Eneo lilikojiri tukio la kulipuka kwa Bomu. |
Na Mwandishi Wetu
Serikali ya Iraq imetangaza siku
tatu za maombolezo ya kitaifa kufuatia maafa yaliyotokea kutokana na
shambulio la bomu ambalo limeua watu wapatao mia 120 katika mji mkuu wa
Baghadad.
Katika shambujlio hilo watu mia na hamsini walijeruhiwa vibaya
wakati lori lililokuwa na milipuko lilipolipuka nyakati za usiku karibu
na msikiti katika wilaya ya Karanda.
Muda mfupi baada ya mlipuko huo Mkuu wa majeshi ya nchi hiyo Major Generali Kadimu Shabaani alifika katika eneo la tukio na kuweza kushuhudia kile kilichojiri katika eneo hilo.
Kutokana na Kutokea kwa mlipuko huo Serikali ya Iraq imeahidi kuwatafuta na kupambana na wale wote waliohusika katika shambulizi hilo ambalo limewaachia watu majonzi makubwa.
No comments:
Post a Comment