Mkali wa RnB Tanzania, a.k.a Moyo mashine ameongelea hatua ya msanii Diamond kumsaini
msanii mkubwa kama Rich mavoko kwenye label yake ya WCB.
Akiongea na mwandishi wetu
kipindi cha karibuni, Ben pol amesema kuwa hatua ya Diamond platnumz kumsaini
msanii mkubwa kama Rich mavoko katika label ya WCB in kitendo kizuri na
kutafungua njia kwa wasanii wengine kuwa na moyo wa kusaidiana wenyewe kwa wenyewe.
“Ni vizuri sisi kwa sisi tukiaminiana na kufanya kolabo kwenye kazi, Diamond ni mpiganaji na Rich mavoko ni msanii mwenye kipaji na mjanja kwahiyo kufuatia muungano wao unaleza ukaleta mapinduzi makubwa katika muziki”. Alisema Ben pol
Pia mkali huyo wa moyo
mashine amewataka wasanii wenye uwezo wa kuwasaidia wasanii wengine wasisite
kuwasaidia wenzao kwani hiyo ndio njia pekee ya kuupeleka muziki wa Tanzania
kufika mbali.
No comments:
Post a Comment