wananchi wakichangia damu ili kuokoa maisha ya watu wengine wenye shida ya damu wakiwemo wakina mama na watoto. |
|
Kila mwaka tarehe
14 Juni, dunia inaadhimisha Siku ya Wachangia Damu Lengo la maadhimisho haya ni
kukuza uelewa kuhusu huduma ya damu salama, kuhamasisha jamii kuchangia damu
kwa hiari na pamoja na kuwatambua na kuwaenzi watu ambao wamekuwa wakichangia
damu kwa hiari kuokoa maisha ya wagonjwa wanaohitaji huduma ya kuongezewa
damu. Aidha,Siku ya Wachangia Damu Duniani ni ukumbusho wa siku ya
kuzaliwa ya Ndugu Karl Landsteiner,
ambaye ndiye aliyegundua mfumo wa makundi ya damu ya “A”,”B” na “O”,na alizawadiwa tuzo ya Nobel kutokana na ugunduzi
huo.
Mwaka huu, Wizara ya
Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto kupitia Mpango wa Taifa wa
Damu Salama inaadhimisha Siku ya Wachangia Damu Duniani kwa kuhusisha Mikoa
yote ambayo pia itashiriki katika kampeni ya Siku ya Wachangia Damu Duniani kwa
kukusanya damu kila Mkoa, angalau Chupa za damu 100 kwa kila Halmashauri, Lengo
ni kukusanya chupa 20,000 nchi nzima.
Kitaifa Maadhimisho
haya yatafanyika tarehe 14/6/2016 Mkoani
Dodoma kwa kuhusisha vyuo vikuu vilivyopo Mkoani Dodoma, ambapo vitashiriki
katika zoezi la kuchangia damu. Aidha, kilele cha maadhimisho hayo kilitanguliwa
na kampeni ya siku mbili ya kuhamasisha jamii kuhusu umuhimu wa kuchangia damu
kwa hiari na ukusanyaji wa damu. Ili kuendana na kauli mbiu ya ‘’HAPA
KAZI TU’’ hakutakuwa na sherehe au shamrashamra zozote zaidi ya
kukusanya damu.
Kauli Mbiu ya maadhimisho ya mwaka huu ni “SOTE
TUNAUNGANISHWA NA DAMU (BLOOD CONNECTS US ALL)”. Kauli Mbiu hiyo
inalenga;
- Kuonyesha jinsi gani maisha ya watu yameweza
kuokolewa na watu ambao wamekuwa wakichangia damu.
- Kuhamasisha wachangiaji damu wa kila mara,
waendelee kuchangia damu.
- Kuhamasisha watu wenye afya njema ambao
hawajawahi kuchangia wachangie damu.
- Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia,
Wazee na Watoto kutambua wachangia damu wa kujirudia mara kwa mara na
kuhakikisha upatikanaji wa damu na mazao ya damu ya kutosha kwenye hospitali
zetu.
Ili kuhakikisha kuwa damu ya kutosha inakusanywa
na kupunguza vifo vinatokanavyo na upungufu wa damu, Mpango wa Taifa wa Damu
Salama unafanya kazi ya kukusanya damu kwa kushirikisha Halmashauri zote
nchini. Huu ni mkakati ambao ulibuniwa ili kuongeza makusanyo ya damu ambayo
mahitaji yake kwa mwaka ni chupa 450,000. Kwa mujibu wa
Shirika la Afya Duniani mahitaji ya damu salama ni asilimia moja (1%) ya idadi
ya watu wote. Mkakati wetu mpya wa kuhakikisha damu inakusanywa kwa
kushirikisha Halmashauri pia umesaidia kusogeza huduma karibu na wananchi.
Mkakati huu umeanza kuzaa matunda kwani taarifa
ya robo mwaka (Januari - Machi 2016) inaonyesha jumla ya chupa za damu 42,978
zilikusanywa toka mikoa yote hapa nchini, ambayo ni asilimia 101 ya
lengo la kukusanya chupa 42,500 Aidha, kwa
mwaka 2016/2017 Mpango wa Taifa wa Damu Salama umejiwekea lengo la kukusanya
chupa 300,000, ambapo kati ya hizo, chupa 160,000 zitakusanywa kwenye Kanda 6
za Mpango wa damu salama ambapo inakadiriwa chupa zipatazo 140,00 zitakusanywa
na Halmashauri zote nchini.
Wizara inatambua mchango wa wanahabari katika
kuihabarisha jamii kuhusu huduma ya damu. Hivyo napenda kuchukua fursa hii
kuwashukuru sana wanahabari kwa kuendelea kuelimisha jamii yetu kuhusu umuhimu
wa kuchangia damu kwa hiari.
“Ninapenda
kuwashukuru na kutambua wanahabari na vyombo vya habari ambayo vimekuwa mstari
wa mbele katika kuhamasisha jamii kuhusu kucnagia damu kwa hiari. Tunawashukuru
sana.”
“Aidha, Wizara yangu inatoa shukurani kwa
wachangia damu mmoja mmoja na Taasisi mbalimbali zikiwemo shule, vyuo na
madhehebu ya dini kwa ushiriki wao katika kuchangia damu. Pia, Natoa shukurani
za dhati kwa mashirika mbalimbali kama Shirika la Marekani la Kudhibiti na
Kuzuia Magonjwa (CDC), Shirika la Afya Duniani (WHO) na Mfuko wa Dunia
(Global Fund) kwa misaada ambayo wamekuwa wakitoa kwa Mpango wa Taifa wa
Damu Salama katika kuhakikisha upatikanaji wa damu salama nchini.”
“Pia tunamshukuru Mhe. Dkt. John Pombe
Magufuli, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa uamuzi wake wa kutoa
msamaha wa ushuru wa forodha kwa chupa zinazotumika kwa ajili ya kukusanya damu
kwenye hospitali (blood collection tubes). Hakika uamuzi wake huu utaokoa
maisha ya maelfu ya watanzania hasa wanawake wajawazito wanaofariki kwa kukosa
damu. Tunamshukuru sana.”
Damu salama ni muhimu katika utoaji huduma za
Afya. Bila damu hakuna maisha, hivyo ni lazima tuhakikishe uwepo wa damu salama
wakati wote kwenye Hospitali/Vituo vya kutolea huduma za Afya.
No comments:
Post a Comment