Vilainishi |
SHIRIKA la Viwango Nchini(TBS) jana limeendelea na operesheni ya kuondoa bidhaa hafifu sokoni kwa kukamata zaidi ya lita 400 za virainishi katika baadhi ya maduka ya jumla yaliyopo Kariakoo.
Akizungumza wakati wa operesheni hiyo Mkaguzi Afisa Viwango wa Shirika hilo, Yona Afrika, alisema kuwa katika zoezi hilo wamebaini kwamba vilainishi vingi vilivyopo sokoni vipo chini ya kiwango kwa kuwa kwenye daraja E na kushuka chini
Alisema kuwa vilainishi hivyo ili viwe bora ni lazima viwe na viwango vya daraja F kwenda juu na kwamba vilainishi vyote vitakavyo bainika havina viwango vya ubora vitaondolewa sokoni.
"Katika operesheni hii tumebaini kwamba vilainishi vingi vilivyopo madukani hususani kariakoo havina ubora viko katika daraja F hivyo vinaweza kusababisha madhara makubwa kwenye injini na mitambo," alisema.
Kwa upande wake, Afisa Habari wa TBS, Neema Mtemvu, aliwataka wafanyabiashara wote kuhakikisha kwamba wanazingatia taratibu za kuingiza bidhaa.
Alisema kuwa TBS haitasita kuwachukulia hatua za kisheria kwa wafanyabiashara ambao wamekuwa wakikiuka kanuni kwa kuingiza nchini bidhaa zisizo na viwango.
Alisema kuwa jana wameanza na bidhaa za virainishi vya injini na mitambo lakini zoezi hilo pia litaendelea katika bidhaa nyingine lengo likiwa ni kuhakikisha kwamba Tanzania ina kuwa ni sehemu ya kuwepo kwa bidhaa bora na zinazokidhi viwango.
No comments:
Post a Comment