MUANGALIZI

Hot

Post Top Ad

Your Ad Spot

Thursday, March 1, 2018

Dk Shein awaapisha mawaziri, wakuu wa wilaya

3:00:00 AM 0
 
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dk Ali Mohamed Shein leo Machi 1, 2018 amewaapisha viongozi aliowateua jana Februari 28, 2018 kushika nyadhifa mbalimbali katika Serikali ya Mapinduzi Zanzibar (SMZ).
Taarifa iliyotolewa na Ikulu Zanzibar leo, inaeleza kuwa hafla hiyo imefanyika Ikulu mjini Zanzibar na kuhudhuriwa na viongozi mbalimbali wa Serikali.
Baadhi ya viongozi hao ni Makamu wa Pili wa Rais, Balozi Seif Ali Idd; Spika wa Baraza la Wawakilishi,  Zubeir Ali Maulid; Jaji Mkuu wa Zanzibar, Omar Othman Makungu; Mwanasheria Mkuu wa Zanzibar,  Said Hassan Said; mawaziri, naibu mawaziri na wakuu wa mikoa.
Walioapishwa ni Waziri wa Biashara na Viwanda Balozi, Amina Salum Ali;  Waziri wa Vijana, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Balozi Ali Abeid Karume; Waziri wa Ujenzi, Mawasiliano na Usafirishaji na Dk Sira Ubwa Mamboya.
Wengine ni Waziri wa Afya, Hamad Rashid Mohamed; Waziri wa Kilimo, Maliasili, Mifugo na Uvuvi,  Rashid Ali Juma; Waziri wa Ardhi, Nyumba, Maji na Nishati, Salama Aboud Talib; Waziri wa Habari, Utalii na Mambo ya Kale, Mahmoud Thabit Kombo pamoja Waziri wa Kazi, Uwezeshaji, Wazee, Wanawake na Watoto, Maudline Cyrus Castico.
Pia wamo Naibu Waziri wa Ardhi, Nyumba, Maji na Nishati, Juma Makungu Juma;  Naibu Waziri wa Habari, Utalii na Mambo ya Kale, Choum Kombo Khamis; Naibu Waziri wa Kazi, Uwezeshaji, Wazee, Wanawake na Watoto, Shadia Mohamed Suleiman; Naibu Waziri wa Kilimo, Maliasili, Mifugo na Uvuvi, Dk Makame Ali Ussi na  Naibu Waziri wa Biashara na Viwanda, Hassan Khamis Hafidh.
Pia, Dk. Shein amewaapisha wakuu wa wilaya aliowateua ambao ni  Issa Juma Ali (Mkoani-Pemba) na Rajab Ali Rajab wa Kaskazini B, Unguja.
Viongozi walioapishwa wameahidi kuendelea kumsaidia Rais Dk. Shein katika kuhakikisha Zanzibar inazidi kupata maendeleo, kuimarisha ushirikiano na kuwatumikia wananchi.
Pia, wameahidi kuleta mabadiliko na kufanya kazi kwa vitendo sambamba na kuendelea kusimamia amani na utulivu uliopo nchini.
Jana, Dk Shein alifanya mabadiliko madogo katika Baraza la Mapinduzi kwa kuongeza wizara moja zaidi na kuwabadilisha wizara baadhi ya Mawaziri.
Kufuatia mabadiliko hayo, shughuli za vijana zimehamishiwa katika Wizara mpya ya Vijana, Utamaduni, Sanaa na Michezo shughuli za mazingira zimehamishiwa katika Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais na shughuli za Wakala wa Serikali wa Uchapaji zimehamishiwa Wizara mpya ya Habari, Utalii na Mambo ya Kale.
Aidha, amewateua naibu mawaziri wapya wawili na kumbadilisha wizara naibu waziri mmoja ambapo kufuatia mabadiliko hayo, SMZ hivi sasa ina wizara 14.
Read More

Simba, Yanga FC zachibwa mkwara na KARIA

2:44:00 AM 0
 
 
Rais wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) ametamka kuwa hataruhusu klabu yoyote kucheza Ligi Kuu Bara kama itakuwa haijawakatia bima wachezaji wake watakaowatumia katika msimu wa 2018/2019.
 
Kauli hiyo, aliitoa kwenye ufunguzi wa semina ya utawala bora kwa klabu za ligi kuu na Ligi Daraja la Kwanza iliyofanyika jana Rombo Green View iliyokuwepo Ubungo jijini Dar es Salaam ambayo ilihusisha klabu kongwe za Simba na Yanga.
 
Semina hiyo, iliandaliwa na Kampuni ya Maendeleo na Utafiti wa Michezo (ISDI) kwa kushirikiana na Alliance Life Assuarance na TFF kwa lengo la kutoa elimu kwa viongozi wa klabu kujua jinsi ya utawala, kujiongoza na kutafuta wadhamini.
 
Akizungumza na Waandishi wa Habari kabla ya kufungua semina hiyo, Karia alisema kikubwa anataka kuona klabu maendeleo na mafanikio kwa klabu hizo huku akiamini kupitia semina hiyo wawakirishi hao watapata elimu nzuri.
 
 
Karia alisema, moja ya maendeleo anayotaka kuyaona ni klabu kuwakatia bima wachezaji wake ambalo amepanga kulisimamia mwenyewe na hataruhusu timu yoyote kucheza ligi kama itakuwa haijakamilisha zoezi hilo.
 
“Niseme kuwa, sitakuwa na masihala juu la hili la bima ni lazima kila klabu iwakatie bima ya afya wachezaji wake na uzuri wapo hapa Alliance Life Assuarance ambao wanausika na bima, hivyo tutazungumza nao kujua jinsi ya kufanya.
 
“Niseme kuwa, kama klabu haitakuwa imewakatia bima wachezaji wake, basi haitacheza ligi kuu msimu ujao na hilo nitahakikisha ninalisimamia vizuri na kama itakuwepo klabu imeshindwa kutimiza hilo basi itatakiwa kuwasiliana na bodi ya ligi tujue jinsi ya kuwasaidia ili wakatiwe bima,”alisisitiza Karia.
 
“Na hilo alitaangalia ukubwa wala udogo wa klabu ni lazima kila timu ifuate kanuni za ligi kuu ambazo tumeziweka,”alisema Karia.
 
SOURCE: global publisher
Read More

Tuesday, January 30, 2018

LIVE VIDEO: JPM Azindua Hati za Kusafiria

10:42:00 PM 0
Tazama hapa chini Video Rais John Magufuli Akizindua hati za kusafiria.


Read More

Saturday, January 27, 2018

Aslay akemea mashabiki kumfananisha na Rich Mavoko

3:50:00 AM 0
Msanii wa muziki Bongo, Aslay amesema si vizuri kufananishwa na Rich Mavoko kwani ni msanii ambaye amemtangulia katika muziki.
Muimbaji huyo amesema Rich Mavoko amekuwa akifanya vizuri kila siku, hivyo mashabiki wanaomshindanisha wanakosea.
“Huwezi kunishindanisha na Rich Mavoko, yule ni kaka yangu halafa anafanya vitu vikubwa, nimemkuta kwenye muziki na amefanya vitu vikubwa, kwa ukisema unanishindanisha na Rich Mavoko utakuwa unakosea,” Aslay ameiambia Bongo5.
Katika hatua nyingine Aslay ameeleza sababu ya yeye kuwa miongoni mwa wasanii ambao ngoma zao zinapata views zaidi katika mtandao wa YouTube.
“Ni mashabiki wangu wa kweli ndio maana unakuta hata nikitia ngoma leo kesho unakuta nina laki moja, kwa hiyo siwezi kusema labda nilikuwa nashindana au nina vitu vikubwa sana navifanya niwe na views wengi YouTube ni mashabiki zangu kunipenda kweli,” amesema.
Read More

VIDEO: Pah One - Hatuna Hbari

3:28:00 AM 0
Kundi la Pah One wamerudi kivingine baada ya kukaa kimya kwa muda mrefu, wameachia video ya ngoma yao mpya ‘Hatuna Habari’, video imeongozwa na Mims. Itazame hapa.


Read More

Vifahamu Vyakula Vinavyoondoa Mumivu ya Hedhi

3:19:00 AM 0

Kila mwanamke hupitia hatua ya kupatwa na hedhi mara moja kwa mwezi, ikiwa ni maumbile ya kawaida waliyoumbwa nayo. Lakini wanawake wengi husumbuliwa na matatizo kadhaa siku chache kabla au wakati wa siku zao, matatizo hayo hutofautiana kati ya mtu na mtu kutegemeana na afya ya muhusika, wapo baadhi ya wanawake huumwa na kiuno, wengine tumbo n.k

Dlili za matatitizo ya hedhi
Siku chache kabla ya hedhi, baadhi ya wanawake hupatwa na hofu na huwa wenye hasira. Husumbuliwa na mfadhaiko wa akili, huumwa na kichwa, matiti hujaa maziwa, hukosa usingizi na kuvimba sehemu za siri. Hali hii husababishwa na kukosekana kwa uwiano wa homoni (Homone imbalance) na hali hii huweza kukoma ndani ya saa 24 baada ya kuanza hedhi.

Wengine hupatwa na maumivu makali sana wakati wa hedhi. Maumivu hayo huwapata akina mama ama siku mbili ama tatu kabla au mara tu waanzapo siku zao. Hali hii pia inasababishwa na kutokuwepo kwa uwiano wa homoni mwilini, ambako kumesababishwa na ukosefu wa virutubisho fulani.

Wengine hutokwa na damu nyingi kuliko kawaida au kukaa katika siku za hedhi kwa kipindi kirefu kuliko kawaida. Kuna sababu nyingi zinazoweza kuchangia hali hii, ikiwemo kuugua kwa muda mrefu, kupatwa na hofu, huzuni, mshtuko na sababu nyingine za kitabibu.

Vifatatavyo ni vyakula vinavyoweza kutibu maumivu wakati wa hedhi

2. Tangawizi
Tangawizi nayo ni dawa nzuri sana ya kutibu matatizo yatokanayo na hedhi, hasa katika tatizo la maumivu makali na kutokupata hedhi. Chukua kipande cha tangawizi mbichi, kiponde na kiweke kwenye kikombe cha maji ya moto kwa dakika chache, kisha tia sukari kiasi na unywe mchanganyiko huo, kwa siku mara mbili kila baada ya mlo.

2. ufuta.
Ufuta (Sesame) nao ni miongoni mwa mbegu za asili unazoweza kula na kutibu matatizo ya hedhi. Saga ufuta na pata unga wake kisha uchanganye na maji ya moto, kunywa mara mbili kwa siku. Kinywaji hiki huondoa maumivu wakati wa hedhi kwa wasichana wadogo.

Ukitumia mara kwa mara kinywaji hiki cha ufuta, hutibu pia tatizo la kupata hedhi kidogo. Pia unaweza kuchangaya maji ya kuoga ya uvuguvugu na mbegu za ufuta zilizopondwa pondwa kiasi cha kiganja kimoja, nayo hutoa nafuu kubwa kwa wanaosumbuliwa na maumivu, hasa ukitumia siku mbili kabla ya siku zako.

3. Papai
Mungu ametuumba na kutupa mazao mengi ambayo yana uwezo wa kutatua matatizo yetu ya kiafya, iwapo tutagundua siri hiyo. Papai bichi nalo linaelezwa na watafiti wetu kuwa lina uwezo wa kulainisha misuli ya njia ya uzazi hivyo kufanya utokaji wa hedhi kuwa mwepesi usio na maumivu. Papai huwa na manufaa zaidi kwa wasichana haswa kwa wale wenye tatizo la kutopata siku zao kutokana na kuwa na ‘stress’ au mawazo. Utapata faida hiyo kwa kula mara kwa mara tunda hilo bichi (ambalo halijaiva lakini limekomaa)

4. Juisi za mboga za majani.
Kwa kutumia vyakula asilia unaweza kuepukana na maumivu ya mara kwa mara wakati wa siku zako. Katika orodha ndefu ya juisi za mboga zinazotibu kwa uhakika matatizo yote ya hedhi, ni Kotimiri (Parsley), mboga ya majani ambayo upatikanaji wake ni rahisi. Kwa mujibu wa watafiti, Kotimiri ina uwezo wa kurekebisha uwiano wa homoni hivyo kuondoa matatizo kadhaa ya hedhi.

Inaelezwa kuwa uwezo wa Kotimiri kurekebisha matatizo ya hedhi unatokana na kuwa na aina ya kirutubisho kiitwacho ‘Apiol’ ambacho pia kimo miongoni mwa homoni za jinsia ya kike (estrogen). Maumivu na mvurugiko wa siku hurejea katika hali ya kawaida kwa kunywa juisi ya Kotimiri mara kwa mara.

Aidha, juisi hiyo inapochanganywa na juisi ya viazi pori (Beet Root), karoti au matango huwa na nguvu zaidi. Kiwango kinachoshauriwa kuchanganya kiwe na ujazo sawa kwa kila aina ya juisi utakayochanganya. Juisi yenye mchanganyiko huo ni rahisi kutengeneza na ni dawa inayoweza kumsaidia mwanamke wakati wote wa maisha yake bila kuhitaji kutumia dawa zingine kali za kuzuia maumivu (pain killers) ambazo huwa na madhara baadaye
Read More

Ruby, Clouds Media Bifu limekwisha

2:53:00 AM 0

Msanii wa muziki Bongo, Ruby amemaliza tofauti baina yake na Clouds Media Group. 

Muimbaji huyo ametumia kipindi cha XXL kuwaomba radhi wale wote aliowakwaza katika chombo hicho cha habari.

“Yeyote, awe ni mwanakamati wa Clouds, team Clouds au awe ni shabiki wa nje I like to apologize guy to say sorry to my country, sorry to this management Clouds, I love them so much all I need is support mimi naamini kwamba ukiwa mjinga kwenye kila kitu utapata kujua vitu vingi sana,”
amesema Ruby.

“Nilikaa nikamuomba Boss wangu Ruge samahani, mimi ni mdogo wewe ni mkubwa, of course kwa chochote kile mimi ndio nakosea,” amesema.

Clouds Media Group walikuwa wamesitisha kucheza nyimbo za msanii huyo kutokana na tofauti zao, hivyo sasa nyimbo zake zinachezwa na inaelezwa tangu November mwaka jana ilitolewa ruhusu kwa ngoma zake kuchezwa.
Read More

BREAKING NEWS: IGP Sirro azungumza na Viongozi wa Dini

Trump, Kagame Uso kwa uso

12:43:00 AM 0

Rais wa Marekani, Donald Trump amekutana na kufanya mazungumzo na Paul Kagame ambaye ni Rais wa Rwanda na  Mwenyekiti wa Umoja wa Afrika (AU) na kumuomba afikishe salamu zake za upendo kwa viongozi wengine wa mataifa wanachama wa AU.

Viongozi hao wawili wamekutana mjini Davos, Uswizi baada ya Mkutano wa Viongozi na Watu Mashuhuri Kuhusu Uchumi na Biashara Duniani, Mkutano huo wa Kagame na Trump umekuja wiki chache baada ya kiongozi huyo wa Marekani kutoa kauli iliyotafsiliwa kama ni kuyakashifu mataifa ya Afrika.

Hatua hiyo ilimfanya kushutumiwa vikali na viongozi wa AU na baadhi ya viongozi wa nchi za Afrika kama vile Botswana na Ghana ambapo amekanusha kwamba alitumia neno hilo kuyakashifu mataifa ya Afrika huku akikiri kutumia maneno makali akiyaeleza mataifa ya Afrika, Haiti na El Salvador alipokuwa anazungumzia wahamiaji wanaoingia Marekani.

Wakati wa mkutano wake na Kagame,  Trump hajaonyesha dalili zozote za majuto kuhusu tamko lake la awali kuhusu Afrika huku akisifia kuwa mkutano wao huo ulikuwa “wa kufana sana”, na kueleza nchi hizo mbili kama washirika wa kibiashara ambao wanajivunia “uhusiano mzuri sana.”

“Ningependa kukupongeza, Bw Rais, unapochukua majukumu ya kuwa kiongozi mpya wa Umoja wa Afrika, ni heshima kubwa … najua unaenda kuhudhuria mkutano wa kwanza karibuni. Tafadhali, fikisha salamu zangu.”

Rais Kagame alisema wameshauriana kuhusu ushirikiano wa nchi hizo mbili, ikiwa ni pamoja na usaidizi wa Marekani kwa Rwanda katika operesheni zake kote duniani, pamoja na masuala ya kiuchumi, biashara, uwekezaji na idadi ya watalii wa Marekani wanaozuru Rwanda, ambayo inaongezeka. Mkutano wa viongozi wa nchi wanachama wa AU utafanyika kesho Jumapili na Jumatatu.
Read More

Thursday, January 25, 2018

Mke Kumtaka wema aolewe na Nabii Tito

1:27:00 AM 0
African Sweetheart, Wema Sepetu
 Katika hali isiyotarajiwa, imeelezwa kuwa msanii nyota wa filamu za Kibongo, Wema Sepetu, amemlipua mke wa ‘Nabii’ Tito baada ya mwanamke huyo kumshawishi kupitia mitandaoni aolewe na nabii huyo.

Chanzo makini kilisema kuwa, msanii huyo amekasirishwa na kitendo cha mke huyo kumshawishi kuolewa na mumewe anayeitwa Onesmo Machija ‘Nabii Tito’ (44).

“Wema Sepetu nakupenda sana hata Nabii Tito anakupenda sana, kwanza mzuri, una shepu nzuri hata katika mambo ya Kiafrika unaongoza kwa uzuri.

“Nabii Tito huyo kwa watu wasiomfahamu wanasema sio nabii lakini kwa mimi ninayemfahamu na kuishi naye naona mambo ya kinabii anayofanya, nakuomba ukubali hata mimi nakupenda sana, kwanza una shepu nzuri.

“Uwe mke mwenzangu, ukubali kuwa mke wa Nabii Tito. Sikia kilio cha mke wa nabii,” amesikika kwenye video mke huyo wa Nabii Tito akimbembeleza Wema.

Naye Nabii Tito kwenye video hiyohiyo amechombeza kwa kubembeleza kwamba Wema akubali kuwa mkewe ili kanisa lao likuwe.

Alipotafutwa Wema na kuulizwa kuhusiana na video hiyo alisema, ameiona na amekasirishwa na kile walichokifanya nabii huyo na mkewe.

“Kiukweli wameniudhi sana kwa kunidhalilisha. Nawasiliana na mwanasheria wangu ili nimburuze mahakamani mwanamke huyo,” alisema Wema.

Hata hivyo, Jeshi la Polisi mkoani Dodoma, mapema wiki hii lilimkamata nabii huyo na kumfanyia mahojiano kutokana na mahubiri ya kidini anayoyafanya na limesema mtu huyo ana matatizo ya akili.

Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Dodoma, SACP Gillesi Muroto amesema Juni 23, 2014, mtu huyo aliwahi kulazwa Hospitali ya Taifa ya Muhimbili kwa ajili ya matibabu ya akili chini ya daktari aliyejulikana kwa jina moja la Dk. William ambapo aliporuhusiwa alitakiwa kurejea hospitalini hapo Julai 9 mwaka huohuo lakini hakurejea.

Kamanda Muroto aliendelea kusema kwamba, baada ya hapo Machija ambaye kanisa lake halijasajiliwa popote, aliibukia mkoani Dodoma katika Kijiji cha Nong’ona kilicho karibu na Chuo Kikuu cha Dodoma (Udom) akifanya mahubiri ya kidini yaliyodaiwa kuwa hayakuwa na maadili ya kidini.

“Kwa msingi huo, jeshi la polisi limempeleka Hospitali ya Rufaa ya Milembe iliyoko mkoani Dodoma kwa ajili ya kumpima tena matatizo hayo ya akili na baada ya majibu kutolewa, Dk. Dixon Philipo aliyemshughulikia alithibitisha kwamba bado ana matatizo hayo ya akili,” alisema kamanda Muroto juzi na kusisitiza kuwa wanaendelea kumshikilia kutokana na matendo yake aliyoyafanya ili kufanya uchunguzi zaidi.


Nabii Tito na mkewe pamoja na mfanyakazi wake wa ndani.
Read More

Bifu zito Kati ya Stamina na Edu boy

1:06:00 AM 0

Msanii wa bongo fleva anaejulikana kwa jina la edu boy, alieachia jiwe lake jipya siku chache zilizopita amejikuta kuingia kwenye bifu zitto na msanii stamina ambae alifanya nae remix ya ngoma yake ya Naiee, baada ya kutoa ngoma mpya inayoitwa TUNASAFISHA ambapo ndani ya ngoma hiyo amewapita wasanii wengi kwa kuwachana akiwemo Diamond, alikiba dogo janja stamina na wengine wengi.

Bifu hili kati ya stamina na Edu boy limesababishwa na ngoma hiyo baada ya kuibwa kuwa stamina anaimba kwa kusafiria nyota za wasanii wenzake, Edu boy. katika mahojiano aliofanyiwa edu boy na times fm ameeleza uwa kabl hajatoa ngoma hiyo alimshirikisha stamina na alijibiwa kuwa kama kamchana nae atamjibu na baadae kilichotokea  baada ya ngoma kutoka alishangaa kuona amefungiwa (BLOCK) na stamina kwenye kila njia ya mawasiliano

Vile vile edu alieleza kuwa kama ni bifu, liwe la kimuziki nae aingie studio amjibu na ikiwezekana waingie ulingoni ili zaidi ya menzake ajulikane na kusisitiza kuwa hata stamina akiiingia ulingozi hataweza kwani atamuaibisha.
Read More

Afariki dunia Baada ya Kutoa Sadaka

12:49:00 AM 0

WAUMINI wa Kigango cha Muze, Parokia ya Zimba Kanisa Katoliki Jimbo la Sumbawanga waliofurika kanisani kwa ibada ya misa ya Jumapili walipatwa na taharuki kubwa huku ibada ikisimama kwa muda baada ya mwanakwaya kupoteza fahamu muda mfupi baada kutoa sadaka.

Mwanakwaya huyo akiwa na ujauzito wa miezi mitano aitwaye Flora Nandi (25) akiwa mwanakwaya wa Kwaya ya Mtakatifu Cecilia alifariki dunia akiwa anakimbizwa kupatiwa huduma katika zahanati iliyopo katika kijiji cha Muze katika Bonde la Ziwa Rukwa wilayani Sumbawanga.


Mkasa unaofanana na huu ulitokea miezi sita iliyopita pale mkazi wa Mtaa wa Makanyagio katika Manispaa ya Mpanda mkoani Katavi, Beatrice Kangu (48) alifikwa na umauti muda mfupi baada ya kutoa sadaka katika ibada ya Jumapili iliyofanyika katika Kigango cha Kanisa Katoliki Jimbo la Mpanda kilichopo katika Mtaa wa Makanyagio B.
source: Tanzania Today
Read More

Daktari wa Olympic ahukumiwa Miaka 175 Jela

12:42:00 AM 0

Aliyekuwa Daktari wa timu ya taifa ya akina dada ya michezo ya kuruka hewani nchini Marekani Larry Nasser, amehukumiwa kifungo cha miaka 175 jela. Nasser mwenye umri wa miaka 54, amepewa adhabu hiyo baada ya kupatikana na makosa 10 ya kuwanyanyasa kimapenzi mamia ya wanamichezo wa kike, ambao walijitokeza kutoa ushahidi.
Wasichana na wanawake 160, walijitokeza kutoa ushahidi dhidi ya daktari huyo ambaye juhudi zake za kuomba radhi hazikuzaa matunda.

Jaji Rosemarie Aquilina amesema daktari huyo ni mtu hatari.
“Najisikia fahari na furaha kubwa kutoa adhabu hiyo kutokana na kitendo alichofanya Nasser na nataka iwe fundisho kwa wengine, “ Jaji Rosemary Aquilina ameiambia mahakama.
Takriban wasichana 140 wamewasilisha kesi dhidi ya Nasser, taasisi ya USA Gymnastics na chuo kikuu cha MSU, wakidai kuwa taasisi hizo mbili zilipokea tuhuma za unyanyasaji wa kingono dhidi ya daktari huyo miaka kadhaa ya nyuma.
Wakati huo huo mkuu wa chuo kikuu cha jimbo la Michigan (MSU) alikokuwa anafanya kazi Nasser kati ya mwaka 1997 na 2016, amejiuzulu.
Lou Anna Simon amekuwa akikabiliwa na shinikizo kujiuzulu.
Read More

Thursday, December 28, 2017

Awaua watoto wake wawili kwa sumu

6:45:00 AM 0
KIAMBU, KENYA: Jeshi la Polisi linamshikilia Mwanaume mmoja aliyewaua Watoto wake wawil 2 na yeye kunywa sumu ambayo haikumuua.

Watoto hao waliouawa
mmoja alikuwa na miaka 7 na mwingine miaka 3

Inadaiwa kuwa siku moja kabla ya Sherehe ya Christmas familia hiyo ilisafiri hadi Narumoru ambako Mama wa Watoto hao alibakia huko kwasababu ambazo hazijajulikana.
Read More

Moto wazidi kuwaka kati ya Zari na Hamisa

5:56:00 AM 0

Baada ya mwanamitindo Hamisa Mobetto kumtibua upya mama watoto wa Diamond, Zari The Boss Lady ikiwemo kumuita mcheza picha chafu, Zari ajibu mapigo tena.
Mobetto ambaye alikuwa nchini Uganda weekend iliyopita kwaajili ya show ya Girls Power, alimtupia dongo Zari na kumuita mcheza picha za uchi.

Alhamisi hii Zari ameamua kumtolea uvivu Mobetto kwa kuandika ujumbe mkali mfululizo kupitia mtandao wa snapchat.
“Bora mimi changudoa mzee niliye na mafanikio na bado ananipenda kuliko kijana wa miaka 20+ mama uliyeachwa solemba mara mbili na tuzo juu #MchepukoUsioNaAKili #MweweWaMwaka,” , aliandika Zari Snapchat.


“Kijana, kijana kila siku kijana, kijana na mzuri lakini huwezi kutafuta mwanaume wa kwako mwenyewe….namna chan**doa usivyojiamini, Kama unajiamini na uzuri na akili basi acha tuone mwanaume gani atakutaka baada ya drama hizi, baby daddy 3 loading ukiwa na miaka 20+ atakuwa mjinga pia,” alisema Zari kupitia ujumbe huo.
Zari akaongeza “sio wewe cha***doa uliyelia social media ukidai Lulu kakuibia bwana’ko lakini umegeuka kufanya hicho hicho ulicholilia wakati unajua inavyouma, Mungu hawezi kubariki furaha yako juu ya maumivu ya mwanamke mwingine…ng’oo!!!”
“Unaweza kupost picha zote za nyuma ukiwa nae, lakini tayari nimekwisha msamehe makosa yake yaliyopita. Siwezi kubadilisha historia….nimechukulia kawaida naendelea kujenga maisha yangu ya kesho. Uchawi wote unaisha nguvu na sasa anarudi kwa akili zake kumrudia,” amesema Zari na
Read More

Ajibu na Chirwa kutopambana na Mbao FC

5:41:00 AM 0
YANGA SC itaondoka kesho jioni kwa ndege ya Fast Jet kwenda Mwanza tayari kwa mchezo wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara dhidi ya wenyeji Mbao FC Jumapili Uwanja wa CCM Kirumba mjini humo.

Lakini Yanga itaondoka bila washambuliaji wake wote vinara wa mabao msimu huu, Ibrahim Ajib na Mzambia Obrey Chirwa.

Katibu Mkuu wa Yanga, Charles Boniface Mkwasa ameiambia Bin Zubeiry Sports – Online leo Ajib hatakwenda Mwanza kwa sababu anatumikia adhabu ya kadi tatu za njano wakati Chirwa bado yupo kwao, Zambia kwa matatizo ya kifamilia.

Katika mabao 17 ambayo Yanga imefunga kwenye Ligi Kuu msimu huu, 11 yanatoka kwa wawili hao, Chirwa akiwa amefunga sita na Ajib matano.

Pamoja na wawili hao, Yanga pia itaendelea kuwakosa wachezaji wake majeruhi Wazimbabwe, kiungo Thabani Scara Kamusoko na mshambuliaji Donald Dombo Ngoma pamoja na beki mzalendo, Kevin Patrick Yondan.

Mshambuliaji Ibrahim Ajib hatakwenda Mwanza kwa sababu anatumikia adhabu ya kadi tatu za njano


Mkwasa amesema Chirwa anatarajiwa kurejea nchini kuanzia kesho na hawezi kujumuishwa kwenye msafara wa Mwanza wazi hatakuwa fiti.

Kwa ujumla Ligi Kuu inatarajiwa kuendelea kesho baada ya mapumziko ya wiki tatu kupisha michuano ya CECAFA Challenge iliyomalizika nchini Kenya wiki iliyopita kwa wenyeji, Harambee Stars kuwa mabingwa wakiwafunga Zanzibar katika fainali.

Kesho Azam FC watakuwa wenyeji wa Stand United Uwanja wa Azam Complex, Chamazi, Dar es Salaam kuanzia Saa 1:00 usiku na Jumamosi kutakuwa na mechi tatu, Lipuli na Tanzania Prisons Uwanja wa Samora, Iringa kuanzia Saa 8:00 mchana, Mtibwa Sugar na Maji Maji Uwanja wa Manungu, Turiani, Morogoro na Ndanda FC na Simba SC Uwanja wa Nangwanda Sijaona mjini Mtwara zote zikianza saa 10:00 jioni.

Jumapili, mabingwa watetezi, Yanga watakuwa wageni wa Mbao FC Uwanja wa CCM Kirumba, Mwanza saa 10:00 jioni na Njombe Mji FC wataikaribisha Singida United kuanzia saa 8:00 mchana Uwanja wa Saba Saba, Njombe.

Mechi za kukamilisha mzunguko wa 12 zitachezwa mwaka mpya, Januari 1 Mbeya City wakiikaribisha Kagera Sugar Uwanja wa Sokoine mjini Mbeya  na Mwadui wakiikaribisha Ruvu Shooting zote kuanzia saa 10:00 jioni.

Baada ya mechi hizo, Ligi Kuu itasimama tena kupisha mechi za Kombe la Mapinduzi visiwani Zanzibar na raundi ya tatu ya Azam Sports Federation Cup (ASFC) itakayochezwa kati ya Januari 5 na 7 mwakani kabla ya kuingia kwenye mzunguko wa 13 wa ligi kuanzia Januari 13 na 17, 2018.
Read More

Msigwa awapa hongera Kakobe, Gwajima

5:35:00 AM 0
 
Mbunge wa Iringa Mjini kwa tiketi ya (CHADEMA) Peter Msigwa amefunguka na kuwapongeza baadhi ya viongozi wa dini akiwepo Askofu Zakaria Kakobe, Askofu Josephat Gwajima, Askofu Benson Bagonza kwa kile walichofanya kukemea baadhi ya matendo ya serikali

Mchungaji Msigwa ameweka wazi kuwa hicho kilikuwa kilio chake kikubwa kwa viongozi wa dini kwani Tanzania inapaswa kujengwa na watu wote na si wanasiasa tu

"Nawapongeza sana baadhi ya viongozi wa dini kama vile Askofu Kakobe, Askofu Gwajima, Askofu Bagonza na Shayo ambao kwa namna moja kimekuwa kilio changu kikubwa pamoja na wananchi wengine kuona viongozi wa dini wanakuwa kimya wakati mambo hayaendi vizuri, Kwa kifupi niwapongeze sana kwa sababu nchi hii inajengwa na sisi sote na mali yetu sote" alisema Msigwa

Aidha Mchungaji Msigwa aliendelea kusema kuwa yeye amesikitiswa na baadhi ya vijana wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) ambao wanataka kulifanya Taifa la Tanzania lisiwe la watu wa kufikiri

"Hoja alizotoa Askofu Kakobe zinafafanua vizuri na kuwafanya watu wafikiri na kujibu kwa hoja lakini watu wameanza kumshambulia kwa kejeli na maneno ambayo si ya kiugwana, hoja siku zote hujengwa kwa hoja hakuna mtu ambaye yupo juu ya sheria, Kakobe alimuomba Mhe. Magufuli akatubu kwamba anaiendesha nchi kama vile nchi ya chama kimoja" Alisisitiza Msigwa
Read More

Friday, May 12, 2017

New Video: Darfoo X ommy jnr _Nishike

2:06:00 AM 0

Msanii mpya wa bongo fleva ambae amedai anamalengo ya kuwa Tishio katika Tasnia ya Muziki Tanzania Bakari Kaoneka (Darfoo) amedai kuwa anataka kufanya Muziki wa Tanzania kuzidi kwenda mbele zaidi na kudai kuwa yeye anajitahidi kufanya musiki kuwa kitu cha kujivunia katika nchi yetu ya Tanzania na kuahidi kuwa anauwezo wa kufanya hivyo, na kumfikia Diamond platnumz kwani ni msanii pekee alie weza kufanya muziki kuwa na dhamani kubwa. Na hayonyote hayo ni kwasababu ya kwasababu kupenda kujifunza kupitia wasanii waliomzidi.

"Napenda mziki na nmezaliwa nikiupenda na naishi kwenye muziki,na nina malengo ya kuzidi kuupeleka mbali muziki wa Tanzania Uzidi kufika mbali, na naamini nitafanikiwa kwasabau namshirikisha mweneyezi mungu na napenda kujifunza kwa wasanii wakubwa walionizidi maana naamini asiyejifunza kutoka kwa mkubwa hawezi kufikia malengo."

Muongoza muziki ( Director) Ambae amekuwa ni boss wake na director wake amesema msanii wake anauwezo wa kufanya wa kufanya vizuri na kufikisha muziki wa Tanzania mbali kwa kuwa anajuhudin za kujifunza kutoka kwa wengine na amesema kupitia video yake ya kwanza aliofanya kutoka kwenye nyimbo yake ya NISHIKE amesema baada ya hiyo kunaaa zaidi ya video inayofuata.

Read More

Saturday, March 18, 2017

New Video| Barakah Da Prince _ Acha niende

3:16:00 AM 0

msanii machachari wa Bongoflava Baraka Da Prince aamua kutoa kichupa chake kipya kinachoenda kwajina la Acha Niende
Read More

JPM Azima kiki kwa Viongozi

2:57:00 AM 0
KAMA kuna waziri au kiongozi yeyote anataka kutoa taarifa yenye kuwagusa wananchi moja kwa moja, ni dhahiri kuwa sasa atalazimika kujiridhisha zaidi.


Aidha, waziri na viongozi wengine wanatakiwa pia kuzingatia dhana ya uongozi wa pamoja kwa kuwahusisha wenzao na pia kupata maoni ya wataalamu katika wizara au taasisi wanazoziongoza kabla ya kulifikisha kwa umma.

Vinginevyo, mawaziri wajiandae kushuhudia maagizo yao yakitenguliwa huku pia wakijiweka katika hatari ya kufikiriwa kuwa wanafanya hivyo kwa minajili ya kutumia matamko yao kama ‘kiki’ za kuwaonyesha kuwa wanafanya kazi vyema na kwa kasi inayosisitizwa na Serikali ya awamu ya tano.

Angalizo hilo limetolewa na baadhi ya wachambuzi wa amsuala ya kisiasa walizoungumza na Nipashe kuelezea mkasa uliomkuta Waziri wa Sheria na Katiba, Dk. Harrison Mwakyembe, ambaye agizo lake la kuzuia ufungishaji ndoa kwa watu wote wasiokuwa na vyeti vya kuzaliwa lilifutwa na Rais John Magufuli kwa kuonekana kuwa litawaathiri mamilioni ya Watanzania wasiokuwa na vyeti hivyo.

Baadhi ya wachambuzi walidai kuwa Mwakyembe siyo waziri au kiongozi wa kwanza kutoa taarifa zilizomlazimu Rais Magufuli kuingilia kati kwa manufaa ya Watanzania na hivyo, wanapaswa kujua kuwa wana wajibu mkubwa kwa taifa na kutakiwa wajiepushe na matamko binafsi yasiyofanyiwa kazi kwa kina kabla ya kutolewa kwa umma.

“Ni vizuri kwa kila waziri au kiongozi yeyote yule kujipa uhakika wa kila tamko na amri wanazotaka kutoa kwa umma…kwa mfano, ni lazima wahakikishe kwamba wanazingatia sheria na pia wanayoyasema ni kwa maslahi ya umma mpana wa Tanzania.

“Vinginevyo, matamko yao yataendelea kuibua maswali na Rais hatakubali wamharibie kwa sababu ameshasema mara kadhaa kuwa daima atakuwa upande wenye maslahi kwa wananchi wake, na hasa wanyonge,” alisema mmoja wa wachambuzi hao.

“Ni vizuri wakaachana na matamko yenye viashiria vya kuwa na kiki za kuonyesha kuwa nao wako vizuri kuendana na kasi ya serikali ya sasa...wasipozingatia hayo kila mara watajikuta wakiwa tofauti,” mwingine aliongeza.

Neno ‘kiki’ ni la mtaani na limejitwalia umaarufu katika siku za hivi karibuni, likitumiwa kumaanisha mbinu zinazoweza kutumiwa na mtu ili kujipatia umaarufu juu ya jambo fulani. Wasanii na wanasiasa huhusishwa zaidi na neno hilo kutokana na asili ya kazi zao ambazo huwakutanisha zaidi na watu.

Awali, katika agizo lake hilo ambalo alilisisitiza pia jana asubuhi wakati akizungumza na kituo kimoja cha redio jijini Dar es Salaam, Mwakyembe alisema wameamua kuzuia ndoa kwa watu wasiokuwa na vyeti vya kuzaliwa kwa nia ya kuondokana na takwimu za sasa zinazoonyesha kuwa Tanzania Bara ni ya mwisho barani kwa utoaji wa vyeti vya kuzaliwa kwa wananchi wake.

Alisema ni asilimia 12 tu ya Watanzania walioko Bara ndiyo wenye vyeti vya kuzaliwa na kuzidiwa hata na Zanzibar yenye wastani wa asilimia 75, hali aliyosema inashangaza kwa sababu bei ya vyeti hivyo ni Sh. 3,500 tu huku gharama za harusi zikiwa kubwa kulinganisha na kiasi hicho.

Hata hivyo, akizungumza na waandishi wa habari muda mfupi kabla ya kuondoka mjini Dodoma na baadaye taarifa yake kusambazwa kwa umma jana, Rais Magufuli alisema anatengua uamuzi huo wa Waziri Mwakyembe kwa sababu utawanyima fursa ya kuoana Watanzania ambao wengi wao hawana vyeti hivyo vya kuzaliwa, hasa wale wa vijijini.

Alisema hadi sasa idadi ya Watanzania walio na vyeti vya kuzaliwa ni chini ya asilimia 20 huku wengi wao wakiwa ni wananchi waishio vijijini ambako ni vigumu kupata vyeti hivyo, na wengine wakiwa ni waliozaliwa kabla ya kuanza kutolewa kwa vyeti vya kuzaliwa nchini mwaka 1961.

“Kwa hiyo ndugu zangu Watanzania msiwe na wasiwasi wowote, endeleeni na utaratibu wenu wa kuoa na kuolewa kama kawaida na kama kuna kifungu chochote cha sheria kinachomlazimisha mtu awe na cheti cha kuzaliwa ndipo aoe ama aolewe nitamuelekeza Waziri wa Katiba na Sheria Mhe. Harrison Mwakyembe apeleke Bungeni kikarekebishwe” alisema Rais Magufuli, huku akitoa wito kwa wanasheria kuziangalia vizuri sheria zinazohusiana na kuzaliwa na kifo na kuoa na kuolewa ili zisilete mkanganyiko kwa wananchi.

JPM ALIVYOZIMA ‘KIKI’
Mbali na tukio la kuzimwa kwa ‘kiki’ ya Waziri Mwkayembe jana, wapo pia mawaziri na viongozi wengine kadhaa wa serikali na taasisi za umma waliokumbana na rungu la Magufuli la kutengua amri au tarifa zao. Hao ni pamoja na Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Walemavu, Jenista Mhagama; Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (Tamisemi), George Simbachawene na Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Nape Nnauye.

Mhagama alikumbana na mkasa huo Machi 3, 2016 wakati alipotoa taarifa ya kumteua Dk. Carina Wangwe kuwa Kaimu Mkurugenzi wa Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF). Hata hivyo, wakati uamuzi wake ukimpa umaarufu siku hiyo kupitia ‘kiki’ za kwenye mitandao ya kijamii, waziri huyo alilazimika kubatilisha taarifa hiyo kabla Rais Magufuli hajamtangaza Prof. Godius Kahyarara kushika nafasi hiyo NSSF.

Agosti 12 mwaka jana, Simbachwene alisisitiza kuondolewa kwa wamachinga maeneo ya mijini. Hata hivyo, siku chache baadaye, Magufuli alitengua agizo hilo wakati akihutubia jijini Mwanza kwa kutaka wamachinga wasiondolewe kwenye maeneo wanayofanyia biashara hadi pale mamlaka husika zitakapohakikisha kuwa zimewatafutia sehemu za kwenda kufanyia biashara zao.

Waziri mwingine aliyekumbwa na rungu la Magufuli hivi karibuni wakati kauli yake ikiwa imepamba moto na kuibua mijadala kwenye mitandao ya kijamii ni Nape.

Machi Mosi mwaka huu, Nape alielezea umuhimu wa kulinda majina ya wasanii waliotajwa hadharani wakituhumiwa kuhusika na dawa za kulevya, akisema kwamba ni vyema kuzingatia nguvu kubwa walizotumia kujijengea majina hayo na kwamba, ifikiriwe pia ni kwa namna gani watasafishwa ikiwa wataonekana baadaye kuwa hawahusiki na dawa za kulevya.

Nape alizungumza hayo akiwa Dodoma na baadaye kwenye kipindi cha Dakika 45 kinachorushwa na ITV kuelezea hatua iliyochukuliwa na Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda, aliyetangaza hadharani majina ya wasanii kadhaa katika orodha yake ya awali ya watuhumiwa 65 wa dawa za kulevya.

Hata hivyo, siku chache baadaye, Magufuli alionekana kupinga maelezo ya Nape kwa kusisitiza kuwa vita dhidi ya dawa za kulevya isiangalie majina ya watu kwa sababu athari zake ni kubwa kwa taifa.

WALICHOSEMA WABUNGE, WASOMI WANENA
Akizungumzia suala la Mwakyembe, Mbunge wa Kibamba, John Mnyika (Chadema), alisema ni ishara kuwa baadhi ya mawaziri na viongozi wengine wamekuwa wakikurupuka kwa kutoa matamko bila kuyafanyia utafiti wa kina na ndiyo maana Magufuli ametengua agizo alilotoa kuhusu amri ya kuzuia ndoa kwa wasiokuwa na vyeti vya kuzaliwa.

Mbunge wa Busega, Dk. Raphael Chegeni (CCM), alisema awali alikuwa haamini na mwishowe akajikuta akisikitika kusikia tamko la Waziri Mwakyembe kuhusu zuio la ndoa kwa wasiokuwa na vyeti vya kuzaliwa kwa sababu agizo lake halikuwa na msingi wa kisheria.

Alisema kupitia mkasa huo wa Mwakyembe, mawaziri wanatakiwa kuwa makini katika kutoa matamko ya aina hiyo na kwamba, kama wana hoja wanatakiwa kupeleka ndani ya Bunge ili ijadiliwe.

“Kama unatoa tamko leo na Rais analipinga ama kulifuta, hiyo inaonyesha kuwa waziri umekurupuka… matamko kama haya yanamgombanisha Rais na wananchi wake. Mawaziri wajiepusha kutoa matamko ambayo hayajapewa ridhaa,” alisema Chegeni.

Mbunge wa Nzega Mjini (CCM), Hussein Bashe, alisema alichokifanya Rais Magufuli kutengua tamko hilo yupo sahihi kwa kuwa suala la ndoa linagusa imani ya mtu na serikali haitakiwi kuingilia, na kwamba kama kuna jambo la kisheria liwasilishwe bungeni ili lifanyiwe kazi.

Mhadhiri wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM), Dk. Richard Mbunda, alisema inavyoonekana, huenda tangazo alilitoa Mwakyembe ni binafsi kwa mtazamo wake baada ya kuona kuna udanganyifu mkubwa katika eneo hilo.

Mkurugenzi wa Kituo cha Sheria na Haki za Bindamu (LHRC), Dk. Hellen Kijo-Bisimba alisema agizo la Mwakyembe kuhusu masuala ya ndoa linashangaza kwa sababu halipo kwa mujibu wa sheria

“Katika Sheria ya Ndoa, vitu ambavyo mtu anatakiwa kuwa navyo ili afunge ndoa ama sifa, hiyo ya cheti (cha kuzaliwa) haipo… sijui huyo Waziri ameitoa wapi na pia ingekuwepo kisheria ingepingwa kwa sababu watu wengi hawana vyeti vya kuzaliwa,” alisema Bisimba.

Mhadhiri wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Dk. Ally Bashiru, alisema ni vyema Rais Magufuli ameingilia na kutengua agizo la Mwakyembe la kuzuia ndoa kwa asiokuwa na vyeti vya kuzaliwa.
Read More

Post Top Ad

Your Ad Spot