Makami wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan |
MAKAMU wa
Rais Samia Suluhu, amewataka watanzania kuyatunza magari ya Mradi wa Mwendo
Kasi Dar es Salaam (DART) ili yaweze kudumu.
Makamu wa
Rais Samia, aliyasema hayo Dar es Salaam
jana, wakati wa kuyakagua magari hayo ambapo aliwataka madereva wa magari hayo
kufuata sheria na kuyatunza yawe endelevu.
"Watanzania
huu mradi wenu nawaomba myatunze magari haya msiyafuje yakaharibika mapema
tutunze kiweze kudumu."alisema
Samia.
Alisema
magari hayo ni mazuri yakitunzwa vizuri yataweza kutoa huduma bora ndani ya
mkoa huo madereva wakifuata sheria.
Kwa upande
wake Mmiliki wa Mradi huo,Robart Kisena alisema kwa sasa madereva wa mradi huo
wanaendesha kwa kufuta sheria za usalama barabarani na kiwango cha ajali
kimepungua.
Robart
alisema awali mradi huo wakati unaanza ajali zilikuwa nyingi ila kwa sasa
madereva wake wamepata elimu ya kutosha ajali kwa sasa zimekwisha tofauti na
awali.
Aliwataka madereva wa DART kufuata sheria na kanuni za
usalama barabarani ili wasisababishe ajali za kizembe ambazo zinaweza
kuzuilika.
Alisema
dereva akiwa makini pindi anapokuwa barabarani awezi kusabisha ajali madereva
wake wamepata elimu ya kutosha katika mradi huo.
Wakati
huohuo Kisena alizungumzia suala la mgomo kwa madereva wanaotaka kugoma wakidai
maslai yao,alisema taarifa hizo yeye ana hila jana madereva wote wamesaini
mikataba mipya.
Kisena
alisema taarifa za madereva wa DART kugoma aijamfikia katika ofisi yake kama
zipo atazitolea ufafanuzi baadae.
No comments:
Post a Comment