YANGA SC itaondoka kesho jioni kwa ndege ya Fast Jet kwenda Mwanza
tayari kwa mchezo wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara dhidi ya wenyeji
Mbao FC Jumapili Uwanja wa CCM Kirumba mjini humo.
Lakini Yanga itaondoka bila washambuliaji wake wote vinara wa mabao msimu huu, Ibrahim Ajib na Mzambia Obrey Chirwa.
Katibu Mkuu wa Yanga, Charles Boniface Mkwasa ameiambia Bin Zubeiry
Sports – Online leo Ajib hatakwenda Mwanza kwa sababu anatumikia adhabu
ya kadi tatu za njano wakati Chirwa bado yupo kwao, Zambia kwa matatizo
ya kifamilia.
Katika mabao 17 ambayo Yanga imefunga kwenye Ligi Kuu msimu huu, 11
yanatoka kwa wawili hao, Chirwa akiwa amefunga sita na Ajib matano.
Pamoja na wawili hao, Yanga pia itaendelea kuwakosa wachezaji wake
majeruhi Wazimbabwe, kiungo Thabani Scara Kamusoko na mshambuliaji
Donald Dombo Ngoma pamoja na beki mzalendo, Kevin Patrick Yondan.
Mshambuliaji Ibrahim Ajib hatakwenda Mwanza kwa sababu anatumikia adhabu ya kadi tatu za njano
Mkwasa amesema Chirwa anatarajiwa kurejea nchini kuanzia kesho na hawezi
kujumuishwa kwenye msafara wa Mwanza wazi hatakuwa fiti.
Kwa ujumla Ligi Kuu inatarajiwa kuendelea kesho baada ya mapumziko ya
wiki tatu kupisha michuano ya CECAFA Challenge iliyomalizika nchini
Kenya wiki iliyopita kwa wenyeji, Harambee Stars kuwa mabingwa
wakiwafunga Zanzibar katika fainali.
Kesho Azam FC watakuwa wenyeji wa Stand United Uwanja wa Azam Complex,
Chamazi, Dar es Salaam kuanzia Saa 1:00 usiku na Jumamosi kutakuwa na
mechi tatu, Lipuli na Tanzania Prisons Uwanja wa Samora, Iringa kuanzia
Saa 8:00 mchana, Mtibwa Sugar na Maji Maji Uwanja wa Manungu, Turiani,
Morogoro na Ndanda FC na Simba SC Uwanja wa Nangwanda Sijaona mjini
Mtwara zote zikianza saa 10:00 jioni.
Jumapili, mabingwa watetezi, Yanga watakuwa wageni wa Mbao FC Uwanja wa
CCM Kirumba, Mwanza saa 10:00 jioni na Njombe Mji FC wataikaribisha
Singida United kuanzia saa 8:00 mchana Uwanja wa Saba Saba, Njombe.
Mechi za kukamilisha mzunguko wa 12 zitachezwa mwaka mpya, Januari 1
Mbeya City wakiikaribisha Kagera Sugar Uwanja wa Sokoine mjini Mbeya na
Mwadui wakiikaribisha Ruvu Shooting zote kuanzia saa 10:00 jioni.
Baada ya mechi hizo, Ligi Kuu itasimama tena kupisha mechi za Kombe la
Mapinduzi visiwani Zanzibar na raundi ya tatu ya Azam Sports Federation
Cup (ASFC) itakayochezwa kati ya Januari 5 na 7 mwakani kabla ya kuingia
kwenye mzunguko wa 13 wa ligi kuanzia Januari 13 na 17, 2018.
Post Top Ad
Your Ad Spot
Thursday, December 28, 2017
Home
Unlabelled
Ajibu na Chirwa kutopambana na Mbao FC
Ajibu na Chirwa kutopambana na Mbao FC
About Franxin Photography
Templatesyard is a blogger resources site is a provider of high quality blogger template with premium looking layout and robust design. The main mission of templatesyard is to provide the best quality blogger templates which are professionally designed and perfectlly seo optimized to deliver best result for your blog.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Post Top Ad
Your Ad Spot
No comments:
Post a Comment