Breaking News: Messi ahukumiwa ‘kufungwa miezi 21 jela’ - MUANGALIZI

Hot

Post Top Ad

Your Ad Spot

Wednesday, July 6, 2016

Breaking News: Messi ahukumiwa ‘kufungwa miezi 21 jela’


Mchezaji wa Barcelona, Lionel Messi
Na Carlos Nichombe
Mchezaji nyota wa Argentina na Barcelona Lionel Messi amehukumiwa kifungo cha miezi 21 jela baada ya kupatikana na makosa ya kutumia ulaghai wakati wa ulipaji ushuru, vyombo vya habari nchini Uhispania vinaripoti.

Babake Lionel Messi, Jorge Messi, naye amehukumiwa kufungwa jela kwa kuilaghai Uhispania €4.1m (£3.2m; $4.6m) kati ya 2007 na 2009.

Wakati wa kesi, waendesha mashtaka walisema maeneo salama yenye kinga dhidi ya ushuru Belize na Uruguay yalitumiwa kuficha mapato kutokana na uuzaji wa haki za picha za mchezaji huyo.

Mchezaji wa Barcelona, Lionel Messi
Lakini Messi amesema hakufahamu lolote kuhusu masuala yake ya kifedha na kuongeza kuwa hakuona haja ya yeye kuweza kushitakiwa kwa kuwa mambo yote alimuachia mtu mwingine ambaye alikua akisimamia shughuli zote zimuhusuzo yeye.

Wawili hao hata hivyo hawatarajiwi kufungwa jela kutokana na utaratibu uliopo nchini uhispania kuwaruhusu wao kutumikia vifungo vya nje.

Chini ya mfumo wa haki nchini Uhispania, mtu anaweza kutumikia kifungo chochote kilicho chini ya miaka miwili nje ya gereza hivyo kauli hiyo ya haki za binadamu itawasaidia wao kuweza kutumikia kifungo hicho nje ya Gereza.

Messi na babake pia wanaweza kukata rufaa katika Mahakama ya Juu nchini humo kwa ajili ya kupinga uamuzi uliofikiwa na mahakama iliyotoa hukumu kwao.

Ikumbukwe kuwa Messi amepatwa na Jambo hilo Siku kadhaa baada ya kutangaza uamuzi wake wa kustaafu soka la kimataifa mara baada ya timu yake kung'olewa kwenye kinyang'anyiro cha kukata na shoka.

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Your Ad Spot