msanii wa bongo fleva msami mkali wa mabawa akiwa na kipenzi chake kajala |
Na Francis Michael.
Msanii Msami ambaye kwa sasa anafanya poa na
wimbo wake wa ‘Mabawa’ amefunguka na kusema kuwa yeye ni mwanaume na Kajala ni
mwanamke hivyo kwa kile ambacho kinazungumzwa na watu kuwa huenda anatoka naye
kimapenzi
‘Si jambo baya kwani Kajala ni mtoto wa kike na
yeye ni mwanaume hivyo chochote kinaweza kutokea kati yao’.
Msami alisema hayo kupitia kipindi cha eNEWS na
kudai kuwa maneno yanazungumzwa juu yake na Kajala huenda yapo na kama hayapo
labda yanaweza kuja kutokea, ila anadai yeye na Kajala ni washikaji, ambao
wamekuwa wakishirikiana na kusaidia mambo mengi.
“Unajua Kajala ni mtu wangu wa karibu sana,
tunaongea mengi na kushauriana vingi japo ukaribu wetu umetafsiriwa tofauti na
baadhi ya watu wakidhani tunatoka kimapenzi, japo si vibaya kwani sioni kama
kuna ubaya mimi kutoka na Kajala. Sijasema nina mahusiano na Kajala ila
ikitokea tukawa wapenzi tunaweza kuzungumza mimi na yeye kujua hatma yake na
mume wake ambaye anatumikia kifungo kwa sasa” alisema Msami
No comments:
Post a Comment