Mabasi yaendayo mikoani yakiwa yamepaki katika kituo cha ubungo, picha na Global.Info |
MEYA, wa jiji la Dar es Salaam, ambaye pia ni Diwani wa Kata ya Vijibweni Isaya Mwita, amesema hakuna namna ya kufanya wamiliki wa magari yanayosafirisha abiria mikoani kutoka Kituo Kikuu cha Mabasi Ubungo (UBT), kulipa tozo ya sh. 7000 kama ilivyopangwa.
Meya huyo aliyasema hayo, baada ya kusikia kwamba kunamvutano kati ya wamiliki wa magari hayo na mamlaka zunazo kusanya tozo hizo juu ya ongezeko la tozo ambazo wameelekezwa hivi karibuni.
Akizungumza Dar es Salaam jana kwa njia ya simu Isaya , alisema, licha ya kuwataka wamiliki hao kulipa tozo hiyo, hivi sasa anajipanga kukutana na wa miliki hao ili kufanya majadiliano ya pamoja na kwa kina juu ya maamuzi hayo.
Alisema uamuzi wa kuwataka kuendelea kulipa tozo hiyo hakutokani na mtu moja moja bali umetokana na sheria ndogondogo iliyoanzishwa mwaka 2009 ambayo ni marekebisho ya mwaka 2004 iliyokuwa ikitumika kinyume cha sheria ambapo wamiliki hao waliitumia kwa muda mrefu.
"Hapana hakuna nilipotaka kwa kusema kwamba wasilipe tozo hiyo nilichosema, ni kwamba waendelee kulipa tozo hiyo nikiamanisha hiyo ya mwaka 2009.
"Kama wamiliki na wananchi wanakumbuka vizuri kuchechelewa kutumika Sheria hiyo ya mwaka 2009 kumesababisha Rais John Magufuli kutengua uteuzi wa aliyekuwa Mkurugenzi wa Jiji hilo, Wilson Kabwe ambaye hivi sasa ni marehem,"alisema Mwita.
Alisema katika kuliweka sawa suala hilo, amemyagiza Ofisa Habari wa Jiji, Gaston Makwemba, kuandaa kutano utakaowakutanisha kati yake na wamiliki hao, hivi karibuni.
Licha ya kukutana na wamiliki hao, bado anaamini kuwa kuna makosa yaliofanyika huko nyuma hivyo kwa kulitambua hilo, mipango ya jiji bado inasisitiza kuwa lazima kituo hicho kihamishwe na kupelekwa Mbezi kama ilivyokusudiwa awali.
Tangu Julai mosi mwaka huu, kumezuka mvutano kati ya wamiliki wa vyombo hivyo kupinga tozo ya sh. 7000 ambayo ilitatangazwa hivi karibuni na Jiji.
Wamiliki hao wanapinga kwa vile tangu wameanza kulipa tozo hiyo kwa muaka mingi bado kituo hicho kimeendelea kukosa huduma zinazolingana na thamani ya fedha zinazolipwa ikiwa ni pamoja na zile wanazolipa abiria.
No comments:
Post a Comment