Na Francis Michael
Diamond
Platnumz na Zari the Bosslady wapo kwenye mtihani mgumu unaozikumba familia
nyingi za Kiafrika – maelewano hafifu na ndugu wa ukweni!
Mama
Tiffah yupo mjini alipokuja kumsalimia mchumba wake huyo na kusherehekea siku
ya kuzaliwa ya mama mkwe wake.
Licha
ya Diamond kupost kipande cha video controversial Instagram wakiwa bafuni na
mpenzi wake – wengi wanasema uso wa Zari unaonesha sura tofauti, ya huzuni
tofauti na anavyoonekana mwenzie.
Kuna
mengi yalitokea kwenye birthday ya Mama Diamond na ambayo yanazungumzwa kwenye
mitandao ya kijamii kuanzia urafiki usio wa kawaida wa dada yake Diamond, Esma
na Hamisa Mobetto na mengine. Esma amelifafanua hilo kwa post ndefu Instagram.
Lakini
kubwa ni ujumbe wa kutatanisha wa Zari kwenye mtandao wa Snapchat unaoelezea
jinsi ambavyo hajali ukoo mzima usipomkubali.
“Hakuna mtu mwenye uhusiano na dunia
nzima, nchi au ukoo,” aliandika kwenye Snapchat, mtandao ambao wasanii
wanaamini wana uhuru wa kufunguka zaidi.
“Huwa
na uhusiano na mwanaume au mwanamke wao, ni mimi na yangu tu ndivyo vyenye
maana. Unataka kujua kwanini? Ni sababu ilikuwa ni nyie wawili tu pindi
mlipokutana. Na itakuwa ninyi wawili tu pindi mambo yakienda kombo kati yenu.
Haitakuwa ukoo au nchi au mtu mwingine wa tatu,” aliongeza.
Bi.
Sandra ambaye ni mtumiaji mzuri wa Instagramm aliweka petroli kwenye moto baada
ya kupost picha ya Wema na Idris na kuwasifia: Uzalendo kwanza, umependeza
sanaa mamy akee..”
Binamu
wa Diamond, Romy Jones naye amepost picha kumpongeza shemeji yake wa zamani. Wanasema
ushemeji haufagi lakini.
Kuna
mjadala mzito Instagram kuhusu issue hii.
Tetesi
za kuwa Zari hana maelewano mazuri na ndugu zake na Diamond zimekuwa
zikiandikwa kwa muda mrefu na magazeti ya udaku. Kwa yaliyotokea, kuna asilimia
nyingi za ukweli ndani yake.
Hakika Diamond kazi anayo!
Hakika Diamond kazi anayo!
No comments:
Post a Comment