Diwani aapa kupambana na uhalifu - MUANGALIZI

Hot

Post Top Ad

Your Ad Spot

Tuesday, June 14, 2016

Diwani aapa kupambana na uhalifu

DIWANI wa Kata ya Makangarawe Manispaa ya Temeke Dkt.Idd Mahuta amesema kuwa yupo tayari kupoteza kura katika uchaguzi ujao wa 2020 lakini kamwe hawezi kukubali kata yake kuwa kichaka cha wahalifu badala yake atahakikisha wahalifu wote wanafikishwa kwenye vyombo vya sheria.


Akizungumza hayo Dar es Salaam juzi  katika mkutano wa wananchi wa ulinzi na usalama katika mtaa wa Yombo Dovya wilayani humo,alisema kuwa yeye ni mkuu wa amani katika kata hiyo hivyo hawezi kuona vitendo viovu vikiendelea hivyo atahakikisha anapambana ili kukomesha kabisa tabia hizo.


Alisema kuna baadhi ya  tabia ambayo imejengwa ya wazazi kuomba msaada kwake pindi vijana wao wanapokamatwa kwa makosa mbalimbali ya kihalifu hivyo kuazia sasa hayupo tayari kusikiliza jambo lolote linalohusu uhalifu kutoka kwa mzazi nakudai na  yupo tayari kunyimwa kura kipindi cha uchaguzi 2020.


"Nataka niwaambie kuwa nipo tayari kunyimwa kura lakini siwezi kuvumilia kulea makundi ya vijana ambayo ni hatarishi katika jamii eti kwa sababu ya kuogopa kupigiwa kura mwaka 2020,nasema kuazia sasa Ofisi yangu kwa kushirikiana na mkuu wa kituo cha Polisi Temeke pamoja na viongozi wengine tutapambana na vitendo hivi vya kihalifu na ninyi wazazi zungumze na watoto wenu."alisema Diwani Dkt. Mahuta

Aliongeza kuwa huko nyuma wazazi wengi walikuwa wanakwenda kwake ili kumtaka asaidie kutolewa zamana kwa vijana wao pindi wanapokamatwa na Polisi kwa makosa mbalimbali ikiwemo vitendo vya kihalifu nakudai kwamba hivi sasa wala wasijisumbuwe.

Kwa Upande wake Mkuu wa kituo cha polisi (Ocd)kutoka Temeke,Msuya Muhudhwari aliwataka wananchi hao kuwafichua vijana wanaofanya uhalifu ikiwa pamoja na kutoa taarifa zao Polisi ili wawe kushughulikiwa.

Pia alionya wazazi hao kutoruhusu ngoma aina ya Vigodoro katika maeneo yao kwani michezo hiyo kwa asilimia kubwa inasababisha kuwepo kwa vitendo vya kiharifu,ambapo alidai kuwa idadi kubwa ya vijana wanaojitokeza kwenye ngoma hizo ni wahalifu.

"Kwanza mavazi yanayovaliwa katika ngoma hizi hayana heshima katika jamii yetu ya kitanzania lakini pia asilimia kubwa ya watu wanaokuja ni makundi ya vijana ya kihalifu ambapo wengi wao wanasababisha uvunjifu wa amani katika eneo husika."alisema Ocd Muhudhwari

Naye Mwenyekiti wa Serikali ya Mtaa huo wa Yombo Dovyo Bruce Mbagwile aliwaeleza wazazi hao kuwa atakayebainika mtoto wake hajampeleka shule basi ajuwe polisi itamwita kwani hawako tayari kuona watoto wanazagaa mtaani bila kwenda shule.

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Your Ad Spot