Wanawake warembo ni tishio afya za wanaume - MUANGALIZI

Hot

Post Top Ad

Your Ad Spot

Wednesday, July 6, 2016

Wanawake warembo ni tishio afya za wanaume


Mwanamke Mzuri
Mwanamke Mzuri wa Kiafrika
Na Mwandishi Wetu

UTAFITI umebainisha kuwa, wanawake wenye mvuto (warembo ) ni hatari kwa afya za wanaume pindi wanapokutana japo kwa dakika tano.

Kwa mujibu wa utafiti huo, kutoka kwa watafiti wa Chuo Kikuu cha Valencia kilichopo nchini Hispania wamebainisha kuwa, dakika tano pekee zinatosha kupandisha kiwango cha homoni za Cortisol mwilini pale mwanaume anapokutana na mwanamke mwenye mvuto.

Homoni ya cortisol, ni aina ya homoni ambayo hutolewa na tezi ya mwili huku ikisafirishwa kupitia mfumo wa mzunguko wa damu hadi katika ogani za mwili.

Utafiti huo, unabainisha kuwa hali hiyo inaweza kuongezeka zaidi kama mwanaume huyo anamini kuwa mrembo huyo sio saizi yake.

Kwa mujibu wa utafiti huo uliochapishwa katika mtandao wa Yahoo hivi karibuni, Chuo Kikuu hicho kilichopo nchini Hispania kilichapisha matokeo ya utafiti huo baada ya kuwachunguza wanaume wapatao 84 ambao ni wanafunzi kwa kuwaweka katika chumba na kuwapa chemsha bongo ya Sudoku.

Utafiti huo unabainisha kuwa, hali ilibadilika pale alipoingia mwanamke mrembo mwenye mvuto katika chumba hicho na kujikuta wakiwa wawili tu, ambapo viwango vya homoni za cortisol za mwanaume ziliongezeka, jambo ambalo ni kinyume na alipoingia mwanaume na kuachwa wakiwa wawili tu.

Kutokana na hali hiyo, watafiti walihitimisha baada ya kuwachunguza wanaume 84 kuwa, wanaume wengi wanapokuwa na wanawake wenye mvuto hubadilika mitazamo na huwa ni rahisi kuingia mtegoni.


Utafiti uliendelea kuthibitisha kuwa, wanaume wengine huwakwepa wanawake wenye mvuto kwa sababu wanaamini kuwa sio saizi yao.

Aidha, utafiti huo umeonesha kuwa homoni za cortisol kwa wanaume huongezeka katika dakika tano tu anapokutana na mwanamke kijana mrembo mwenye mvuto.

Hata hivyo, wataalam wanasema ongezeko la homoni za cortisol linaweza kuwa halina madhara kama ongezeko lake ni kiwango kidogo, kwani husaidia kutahadharisha.

Aidha, inapokuwa imekithiri,  homoni ya cortisol inaweza kuleta madhara makubwa hasa magonjwa ya moyo, kisukari na kupatwa na mshtuko usio wa kawaida.

Haya yanajiri ikiwa huko nyuma imewahi kubainika kuwa kwa wanaume, homoni nyingi ya cortisol inayotolewa kwa shinikizo la msongo huathiri ufanyaji kazi wa kawaida wa mfumo wa uzalishaji.
Pia msongo wa hali ya juu husababisha homoni ya testosterone kutokufanya kazi vizuri na kusababisha utengenezaji wa shahawa kuwa mdogo ambao huleteleza ugumba wa muda.

Kwa wanawake msongo husababisha kuingia mara kwa mara kwenye hedhi na tarehe kutokua za uhakika za kuingia kwenye siku zao au kusababisha tumbo la hedhi kuuma sana na kupunguza hamu ya kushiriki tendo la ndoa.

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Your Ad Spot