KOCHA wa timu ya Taifa ya Cameroon Hugo Broos amekisifia kikosi chake kwa kucheza jihadi kuhakikisha wanaibuka na ushindi dhidi ya Guinea Bissau bao 2-1.
Mchezo huo wa kundi A,ulikuwa vuta ni kuvute kutokana na Guinea Bissau kuonyesha kandanda safi licha ya kuwa mara ya kwanza kushiriki michuano hiyo.
Kocha wa Cameroon, Hugo Broos |
Katika mchezo huo Cameroon walionekana kutafuta ushindi kwa udi na uvumba licha ya Guinea Bissau kuonyesha upinzani wa hali ya juu.
“Licha ya mchezo kuwa mgumu lakini najivunia wachezaji wangu walionyesha ushirikiano wa hali ya juu Uwanjani kuhakikisha tunaibuka na ushindi na kupata pointi tatu muhimu",.
Cameroon ndio vinara wa kundi A wana pointi 4 huku wakiwa na matumaini ya kucheza Robo fainali, pia wanatarajia kucheza na Gabon katika mchezo wa mwisho.
No comments:
Post a Comment