SHIRIKA la Kimataifa la Waangalizi wa Haki za Binadamu (HRW) limebaini kwamba sheria za kibaguzi, mazoea, ada ya juu, vurugu, na mambo mengine yanasababisha mamilioni ya watoto na vijana kuwa nje ya shule katika nchi nyingi duniani.
Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa jana na Mtafiti wa Watoto kutoka HRW, Elin MartÃnezka kuhusu ripoti iliyotolewa na shirika hilo juu ya nchi mbalimbali duniani kushindwa na kutotimiza haki za kutoa elimu kwa watoto na vijana.
Alisema kwa mujibu wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Elimu, Sayansi na Utamaduni la, UNESCO, limesema kwamba watoto na vijana takribani milioni 124 wapo nje ya shule.
"Ni jambo lililo wazi kwamba mwaka 2016, mamilioni ya watoto na vijana duniani kote walinyimwa haki yao ya elimu," alisema , mtafiti huyo .
Alisema ufuatiliaji dhaifu wa serikali na ukosefu wa sera zisizo na ubaguzi mara nyingi kutoa fursa kwa maafisa elimu kutumia nguvu na kuamua watakavyo katika suala zima la elimu.
Alisema serikali zote duniani katika miongo miwili iliyopita ziliahidi kuondoa vikwazo vya elimu kwa watoto ili waweze kupa elimu.
Alisema nchi 196 ambazo ni wanachama wa Umoja wa Mataifa walipitisha majukumu ya kisheria kwa watoto wote katika maeneo yao na kuridhia Mkataba wa Haki za Mtoto na mikataba ya kimataifa kikanda na wengine yaliyowekwa ili kulinda haki ya kupata elimu.
Alisema Septemba , mwaka jana , serikali zote zilikubaliana kufanya kazi pamoja na kuhakikisha umoja na ubora wa elimu kwa wote ifikapo mwaka 2030, kama sehemu ya Umoja wa Mataifa.
Alisema pamoja na wajibu katika mikataba mingi ya kimataifa ya kuondoa ada za shule za msingi na gharama zinazohusiana, nchi nyingi, ikiwa ni pamoja na Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo na Afrika Kusini, malipo ya ada yameondolewa kwa familia ambazo haziwezi kumudu.
Alisema gharama kubwa za ada katika ngazi ya sekondari huacha mamilioni ya vijana katika nchi za Bangladesh, Indonesia, na Nepal kukosa elimu.
Alisema kwa mujibu wa Shirika la Umoja wa Mataifa linalohudumia watoto UNICEF, shule zenye vurugu huathiri watoto zaidi ya milioni 246 ambapo adhabu ya viboko shuleni pamoja na mazoezi ambayo ni sawa na mateso na udhalilishaji zina athari hasi juu ya uwezo wa watoto kujifunza hususani katika nchi za Tanzania, Afrika Kusini na baadhi ya majimbo nchini Marekani.
Alitaja mambo yanayosababisha wasichana kuwa nje ya shule kuwa ni pamoja na kuenea kwa vitendo vya unyanyasaji wa kijinsia na unyanyasaji na walimu na wenzao.
No comments:
Post a Comment