Jaji Rosemarie Aquilina amesema daktari huyo ni mtu hatari.
“Najisikia fahari na furaha kubwa kutoa adhabu hiyo kutokana na kitendo alichofanya Nasser na nataka iwe fundisho kwa wengine, “ Jaji Rosemary Aquilina ameiambia mahakama.
Takriban wasichana 140 wamewasilisha kesi dhidi ya Nasser, taasisi ya USA Gymnastics na chuo kikuu cha MSU, wakidai kuwa taasisi hizo mbili zilipokea tuhuma za unyanyasaji wa kingono dhidi ya daktari huyo miaka kadhaa ya nyuma.
Wakati huo huo mkuu wa chuo kikuu cha jimbo la Michigan (MSU) alikokuwa anafanya kazi Nasser kati ya mwaka 1997 na 2016, amejiuzulu.
Lou Anna Simon amekuwa akikabiliwa na shinikizo kujiuzulu.
Read More

Thursday, December 28, 2017

Awaua watoto wake wawili kwa sumu

6:45:00 AM 0
KIAMBU, KENYA: Jeshi la Polisi linamshikilia Mwanaume mmoja aliyewaua Watoto wake wawil 2 na yeye kunywa sumu ambayo haikumuua.

Watoto hao waliouawa
mmoja alikuwa na miaka 7 na mwingine miaka 3

Inadaiwa kuwa siku moja kabla ya Sherehe ya Christmas familia hiyo ilisafiri hadi Narumoru ambako Mama wa Watoto hao alibakia huko kwasababu ambazo hazijajulikana.
Read More

Msigwa awapa hongera Kakobe, Gwajima

5:35:00 AM 0
 
Mbunge wa Iringa Mjini kwa tiketi ya (CHADEMA) Peter Msigwa amefunguka na kuwapongeza baadhi ya viongozi wa dini akiwepo Askofu Zakaria Kakobe, Askofu Josephat Gwajima, Askofu Benson Bagonza kwa kile walichofanya kukemea baadhi ya matendo ya serikali

Mchungaji Msigwa ameweka wazi kuwa hicho kilikuwa kilio chake kikubwa kwa viongozi wa dini kwani Tanzania inapaswa kujengwa na watu wote na si wanasiasa tu

"Nawapongeza sana baadhi ya viongozi wa dini kama vile Askofu Kakobe, Askofu Gwajima, Askofu Bagonza na Shayo ambao kwa namna moja kimekuwa kilio changu kikubwa pamoja na wananchi wengine kuona viongozi wa dini wanakuwa kimya wakati mambo hayaendi vizuri, Kwa kifupi niwapongeze sana kwa sababu nchi hii inajengwa na sisi sote na mali yetu sote" alisema Msigwa

Aidha Mchungaji Msigwa aliendelea kusema kuwa yeye amesikitiswa na baadhi ya vijana wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) ambao wanataka kulifanya Taifa la Tanzania lisiwe la watu wa kufikiri

"Hoja alizotoa Askofu Kakobe zinafafanua vizuri na kuwafanya watu wafikiri na kujibu kwa hoja lakini watu wameanza kumshambulia kwa kejeli na maneno ambayo si ya kiugwana, hoja siku zote hujengwa kwa hoja hakuna mtu ambaye yupo juu ya sheria, Kakobe alimuomba Mhe. Magufuli akatubu kwamba anaiendesha nchi kama vile nchi ya chama kimoja" Alisisitiza Msigwa
Read More

Saturday, March 18, 2017

JPM Azima kiki kwa Viongozi

2:57:00 AM 0
KAMA kuna waziri au kiongozi yeyote anataka kutoa taarifa yenye kuwagusa wananchi moja kwa moja, ni dhahiri kuwa sasa atalazimika kujiridhisha zaidi.


Aidha, waziri na viongozi wengine wanatakiwa pia kuzingatia dhana ya uongozi wa pamoja kwa kuwahusisha wenzao na pia kupata maoni ya wataalamu katika wizara au taasisi wanazoziongoza kabla ya kulifikisha kwa umma.

Vinginevyo, mawaziri wajiandae kushuhudia maagizo yao yakitenguliwa huku pia wakijiweka katika hatari ya kufikiriwa kuwa wanafanya hivyo kwa minajili ya kutumia matamko yao kama ‘kiki’ za kuwaonyesha kuwa wanafanya kazi vyema na kwa kasi inayosisitizwa na Serikali ya awamu ya tano.

Angalizo hilo limetolewa na baadhi ya wachambuzi wa amsuala ya kisiasa walizoungumza na Nipashe kuelezea mkasa uliomkuta Waziri wa Sheria na Katiba, Dk. Harrison Mwakyembe, ambaye agizo lake la kuzuia ufungishaji ndoa kwa watu wote wasiokuwa na vyeti vya kuzaliwa lilifutwa na Rais John Magufuli kwa kuonekana kuwa litawaathiri mamilioni ya Watanzania wasiokuwa na vyeti hivyo.

Baadhi ya wachambuzi walidai kuwa Mwakyembe siyo waziri au kiongozi wa kwanza kutoa taarifa zilizomlazimu Rais Magufuli kuingilia kati kwa manufaa ya Watanzania na hivyo, wanapaswa kujua kuwa wana wajibu mkubwa kwa taifa na kutakiwa wajiepushe na matamko binafsi yasiyofanyiwa kazi kwa kina kabla ya kutolewa kwa umma.

“Ni vizuri kwa kila waziri au kiongozi yeyote yule kujipa uhakika wa kila tamko na amri wanazotaka kutoa kwa umma…kwa mfano, ni lazima wahakikishe kwamba wanazingatia sheria na pia wanayoyasema ni kwa maslahi ya umma mpana wa Tanzania.

“Vinginevyo, matamko yao yataendelea kuibua maswali na Rais hatakubali wamharibie kwa sababu ameshasema mara kadhaa kuwa daima atakuwa upande wenye maslahi kwa wananchi wake, na hasa wanyonge,” alisema mmoja wa wachambuzi hao.

“Ni vizuri wakaachana na matamko yenye viashiria vya kuwa na kiki za kuonyesha kuwa nao wako vizuri kuendana na kasi ya serikali ya sasa...wasipozingatia hayo kila mara watajikuta wakiwa tofauti,” mwingine aliongeza.

Neno ‘kiki’ ni la mtaani na limejitwalia umaarufu katika siku za hivi karibuni, likitumiwa kumaanisha mbinu zinazoweza kutumiwa na mtu ili kujipatia umaarufu juu ya jambo fulani. Wasanii na wanasiasa huhusishwa zaidi na neno hilo kutokana na asili ya kazi zao ambazo huwakutanisha zaidi na watu.

Awali, katika agizo lake hilo ambalo alilisisitiza pia jana asubuhi wakati akizungumza na kituo kimoja cha redio jijini Dar es Salaam, Mwakyembe alisema wameamua kuzuia ndoa kwa watu wasiokuwa na vyeti vya kuzaliwa kwa nia ya kuondokana na takwimu za sasa zinazoonyesha kuwa Tanzania Bara ni ya mwisho barani kwa utoaji wa vyeti vya kuzaliwa kwa wananchi wake.

Alisema ni asilimia 12 tu ya Watanzania walioko Bara ndiyo wenye vyeti vya kuzaliwa na kuzidiwa hata na Zanzibar yenye wastani wa asilimia 75, hali aliyosema inashangaza kwa sababu bei ya vyeti hivyo ni Sh. 3,500 tu huku gharama za harusi zikiwa kubwa kulinganisha na kiasi hicho.

Hata hivyo, akizungumza na waandishi wa habari muda mfupi kabla ya kuondoka mjini Dodoma na baadaye taarifa yake kusambazwa kwa umma jana, Rais Magufuli alisema anatengua uamuzi huo wa Waziri Mwakyembe kwa sababu utawanyima fursa ya kuoana Watanzania ambao wengi wao hawana vyeti hivyo vya kuzaliwa, hasa wale wa vijijini.

Alisema hadi sasa idadi ya Watanzania walio na vyeti vya kuzaliwa ni chini ya asilimia 20 huku wengi wao wakiwa ni wananchi waishio vijijini ambako ni vigumu kupata vyeti hivyo, na wengine wakiwa ni waliozaliwa kabla ya kuanza kutolewa kwa vyeti vya kuzaliwa nchini mwaka 1961.

“Kwa hiyo ndugu zangu Watanzania msiwe na wasiwasi wowote, endeleeni na utaratibu wenu wa kuoa na kuolewa kama kawaida na kama kuna kifungu chochote cha sheria kinachomlazimisha mtu awe na cheti cha kuzaliwa ndipo aoe ama aolewe nitamuelekeza Waziri wa Katiba na Sheria Mhe. Harrison Mwakyembe apeleke Bungeni kikarekebishwe” alisema Rais Magufuli, huku akitoa wito kwa wanasheria kuziangalia vizuri sheria zinazohusiana na kuzaliwa na kifo na kuoa na kuolewa ili zisilete mkanganyiko kwa wananchi.

JPM ALIVYOZIMA ‘KIKI’
Mbali na tukio la kuzimwa kwa ‘kiki’ ya Waziri Mwkayembe jana, wapo pia mawaziri na viongozi wengine kadhaa wa serikali na taasisi za umma waliokumbana na rungu la Magufuli la kutengua amri au tarifa zao. Hao ni pamoja na Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Walemavu, Jenista Mhagama; Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (Tamisemi), George Simbachawene na Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Nape Nnauye.

Mhagama alikumbana na mkasa huo Machi 3, 2016 wakati alipotoa taarifa ya kumteua Dk. Carina Wangwe kuwa Kaimu Mkurugenzi wa Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF). Hata hivyo, wakati uamuzi wake ukimpa umaarufu siku hiyo kupitia ‘kiki’ za kwenye mitandao ya kijamii, waziri huyo alilazimika kubatilisha taarifa hiyo kabla Rais Magufuli hajamtangaza Prof. Godius Kahyarara kushika nafasi hiyo NSSF.

Agosti 12 mwaka jana, Simbachwene alisisitiza kuondolewa kwa wamachinga maeneo ya mijini. Hata hivyo, siku chache baadaye, Magufuli alitengua agizo hilo wakati akihutubia jijini Mwanza kwa kutaka wamachinga wasiondolewe kwenye maeneo wanayofanyia biashara hadi pale mamlaka husika zitakapohakikisha kuwa zimewatafutia sehemu za kwenda kufanyia biashara zao.

Waziri mwingine aliyekumbwa na rungu la Magufuli hivi karibuni wakati kauli yake ikiwa imepamba moto na kuibua mijadala kwenye mitandao ya kijamii ni Nape.

Machi Mosi mwaka huu, Nape alielezea umuhimu wa kulinda majina ya wasanii waliotajwa hadharani wakituhumiwa kuhusika na dawa za kulevya, akisema kwamba ni vyema kuzingatia nguvu kubwa walizotumia kujijengea majina hayo na kwamba, ifikiriwe pia ni kwa namna gani watasafishwa ikiwa wataonekana baadaye kuwa hawahusiki na dawa za kulevya.

Nape alizungumza hayo akiwa Dodoma na baadaye kwenye kipindi cha Dakika 45 kinachorushwa na ITV kuelezea hatua iliyochukuliwa na Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda, aliyetangaza hadharani majina ya wasanii kadhaa katika orodha yake ya awali ya watuhumiwa 65 wa dawa za kulevya.

Hata hivyo, siku chache baadaye, Magufuli alionekana kupinga maelezo ya Nape kwa kusisitiza kuwa vita dhidi ya dawa za kulevya isiangalie majina ya watu kwa sababu athari zake ni kubwa kwa taifa.

WALICHOSEMA WABUNGE, WASOMI WANENA
Akizungumzia suala la Mwakyembe, Mbunge wa Kibamba, John Mnyika (Chadema), alisema ni ishara kuwa baadhi ya mawaziri na viongozi wengine wamekuwa wakikurupuka kwa kutoa matamko bila kuyafanyia utafiti wa kina na ndiyo maana Magufuli ametengua agizo alilotoa kuhusu amri ya kuzuia ndoa kwa wasiokuwa na vyeti vya kuzaliwa.

Mbunge wa Busega, Dk. Raphael Chegeni (CCM), alisema awali alikuwa haamini na mwishowe akajikuta akisikitika kusikia tamko la Waziri Mwakyembe kuhusu zuio la ndoa kwa wasiokuwa na vyeti vya kuzaliwa kwa sababu agizo lake halikuwa na msingi wa kisheria.

Alisema kupitia mkasa huo wa Mwakyembe, mawaziri wanatakiwa kuwa makini katika kutoa matamko ya aina hiyo na kwamba, kama wana hoja wanatakiwa kupeleka ndani ya Bunge ili ijadiliwe.

“Kama unatoa tamko leo na Rais analipinga ama kulifuta, hiyo inaonyesha kuwa waziri umekurupuka… matamko kama haya yanamgombanisha Rais na wananchi wake. Mawaziri wajiepusha kutoa matamko ambayo hayajapewa ridhaa,” alisema Chegeni.

Mbunge wa Nzega Mjini (CCM), Hussein Bashe, alisema alichokifanya Rais Magufuli kutengua tamko hilo yupo sahihi kwa kuwa suala la ndoa linagusa imani ya mtu na serikali haitakiwi kuingilia, na kwamba kama kuna jambo la kisheria liwasilishwe bungeni ili lifanyiwe kazi.

Mhadhiri wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM), Dk. Richard Mbunda, alisema inavyoonekana, huenda tangazo alilitoa Mwakyembe ni binafsi kwa mtazamo wake baada ya kuona kuna udanganyifu mkubwa katika eneo hilo.

Mkurugenzi wa Kituo cha Sheria na Haki za Bindamu (LHRC), Dk. Hellen Kijo-Bisimba alisema agizo la Mwakyembe kuhusu masuala ya ndoa linashangaza kwa sababu halipo kwa mujibu wa sheria

“Katika Sheria ya Ndoa, vitu ambavyo mtu anatakiwa kuwa navyo ili afunge ndoa ama sifa, hiyo ya cheti (cha kuzaliwa) haipo… sijui huyo Waziri ameitoa wapi na pia ingekuwepo kisheria ingepingwa kwa sababu watu wengi hawana vyeti vya kuzaliwa,” alisema Bisimba.

Mhadhiri wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Dk. Ally Bashiru, alisema ni vyema Rais Magufuli ameingilia na kutengua agizo la Mwakyembe la kuzuia ndoa kwa asiokuwa na vyeti vya kuzaliwa.
Read More

Tuesday, January 31, 2017

Matokeo ya Kidato cha NNE 2016

Friday, January 27, 2017

Amuua Mke wake kisa Upoteza wa Mia 200

1:29:00 AM 0
Mkazi wa kijiji cha Mwamgongo mkoani hapa Zubeda Said (33) anadaiwa kupigwa na mumewe hadi kuuawa baada ya kupoteza fedha yenye thamani ya shilingi 200.

Akizungumza na waandishi wa habari mjini hapa jana, dada wa marehemu, Siwema Masoud alidai kuwa awali ndugu yake huyo alimpigia simu kuwa Januari 19 usiku alipigwa na mumewe kwa kupotea Sh 200.

Alisema siku moja kabla alimpa mtoto wa kaka yake mwenye umri wa miaka mitano Sh 200 akanunue maandazi, lakini mtoto huyo aliporwa fedha hiyo na wenzake, akashindwa kurudi nyumbani kwa siku mbili, akarudi siku ya ugomvi wa wawili hao na mumewe kukasirika. 

Alidai kuwa mume huyo, Kunduwenda Kiza (37) akimfokea mtoto huvyo mama mtu kuamua kumwomba radhi mumewe huyo lakini bila mafanikio kwani katika hali ya kushangaza mumewe alimpiga mpaka kupoteza fahamu.

Siwema asilimulia kuwa kesho yake saa 9.45 alfajiri hali ya Zubeda ilibadilika na  kutokwa damu sehemu mbalimbali zilizo wazi mwilini mwake, mumewe akamkimbiza kwenye zahanati ya kijiji hicho na Januari 20, alipewa rufaa kwenda hospitali ya mkoa ya Maweni.

Alisema  Januari 21, saa 12.45 Zubeda alipoteza maisha hali iliyowapa mashaka na kufikisha taarifa Polisi  kwa uchunguzi wa maiti lakini walipokwenda na askari hospitalini wakaambiwa jalada halionekani.

Hata hivyo, mganga aliyetambuliwa kwa jina la Dk Muganyizi alijitolea na kuufanyia uchunguzi mwili huo na baada ya uchunguzi maiti alibaki mochari.

Lakini wakati ndugu wakijiandaa kwenda kuchukua mwili walishangaa kukuta umeondolewa, na kwa msaada wa polisi waliukamata ukisubiri kusafirishwa kinyemela.

Mwandishi alifika Maweni na kugundua kuwa kabla ya kifo alilazwa wodi 2(b) ya wanawake huku jalada lenye taarifa zake likiwa limetoweka huku uchunguzi wa Mganga ukibaini kuwa na majeraha ndani ya mwili yaliyosababisha kuvuja damu kulikochangia kifo hicho.

Kamanda wa Polisi wa Mkoa, Ferdinand Mtui  alikiri kupokea taarifa za kifo cha kutatanisha cha Zubeda.

Kamanda Mtui alisisitiza kuwa mshukiwa Kiza anashikiliwa na Polisi   kwa upepelezi na ikibainika ametenda kosa hilo, atafikishwa mahakamani.
Read More

Monday, January 23, 2017

ANGALIA LIVE ZIARA YA RAIS WA UTURUKI NCHINI TANZANIA

Rais RECEP TAYYIP ERDOGAN alivyowasili Nchini

3:22:00 AM 0
Rais wa Uturuki RECEP TAYYIP ERDOGAN akiwa ameambatana na mke wake mama Emine Erdogan akiwa anawasili nchini Tanzania katika uwanja wa kimataifa wa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere jijini Dar es salaam na atakuwa na ziara ya zipatazo siku mbili



Rais wa Uturuki mhe. RECEP TAYYIP ERDOGAN akiwa amepokelewa na Waziri mkuu Mhe. KASSIM MAJALIWA

Read More

Thursday, January 19, 2017

Malizni aula FIFA

7:41:00 AM 0
Rais wa TFF


Shirikisho la Kimataifa la Mpira wa Miguu (FIFA) limemteua Rais wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), Jamal Malinzi kuwa Mjumbe wa Kamati ya Maendeleo ya soka ya FIFA kwa miaka minne ijayo.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa Januari 18, na kusainiwa na Katibu Mkuu wa FIFA, Fatma Samoura imeonesha Malinzi atadumu katika nafasi hiyo kuanzia mwaka huu hadi mwaka 2021.

“Tuna faraja kukufahamisha kuwa umeteuliwa kuwa Mjumbe wa Kamati ya Maendeleo ya FIFA, na tunachukua nafasi hii kukupongeza kwa uteuzi huu na ni imani yetu utatumia vyema muda wako na nguvu zako katika nafasi hii mpya uliyoipata,” ilisema sehemu ya taarifa hiyo.

Taarifa hiyo ilifafanua kuwa Kamati hiyo inayoongozwa na Sheikh Salman Bin Ebrahim Al Khalifa Rais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Bara la Asia, ina majukumu ya kusimamia mipango ya maendeleo ya mpira wa miguu duniani kote.

Imeelezwa wajumbe wengine watakaoteuliwa kujiunga na kamati hiyo watatangazwa kupitia mtandao wa Shirikisho hilo ambao ni www.FIFA.com.

Uteuzi wa Malinzi katika vyombo vikubwa vya maamuzi ya mpira wa miguu vinaendelea kuwa mfululizo kwa watanzania kupata nafasi kubwa katika vyombo muhimu kama FIFA na CAF kwani ikumbukwe mwishoni mwa mwaka jana Shirikisho la Mpira wa miguu Afrika Huu lilimteua Rais Malinzi kuwa mjumbe wa kamati maalum inayoongozwa na rais wa CAF, Issa Hayatou ya kuboresha mfumo wa uongozi shirikisho hilo.

Hata hivyo TFF ilimshukuru Rais Gianni Infantino na kamati yake ya ushauri kwa kumteua Malinzi katika nafasi ya ujumbe katika kamati hiyo muhimu ya maendeleo ya soka ulimwenguni.
Read More

Waziri Mkuu aridhishwa na uwekezaji wa mdau wa SAGCOT

7:38:00 AM 0
Waziri Mkuu wa Tanzania, Kassim Majaliwa

Na Mwandishi Wetu,
WAZIRI Mkuu Kassim Majaliwa amempongeza mdau wa Mpango wa Kuendeleza Kilimo katika Ukanda wa Kusini (SAGCOT) kwa upande wa ufugaji, ASAS Diaries Limited kwa kuwainua wafugaji wadogo wadogo mkoani Iringa.

Akitembelea shamba kubwa la mifugo linalomilikiwa na ASAS jana, Waziri Mkuu Majaliwa aliwataka wawekezaji wengine nchini kuiga mfano wa mwekezaji huyo kwani itasaidia kupunguza migogoro isiyo ya lazima.

“Huu ni mfano mzuri wa uwekezaji ambao unasaidia wafugaji wadogo wadogo wanaomzunguka mwekezaji mkubwa kunufaika kwa soko la uhakika,utaalam na huduma za kijamii pia,” alisema waziri mkuu.

Majaliwa amejionea ufugaji mkubwa wa kisasa katika shamba hilo ambalo lina ng’ombe wa kisasa wa maziwa zaidi ya 1,000  na kuwataka wafugaji wadogo kuchangamkia fursa wanazozipata.

“Wakati sasa umefika kwa Watanzania kupenda bidhaa zinazotengenezwa hapa nyumbani kwani zipo zenye ubora wa hali ya juu,” alisema waziri mkuu na kuongoza kuwa ameridhishwa na uwekezaji kwenye shamba hilo la mifugo la ASAS.

Awali akimkaribisha Waziri Mkuu, Mkurugenzi Mtendaji wa ASAS Diaries Limited,  Fuad Jaffer, alisema kampuni imefanikiwa katika uboreshaji wa mifugo, udhibiti wa magonjwa ya mifugo kuzalisha mitamba na madume bora.

“Tumefanikiwa kuimarisha mahusiano mazuri na jamii kwani Kampuni imeajiri watumishi wengi kutoka maeneo yanayotuzunguka,” alisema  Jaffer.

Mkurugenzi Mtendaji huyo alimwambia waziri mkuu kuwa kiwanda kinasindika lita 14,000 za maziwa kila siku ambayo ni sawa na asilimia 24 ya uwezo wa kiwanda.

Waziri Mkuu alitembelea shamba hilo la ASAS ambaye pia ni mdau muhimu wa SAGCOT, ikiwa njiani kuelekea katika Mkoa wa Njombe.

Kwa upande wake, Mkuu wa Kongani na  Ubia wa Maendeleo wa SAGCOT,   Maria Ijumba, aliwaambia waandishi wa habari kuwa ASAS ni mfano wa kuigwa kwa wadau wa SAGCOT kwenye sekta ya ufugaji.

“Kwa kweli Serikali inapaswa imuunge mkono kwa dhati kwani mchango wake katika jamii zinazomzunguka ni mkubwa sana. ASAS mbali ya kuwasaidia wafugaji wadogowadogo anachangia sana katika maendeleo ya jamii zinazomzunguka,” alisema  Ijumba.

 Ijumba alitoa pia mwito kwa Watanzania kujijengea tabia ya kupenda kunywa maziwa yaliyosindikwa na hasa yalitengenezwa hapa nchini.

“Sisi kama SAGCOT tunafanya kazi kwa karibu na wadau wetu ili wafikie malengo waliyojiwekea,” alisisitiza.

Read More

NASISITIZA JAMBO

7:34:00 AM 0
Waziri wa Maliasili na Utalii, Prof. Jumanne Maghembe, (kushoto) akisistiza jambo kwa wajumbe wa Kamati ya Bunge ya Ardhi, Maliasili na Utalii walipotembelea ofisi za Taasisi ya Utafiti wa Misitu Tanzania (TAFORI) mkoani Morogoro jana. (Picha na Hamza Temba - WMU)

Read More

CWT yashauriwa iache tabia ya kukimbilia mahakamani

7:32:00 AM 0


MWANAHARAKATI wa kutetea haki za elimu nchini, David Msuya, ameshauri Chama cha Walimu Tanzania (CWT) kuangalia zaidi matatizo yanayokumba walimu na kutatua changamoto hizo na si kukimbilia kufungua kesi mahakamani.

Akizungumza kwa njia ya simu na mwandishi wa habari hizi jijini  Dar es Salaam jana, David alisema anatoa ushauri huo  baada ya Mkuu wa Mkoa Mtwara, Halima Dendego, kutoa agizo la kuwavua vyeo walimu wakuu wa mkoa huo kutokana na kushuka kwa elimu mkoani hamu, lakini CWT imepinga ikitishia kwenda mahakamani endapo walimu hao watavuliwa vyeo.

Alisema hatua hizo zisichukuliwe kwa walimu pekee, bali hata kwa maofisa elimu wasiowajibika kwa kuvuliwe madaraka kwani wengi wao hukaa maofisini tu na hawaendi kuona na kuwasikiliza walimu kero zao maofisini.

"Hali hii inadhohofisha sana suala la elimu nchini, wakati mwingine  maofisa wa elimu hawaendi kule mashuleni kusikiliza kero za walimu na hata wakifuatwa maofisini kwao, walimu hawapati nafasi ya kuwaona,"alisema David

Aliitaka Serikali kutowavumilia wafanyakazi wasiowajibika na si kwa walimu pekee bali hata katika taaluma zingine nchini

Aidha, alisema Sheria ya Maadili inasema mwajiri atatimiza wajibu wake kwa kumpatia mwajiriwa wake mshahara kwa kila mwezi na kwa wakati, lakini inaonekana kuwa kinyume kwani Sheria hiyo haitekelezwi

"Matatizo ya walimu ni mengi, changamoto ni nyingi siku hadi siku kama wao Chama cha walimu wanajua kutetea na kushughilikia kero ili  ziishe na si kushabikia mambo,"alisema David

Alisema kuwa CWT inaonekana kuwa mtetezi wa walimu, lakini si kweli.

Aliongeza kuwa Mkuu wa Mkoa  ni sawa na  Rais kwenye eneo lake la utawala, hivyo akitoa tamko kama hilo linapaswa kusikilizwa na kutekeleza.

Alisema ni wajibu wa Tume ya Maadili kusikia agizo hilo na CWT ni wajibu wao kufanyia kazi  kutokana na uzito wa jambo hilo.

"Mimi naunga kauli ya Mkuu wa Mkoa kuhusu kuvuliwa vyeo walimu wakuu na ikiwezekana mpaka kwa maofisa elimu wa Mkoa wa Mtwara ili kuendana na kasi ya Rais John  Magufuli ya Hapa Kazi Tu,"alisema David


mwishooooooooooooooo
Read More
7:15:00 AM 0

Mbarawa  azitaka taasisi kujiunga na kituo cha kumbukumbu.

Waziri wa Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa
Na mwandishi wetu

Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa ameziagiza Taasisi zote za Serikali nchini kuhakikisha zinaleta taarifa zao kuhifadhiwa katika kituo cha Taifa cha Kuhifadhi kumbukumbu cha Kijitonyama (IDC) kwani kituo hicho ni salama na kina ubora wa hali ya juu katika Kanda ya Afrika Mashariki na Kati.

Aidha, alizitahadharisha baadhi ya Taasisi zenye mpango wa kujenga na  kuanzisha vituo vyao vya kuhifadhi kumbukumbu kuacha mara moja mpango huo,  kwani kufanya hivyo ni kuingilia kazi ya kituo hicho na kupoteza fedha za Serikali.

Hayo yalisemwa jijini Dar es salaam na Waziri huyo mara baada yakutembelea kituoni hapo na kupokea taarifa ya uendeshaji wa kituo hicho kutoka kwa Mkuu wa Kituo.

“Sioni sababu kwa Taasisi nyingine kutaka kujenga vituo vyao vya kuhifadhi kumbukumbu, Serikali imeshawekeza fedha nyingi kwa ajili ya ujenzi wa kituo hiki, hivyo taasisi zote nchini zinalazimika kutumia kituo hiki”,  alisema Profesa Mbarawa.

Sambamba na hilo alizisisitiza kampuni zilizo chini ya Wizara yake kuwa mfano wa kuigwa na taasisi nyingine nchini kwa kuwa wa kwanza kuleta taarifa zao kuhifadhiwa katika kituo hicho.

Kwa upande wake, Mkuu wa Kituo hicho Abdul Mombokaleo, alifanunua kuwa hadi sasa wameshafanikiwa kuunganisha wateja 13 kujiunga na kituo hicho na wengine zaidi ya 40 wapo katika mchakato wa kujiunga.

Katika hatua nyingine, Waziri Mbarawa alitembelea ofisi za Kampuni ya Simu Tanzania (TTCL) na kusema kuwa ameridhishwa na utendaji wa kampuni hiyo kutokana na jitihada zake za kuteka soko la ushindani katika kampuni za mawasiliano nchini.

“Nimefarijika zaidi kuona sasa TTCL inafanya vizuri katika eneo la masoko kwani nimeshuhudia matangazo mengi barabarani, kwenye runinga, magazetini na katika mitandao ya kijamii, hii inadhihirisha sasa mna mpango wa kuifufua kampuni hii”, alifafanua Profesa Mbarawa.

Aliutaka uongozi wa kampuni hiyo kuwa wabunifu na kufanya kazi kwa uadilifu na ushirikiano ili kuleta mabadiliko chanya yatakayoboresha kampuni hiyo na kuteka zaidi soko la mawasiliano nchini.
Read More

Hakielimu yazindua Mpango Mkakati wa miaka mitano

7:06:00 AM 0
 Na Mwandishi Wetu

Mhandiri wa Chuo kikuu cha Dar es Salaam, Profesa Kitillya Mkumbuko akizungumza na wadau wa elimu katika moja ya mikutano ya hakielimu

BALOZI wa Sweden Nchini Tanzania Katrina Rangnitt amezindua mpango mkakati wa  miaka mitano  2017/2021 wa Taasisi isiyokuwa ya kiserikali ya Haki Elimu unaojikita katika uboreshaji elimu nchini Tanzania.
Akizindua mpango huo balozi wa Sweden  Rangnitt kwa kushirikiana na  bodi ya taasisi hiyo, alisema kuwa mkakati huo ni kufanya ushawishi kwa serikali  ili iandae na kutekeleza sera ambazo zitakuwa fursa kwa watoto hususani katika kuandikishwa shule, usawa wa elimu jumuishi iliyo bora, inayotolewa kwenye mazingira rafiki na salama kwa wote.
Pia alisema mkakati huo utahakikisha kuwa wananchi wanapata taarifa, wanajipanga kwa  kushiriki katika kutatua changamoto zilizopo katika shule nyingi nchini hususani kwa kufuatilia utawala na utoaji elimu bora.
Kwa upande wake Mkurugenzi mtendaji wa Haki Elimu John Kalage, alisema kuwa mkakati huu wa  miaka mitano ni kuhakikisha  wanashawishi mabadiliko ya  sera na utekelezaji wake.
Alisema elimu ya Tanzania haina falsafa iliyo  wazi hivyo inashindwa kufiki ujumuishaji kamili wa makundi yote na kutoa  matokeo bora ya kujifunza  yenye manufaa kwa wanafunzi.
"Shule  si sehemu salama kwani mtoto mmoja kati ya wawili hukumbana na ukatili ambao umezoeleka kutendwa na walimu hivyo kuna haja ya  kufanya marekebisho zaidi sera ya elimu na kampeni ya kuhimiza utekelezaji makini wa sera ya elimu ya mwaka 2014 ili kuhakikisha upatikanaji wa elimu na ubora wake vinaimarika,"alisema Kallage.
Alisema licha ya juhudi za serikali  zinazoendelea, sekta ya elimu nchini Tanzania bado imesongwa na  changamoto kubwa ambazo ni pamoja na  matokeo duni ya ufundishaji wa wanafunzi, utoro wa Waalimu na uwezo mdogo wa kufundisha na kukosekana kwa  usawa wa kijinsia.
Pia alisema  kushamiri kwa  mfumo tabaka wa elimu ni tatizo kwani watoto wa wenye fedha wachache wanapata elimu bora kwenye shule binafsi na masikini wanaachwa kwenye elimu duni katika shule za serikali.
Aliongeza kuwa kukosekana kwa falsafa na malengo ya elimu vinavyoeleweka kwa kila mtu matokeo yake, elimu ya Tanzania imekosa falsafa na malengo ya kuiongoza.
Naye Mhadhiri wa Chuo kikuu cha Dar es Salaam Profesa Kitillya Mkumbo,alisema serikali inatakiwa kuchukua hatua za muda mfupi za kutatua changamoto za elimu ya msingi kutokana na mfumo ambao siyo bora.
Pia alisema Mtazamo wa serikali kwa vyuo vya ufundi bado msukumo wake ni mdogo, hivyo wanatakiwa kuelekeza nguvu katika vyuo hivyo ili kupata watu wenye ujuzi na kufikia lengo la kuwa na serikali ya viwanda.
Vile vile alisema elimu ya juu hapa nchini  inawalimu wachache  wenye shahada ya uzamivu ambapo ni asilimia 25 tu na chuo Kikuu cha Dar es Salaam ndiyo wenye  walimu wengi wenye shahada hizo  hivyo kuna haja ya  serikali kuwekeza kwenye elimu na kutoa elimu bora.
Read More

Monday, December 19, 2016

DC MKURANGA AWATAKA MADEREVA BODABODA KUZINGATIA SHERIA

6:00:00 AM 0
 Na Mwandishi Wetu

MKUU wa Wilaya ya Mkuranga Albert Sanga amewataka madereva bodaboda wa wilaya hiyo
kuzingatia kanuni na sheria za usalama barabarani pindi waendeshapo vyombo vyao vya moto ili kuweza
kupunguza tatizo la ajari katika wilaya hiyo.

Mkuu wa Wilaya ya Mkuranga, Albarto Sanga akizungumza na madereva bodaboda wakati wa hafla fupi ya kuwakabidhi vyeti pamoja na leseni zao.

Hayo aliyasema juzi wilayani humo wakati alipokuwa akizungumza na madereva hao wakati wa sherehe za
kuwatunuku leseni na vyeti madereva bodaboda zaidi ya 1580 waliohudhuria mafunzo ya uendeshaji wa vyombo vya moto.

Akizungumza na madereva hao katika hafla hiyo, Sanga aliushukuru uongozi wa chuo cha New Vision kwa kutoa mafunzo bora ya udereva kwa madereva wa bodaboda wa wilaya hiyo na kuongeza kuwa mafunzo hayo yataweza kuleta maendeleo kwa madereva hao na kuongeza hali ya uwajibikaji ambayo kipindi cha nyuma walikuwa hawana.

Mbunge wa Jimbo la Mkuranga, Abdallah Ulega akiwaelekeza jambo madereva wa bodaboda wilaya ya Mkuranga, katika hafla hiyo Ulega alitoa kiasi cha Sh. Milioni moja ili kuweza kufanikisha malengo ya chama hicho cha bodaboda
Alisema endapo madereva hao wataweza kuzingatia kanuni na sheria za usalama barabarani wataweza kupunguza ajari za mara kwa mara na kuongeza uzalishaji wa malighafi mbalimbali zitakazoweza kuiinua wilaya hiyo kiuchumi.

"Lakini pamoja na kuzingatia sheria za usalama barabarani nawaomba sajilini chama chenu na kama mtaweza kufanya hivyo basi mtakuwa mmefungua fursa mbalimbali ikiwemo za kupata mikopo itakayowanufaisha katika mambo yenu ya udereva wa bodaboda pamoja na hali ya maisha kiujumla," alisema Sanga.

Aliongeza kuwa madereva hao wanapaswa kuongeza bidii katika kufanya kazi zao ili waweze kununua pikipiki zao wenyewe badala ya kutrgemea pikipiki za watu wengine ambazo zinawafanya wasipate mafanikio.

Kwa upande wake Mkurugenzi wa Chuo cha Udereva cha New Vision, Jonas Bigoya alisema tatizo la ajari za barabarani linaweza likaepukika endapo madereva wataweza kuhudhuria mafunzo mbalimbali katika vyuo vilivyosajiliwa kwa mujibu wa sheria.

Alisema Watanzania wanapaswa kutambua madereva bodaboda na wao wanafanya kazi kama wafanyavyo watu wengine katika sekta muhimu za kukuza uchumi wa nchi hivyo kutoa mafunzo kwao kutaweza kuwaongezea ujuzi na mbinu mbalimbali za kuweza kuboresha mazingira yao ya kazi.

"Chuo chetu tumegundua tatizo la ajari kwa jinsi linavyozidi kutokea hapa nchini na tutaendelea kutoa elimu maeneo yote ya nchi ili tuweze kutoa elimu na kutokomeza tatizo la ajari linalozidi kutokea mara kwa mara," alisema Bigoya.

Bigoya alimtaka Mkuu wa Mkoa wa Pwani kukiruhusu chuo hicho kupita katika kata zote za mkoa huo ili kuweza kutoa elimu kwa wananchi ambao wanamiliki vyombo vya moto.

Aliongeza chuo hicho kitaweza kutoa mafunzo hayo ya udereva kwa gharama nafuu ambazo zitamuwezesha kila mtanzania kumudu gharama hizo tofauti na baadhi ya vyuo ambavyo vimekuwa vikitoza gharama kubwa zinazowafanya watanzania wengi kushindwa kuhudhuria masomo hayo.








Mkaguzi msaidizi wa Polisi Mkuu Usalama barabarani Mkuranga, Hamidu Mtiginjole akiwaasa madereva wa bodaboda wilaya ya Mkuranga kuzingatia sheria na kanuni za usalama barabarani pindi watumiapo vyombo vya moto.
Akizungumza kwa niaba ya Wanakikundi cha Timu Safiri na Safari Salama inayoundwa na wanachama zaidi ya kumi, Mwenyekiti wa kikundi hicho Edward Chienela alisema kuwa waliamua kuaandaa programu hiyo pasipo malipo ili kuweza kutoa elimu kwa wananchi wanaoshindwa kwenda mjini kupata elimu ya udereva.

Alisema kikundi hicho kitaendelea kuandaa programu za aina hiyo ili kuweza kuhakikisha madereva wote wa wilaya hiyo wanaendesha vyombo vyao hali ya kuwa wanaelimu ya kutosha.

Mafunzo hayo yaliyotolewa kwa muda wa mwezi mmoja yaliweza kuhudhuriwa na madereva zaidi ya 1580 kutoka katika kata 25 za wilaya hiyo huku 1407,wakitunukiwa vyeti, 600 wakitunukiwa leseni zao na 807 wakiwa wanasubiria mchakato wa kukamilisha leseni zao.
Read More

Saturday, November 26, 2016

DC TEMEKE ATAKA WATANZANIA KUUNGANA KULETA MAENDELEO

5:10:00 AM 0
Mkuu wa Wilaya ya Temeke, Felix Lyaniva, Picha na Maktaba.
MKUU wa Wilaya ya Temeke Felix Lyaniva amewataka watanzania kuacha itikadi za kidini pamoja na siasa katika utendaji wao wa kazi badala yake waungane kwa pamoja katika kufanya shughuli mbalimbali zenye lengo la kusaidia kutatua matatizo yanayoikumba jamii.

Akizungumza na wadau mbalimbali waliojitokeza katika uzinduzi wa zoezi la uchangiaji wa damu lililoandaliwa na Jumuiya ya Akhlaaqul Islam (JAI) katika viwanja vya Mwembe Yanga Jijini Dar es Salaam, Lyaniva amesema kuwa watanzania wanapaswa kujitokeza kwa wingi katika kushiriki kazi zinazoonekana kuokoa uhai wa wananchi ikiwemo zoezi hilo muhimu la uchangiaji damu.

Amesema kwa sasa kumekuwa na uhitaji mkubwa wa damu katika hospitali mbalimbali nchini kutokana na makundi yanayohitaji damu kuwa mengi zaidi na kuongeza kuwa endapo watanzania watajitokeza kwa wingi katika uchangiaji wa damu wataweza kupunguza tatizo hilo ambalo linaonekana kugharimu maisha ya wagonjwa wengi.


Lyaniva amesema kitendo cha kujitolea kuchangia damu ni cha kiungwana na kinapaswa kutendwa na kila mtu mwenye vigezo vya kufanya hivyo kwani damu hainunuliwi madukani kama ilivyo bidhaa nyinginezo ambazo zinatengenezwa kiwandani.

Hata hivyo Lyaniva amewataka madereva wanaotumia vyombo vya moto kuendesha pole pole vyombo hivyo na kueleza kuwa endapo watakuwa wakiendesha kwa kufuata taratibu za usalama barabarani wataweza kupunguza ajari za mara kwa mara  na kupelekea mahitaji ya damu kuwa madogo tofauti na ilivyo sasa ambapo ajari zimekuwa zikijitokeza kila kuchapo.

"Nadhani mnatambua kwamba damu inapatikana kwa binadamu pekee na kujitolea kutoa damu yako kwa watu usiowajua kwa hakika unapata swawabu kubwa kutoka kwa Mungu kwa sababu damu hii inakwenda kuokoa maisha ya maelfu ya watanzania wenye uhitaji wa damu kila siku wakiwemo Majeruhi wa ajari, Watoto, Wamama wajawazito pamoja na wagonjwa wa Saratani ambao wote kwa ujumla wanawategemea ninyi," alisema Lyaniva.

Kwa Upande wake Mlezi wa JAI, Sheikh Nurdin Kishki amewataka waislamu kushindana katika kufanya mambo mema yenye lengo la kulisaidia taifa katika utatuzi wa matizo mbalimbali yanayolikabili badala ya kushindana kufanya mambo yanayovunja umoja na mshikamano ambayo yanapelekea kuvunjika kwa amani ya taifa.
Sheikh Nurdin Kishki, Picha na Maktaba.

Amesema waislamu wanapaswa kushindana katika matukio muhimu ya shughuli za kijamii kunawafanya wazidi kupata heshima katika taifa la Tanzania na kuongeza kuwa endapo wataendelea kubishana na kushindana katika masuala ya vita jamii ya watanzania haitawaamini na itawaona kama vile ni watu wasio na maana yoyote ile.

"Nataka mtambue hata katika vitabu vyetu vitakatifu vimeonesha umuhimu uliopo katika kushiriki shughuli hizi za kijamii na leo hii natarajia kuona misikiti ikishindana katika kuleta waumini wao kuja kutoa damu kwa sababu nahakika hiki kitendo ni cha kiungwana kuliko vyote tuvitendavyo," alisema Kishki.

Ameongeza kuwa katika zoezi hilo la ukusanyaji wa damu wanatarajia kupata chupa zaidi ya Elfu tatu ambazo zitakabidhiwa kwa damu salama ili kuweza kuzigawanya kwenye hospitali zenye uhitaji wa damu.
Read More

Post Top Ad

Your Ad Spot