Jay Z akiwa na Mkewe. |
Na Mwandishi Wetu
Kampuni ya Apple inadaiwa kutaka kuchukua umiliki wa huduma ya kusikiliza muziki ya moja kwa moja ya mwanamuziki Jay Z 'Tidal'.
Duru zimearifu jarida la Wall Street kwamba mazungumzo yameanza na huenda yakasababisha kupatikana kwa makubaliano.
Msemaji wa Tidal amekana kwamba imefanya mazungumzo na Apple na kuongeza kuwa wataujulisha umma pindi watakapokuwa wamefanya mazungumzo hayo.
Jay Z alizindua huduma hiyo mnamo mwezi Machi mwaka uliopita kama mpinzani wa Spotify.
Jay Z akiwa pamoja na wadau katika kumiliki Kampuni hiyo. |
Jay Z aliandamana na Kanye West.
Alicia Keys na mkewe Beyonce ambao wote ni wadau katika kampuni hiyo.
No comments:
Post a Comment