Wanaotoa Tiba mbadala bila kusajiliwa waonywa - MUANGALIZI

Hot

Post Top Ad

Your Ad Spot

Sunday, July 3, 2016

Wanaotoa Tiba mbadala bila kusajiliwa waonywa

MKURUGENZI wa Baraza la waganga watafiti wa tiba mbadala Wilaya ya Kinondoni Maxmilian Lyana,picha na Mtembezi.com

Na Heriald Mwallow

MKURUGENZI wa Baraza la waganga watafiti wa tiba mbadala Wilaya ya Kinondoni Maxmilian Lyana, amewataka watu wanaofanya kazi za tiba mbadala bila kutambuliwa na Wizara ya afya kuacha mara moja.

Lyana alitoa kauli hiyo jana alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari Ofisini kwake Jijini Dar es Salaam na kuleza kuwa wananchi wengi hawaamini huduma zinazotolewa na mataabibu wa tiba mbadala kutokana na kutampeliwa na watu wanaojifanya ni waganga wakati hawajulikani na wanafanyia kazi zao vichochoroni.

Aliwataka wananchi kuamini matibabu yanayotolewa na waganga wa tiba mbadala waliosajiliwa na  Serikali kupitia Wizara ya Afya, Jinsia, Wazee na Watoto na kutambuliwa na Baraza la waganga watafiti nchini.

Lyana ambaye pia ni Mkurungenzi wa kituo cha Ifakara Herbal Clinic kilichopo Tandale sokoni Jijini Dar es Salaam aliongeza kuwa wananchi wanatakiwa waamini tiba asili kuwa ni tiba sahihi ya magonjwa mbalimbali kutokana na dawa zao kufanyiwa uchunguzi wa kina na kutambuliwa Serikali  na hutibu ugonjwa bila kuacha madhara kwa mgonjwa.

"Tunapata shida ya kutoaminika kwa wananchi kutokana na wahuni kujiingiza na kufanya kazi ya utabibu vichochoroni bila kusajiliwa na hawatambuki na Serikali wala Baraza la watatifiti na hivyo kuwatapeli wananchi, nawaomba wananchi watuamini kuwa dawa zetu zinatibu vizuri tena bila kuacha madhara, nawaomba watumie vituo vya tiba mbadala vilivosajiliwa na kutambuliwa na Serikali, kwenye vituo hivyo nawahakikishia watapata matibabu mazuri na hawatatapeliwa kikiwemo kituo changu ya Ifakara Hebal Clinic " alisema Lyana.

Aliongeza kuwa hapo zamani nchi ilipokuwa haina hospitali kama sasa wazee wetu walitumia dawa za asali na ndio maana waliishi miaka mingi tofauti na sasa,

"Ndugu zangu wazee wetu walitumia dawa hizi ndio maana waishi miaka mingi, dawa hizi hutibu ugonjwa bila kuacha madhara yoyote kwa mgonjwa ikiwa mganga atatengeneza bila kuchanganya na vitu visivyo na umhimu au asipochanganya na makemikali yoyote" alisema Lyana.

Alisema kuwa watu wenye magonjwa ya presha ya kupandana, kisukali , kupooza na magonjwa ya uzazi tiba sahihi wanaweza kuipata kwenye vituo vya tiba madala hasa kituo chake na kuongeza kuwa hata vipimo vya magonjwa hayo baadhi ya matabibu waliosoma wanavyo na vinasaidia kutoa tiba sahihi na kuwasihi wale ambao hawana utaalamu wa vipimo
wasiwadanyanye wananchi badala yake wawaelekeze kwenye vituo vyenye wataalamu wa vipimo ili wapate tiba sahihi.

Alisema kuwa dawa wanazotumia wananchimba wenyewe na kuzitengeneza kisha kuziweka kwenye makopo ili kuzihifadhi sehemu salama zaidi kabla ya  mgonjwa kuzitumia anapohitaji matibabu.

Lyana aliishukuru Serikali kwa juhudi inazozifanya katika jitihada za kukuza huduma zinazotolewa mataabibu wa tiba mbada hasa kwa kuanzisha mabaraza kila sehemu jambo linalowafanya kujitangaza na kupata masoko nje ya nchi.

"Serikali imeamua kuboresha huduma za tiba za asili kwa kutujengea uwezo mataabibu, kutweka kitengo cha kushughulikia tiba mbadala kwenye Wizara ya Afya ili kila taabibu aweze kuchunguzwa huduma zake kabla ya kupewa usajili" alifafanua Lyana.

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Your Ad Spot