Staa wa filamu Bongo Jacob Stephen ‘JB’ na mtangazaji wa EFM, Dina Marios wamewafungukia mastaa na mashabiki wao kuwa wao wanajishughulisha bila aibu na kilimo kama fursa ya biashara na chanzo cha chakula na kuwataka na wao wajitokeze kwa wingi kulima.
Hayo waliyaongea katika hafla ya kutangaza majina ya washiriki 19 kati ya washiriki 3000 waliotuma fomu zao kutoka sehemu mbalimbali nchini kushiriki shindano maarufu la Mama shujaa wa Chakula linaloendeshwa na shirika la Oxfam.
Hafla hiyo ilifanyika katika kituo cha mazoezi cha Azura jijini Dar ambapo Jb na Dina walikuwa majaji wa washiriki hao huku wakiwakilisha kama mabalozi wa kampeni ya Grow.
Shindano la mama shujaa wa chakula 2016 linatarajiwa kufanyika katika kijiji cha Enguiki kilichopo Monduli Mkoani Arusha, kuanzia septemba 25 hadi Oktoba 16 na kurushwa katika kituo cha ITV.
Washiriki wa Mama Shujaa wa Chakula 2016 kuwa ni Betty Nyange (62) Mkoa wa Morogoro, Monica Charles Mduwile (44) Mkoa wa Dodoma, Neema Gilbet Uhagile (29) Mkoa wa Njombe, Mary Christopher Lyatuu (29) Mkoa wa Arusha, Loyce Daudi Mazengo (39) Mkoa wa Singida, Anjela
Chogsasi Mswete (48) Mkoa wa Iringa, Lucina Sylivester Assey (54) Mkoa wa Shinyanga, Marta Massesa Nyalama (50) Mkoa wa
Kaskazini Unguja, Christina Machumu (42) Mkoa wa Mara, Happiness Paulo Raulent (35) Mkoa wa
Kagera.
Mary Bony Soko (42) Mkoa wa Ruvuma, Mary Ramadhani Mwiru (39) Mkoa wa Kilimanjaro, Mwanaid Alli Abdalla (53) Mkoa wa Mjini Magharibi, Maria Alfred Mbuya (43) Mkoa wa Mbeya, Eliza Richard Mwansasu (30) Mkoa wa Rukwa, Mwajibu Hasani Binamu (46) Mkoa wa Mtwara, Eva Haprisoni Sikaponda (40) Mkoa wa Songwe, Hidaya Said Musa
(40) Mkoa wa Tanga na Mwasiti Salim Mazuri (40) Mkoa wa Dar es salaam Wilaya ya Kinondoni.
No comments:
Post a Comment