Mwanariadha Oscar Pistorius akiondolewa mahakamani |
Na Mwandishi Wetu.
Bingwa wa mbio za Olimpiki za
walemavu Oscar Pistorius, kutoka Afrika Kusini, amehukumiwa kufungwa
jela miaka sita kwa kumuua mpenzi wake mwaka 2013.
Mawakili wa upande wa mashtaka na wa upande wa mshtakiwa wanaweza kukata rufaa ya kupinga matokeo ya hukumu hiyo kama hawatokubaliana nayo.
Uamuzi wa mahakama nchini umetolewa baada ya kubatilishwa kwa hukumu ya awali ya kumuua bila kukusudia aliyekuwa mpenzi wake mwezi Desemba baada ya upande wa mashtaka kukata rufaa ya kutoridhishwa na hukumu hiyo.
Pistorius mwenye miaka 29, alimpiga risasi mara nne Reeva Steenkamp ambaye alikuwa mpenzi wake February 2013.
Pistorius amepelekwa jela ya Khosi Mampuru mjini Pretoria kwa ajili ya kuanza kutumikia adhabu hiyo huku akisubiri mawakili wake wa upande wa utetezi kwenda kukata rufaa itakayomuwezesha kutoka nje ya gereza hilo.
No comments:
Post a Comment