Na Carlos Nichombe.
KATIBU wa Jamaat Answar Suna Wilaya ya Ilala, Is-Haqa Lally amewataka Waislamu nchini kudumisha na kutunza amani siku zote kama walivyofanya katika mwezi wa Ramadhani.
Lally aliyasema hayo Dar es Salaam jana alipokuwa akizungumza na waumini wa dini ya kiislamu wakati wa mashindano ya kusoma Qur-an
kwa watoto walio
chini ya miaka 15
Alisema waislamu wanapaswa kudumisha amani iliyopo katika taifa kama walivyofanya katika kipindi cha Ramadhani na kuongeza kuwa endapo wasipoitunza amani hiyo taifa linaweza kuingia katika machafuko.
"Taifa likikosa Amani hata watu wake hawawezi kufanya ibada zao, hivyo niwatake waislamu wenzangu tuweze kufanya mambo yaliyo mema kwani tukifanya mambo mabaya hatutoweza kufanya ibada wala shughuli yoyote ya kupata na kukuza vipato vyetu," alisema.
Aliongeza kuwa waislamu wanatakiwa kuwa watu wa kwanza kuwafichua na kuwapinga watu wenye nia ya kuvunja amani iliyopo kwa madai ya kukuza dini ya Uislamu pamoja na kuwaondoa wale waendao kinyume na matakwa ya dini hiyo.
Kwa Upande wa Mratibu wa Mashindano hayo ya Kusoma Qur-an, Sheikh Salum Luanja aliitaka Serikali kuwawezesha waalimu wa dini ili kuweza kujenga kizazi kitakachokuwa na hofu ya Mungu ambacho kitapunguza kufanya mambo mabaya.
Alisema endapo Vijana watakuwa wameshika dini itawajengea uwezo wa kumcha Mungu na itasaidia kupunguza vitendo vibaya nchini ikiwemo Ujambazi, Ufisadi pamoja na Mauaji.
"Sisi ndio watu tunaoweza kuitengeneza jamii kwa kutumia mafundisho ya dini hivyo Serikali iwe karibu nasi ili tuweze kutoa elimu bora zaidi itakayoweza kulinufaisha taifa,"alisema Luanja

No comments:
Post a Comment