Rais wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) ametamka kuwa hataruhusu klabu yoyote kucheza Ligi Kuu Bara kama itakuwa haijawakatia bima wachezaji wake watakaowatumia katika msimu wa 2018/2019.
Kauli hiyo, aliitoa kwenye ufunguzi wa semina ya utawala bora kwa klabu za ligi kuu na Ligi Daraja la Kwanza iliyofanyika jana Rombo Green View iliyokuwepo Ubungo jijini Dar es Salaam ambayo ilihusisha klabu kongwe za Simba na Yanga.
Semina hiyo, iliandaliwa na Kampuni ya Maendeleo na Utafiti wa Michezo (ISDI) kwa kushirikiana na Alliance Life Assuarance na TFF kwa lengo la kutoa elimu kwa viongozi wa klabu kujua jinsi ya utawala, kujiongoza na kutafuta wadhamini.
Akizungumza na Waandishi wa Habari kabla ya kufungua semina hiyo, Karia alisema kikubwa anataka kuona klabu maendeleo na mafanikio kwa klabu hizo huku akiamini kupitia semina hiyo wawakirishi hao watapata elimu nzuri.
Karia alisema, moja ya maendeleo anayotaka kuyaona ni klabu kuwakatia bima wachezaji wake ambalo amepanga kulisimamia mwenyewe na hataruhusu timu yoyote kucheza ligi kama itakuwa haijakamilisha zoezi hilo.
“Niseme kuwa, sitakuwa na masihala juu la hili la bima ni lazima kila klabu iwakatie bima ya afya wachezaji wake na uzuri wapo hapa Alliance Life Assuarance ambao wanausika na bima, hivyo tutazungumza nao kujua jinsi ya kufanya.
“Niseme kuwa, kama klabu haitakuwa imewakatia bima wachezaji wake, basi haitacheza ligi kuu msimu ujao na hilo nitahakikisha ninalisimamia vizuri na kama itakuwepo klabu imeshindwa kutimiza hilo basi itatakiwa kuwasiliana na bodi ya ligi tujue jinsi ya kuwasaidia ili wakatiwe bima,”alisisitiza Karia.
“Na hilo alitaangalia ukubwa wala udogo wa klabu ni lazima kila timu ifuate kanuni za ligi kuu ambazo tumeziweka,”alisema Karia.
SOURCE: global publisher
No comments:
Post a Comment