HATIMAYE Klabu ya Manchester United imerudi kileleni mwa orodha ya klabu zenye vipato vikubwa duniani kwa msimu uliopita mara baada ya kuwapiku miamba ya Soka Nchini Hispania, Real Madrid.
Kwa Mujibu wa taarifa zilizochapishwa na kampuni kubwa ya ukaguzi wa hesabu Duniani, Deloitte zinaonesha mapato ya Man U yameongezeka kutoka Euro Mil.519.5 kwa msimu wa 2014-15 hadi 689 kwa msimu wa 2015-16.
Viongozi wa Klabu ya Manchester United |
Hii ni mara ya kwanza kwa Man U kushika nafasi hiyo tangu walipoiachia mwaka 2003-4 na kuchukuliwa na Madrid waliofanya vizuri kwa kipindi cha miaka 11 mfululizo kwa kutengeneza kiasi cha Euro mil. 577 kiasi ambacho hakikufikiwa na klabu nyingine yoyote duniani.
Ripoti ya Shirika la Deloitte inaonesha ukijumlisha mapato ya timu ishirini bora kwa msimu wa 2015-16 vimeongezeka kwa asilimia 12% na kufikia jumla ya Euro. Bilioni 7.4.
Madrid iliyokuwa kinara kwa miaka 11 imeangukia nafasi ya tatu wakiwa wanajumla ya Euro Mil. 620.1 huku nafasi ya pili ikienda kwa wapinzani wao wakubwa Barcelona wenye Eiro Mil. 620.2 na nafasi ya nne ikidondokea kwa Klabu ya Bayern Munich yenye kiasi cha Euro Mil. 592.
Hata hivyo Ripoti hiyo inaonesha timu za uingereza zimefanikiwa kushika nafasi kubwa zaidi kuliko klabu zote duniani kutokana na kuingiza timu tano katika orodha ya timu kumi zenye mapato makubwa huku Manchester City ikishika nafi ya Tano jambo ambalo halijawahi kutokea.
Mwishooooooooo
No comments:
Post a Comment