MWENYEKITI wa Chama cha Tanzania Labour Party (TLP), Augustino Mrema |
Jana
Rais Magufuli alifanya uteuzi wa viongozi na watendaji wa taasisi
mbalimbali za serikali huku akimteua Mrema kuwa mwenyekiti wa bodi hiyo
katika kipindi cha miaka mitatu.
MWENYEKITI wa Chama cha Tanzania Labour
Party (TLP), Augustino Mrema, amefurahia uteuzi wake wa kuwa Mwenyekiti
wa Bodi ya Taifa ya Parole huku akieleza Rais John Magufuli amelipa
ahadi yake aliyomwahidi wakati wa kampeni ya uchaguzi Mkuu.
Akihojiwa jana kwa njia ya simu, Mrema alisema anamshukuru Rais Magufuli kwa kumpatia nafasi hiyo na ameoonyesha ni mtu ambaye anatekeleza ahadi zake.
“Rais alivyokuja Vunjo katika kampeni zangu aliwaambia wannachi wamchague Mrema kwa kuwa ni jembe na akawaambia wasiponichagua atanipa kazi watu wakajua ni utapeli wa kisiasa sasa wajue kuwa Rais huwa anaishi kwa ahadi na amenipa kazi ambayo ninaijua,” alisema Mrema
No comments:
Post a Comment