Mstahiki Meya wa manispaa ya Kinondoni Boniface Jacob |
WAZABUNI 9 katika Manispaa ya Kinondoni waliopewa jukumu la kutengeneza madawati kwa shule za Msingi wakishindwa kutekeleza agizo hilo kutumbuliwa jipu.
Hayo yalisemwa na Meya wa Manispaa hiyo,kwa tiketi ya( CHADEMA)Boniface Jacob,wakati wa kuzungumza na waandishi wa habari wakati wa afla yakusaini mikataba ya kutengeneza madawati yenye thamani ya sh,bilioni 1.6
"Leo nimewasainisha mikataba hii kwa ajili ya kutengeneza madawati ya shule za msingi na Sekondari na Mzabuni atakaye shindwa kutekeleza maagizo hayo namuondoa katika kazi ndani ya halmashauri yangu"alisema Jacob.
Jacob alisema katika mikataba waliosaini amewataka mpaka kufikia Juni 31 mwaka huu wawe wameshakamilisha mpango huo wa Serikali katika sekta ya elimu.
Aliziomba kampuni wadau,watu binafsi,wafanyabiashara na makundi taasisi na mashirika ndani na nje ya wilaya hiyo, kuunga mkono jitihada zinazofanywa na serikali kuu na halmashauri kuweka mazingira mazuri ya kutoa elimu bure.
.Aidha alisema mpaka kufikia Juni 31 mwaka huu tatizo la madawati litakuwa limekwisha ndani ya manispaa hiyo ambapo watakuwa wamepata jumla ya madawati 12,091 kwa shule za msingi na viti 6,552 na meza 6,552 kwa shule za sekondari.
Alisema halmashauri hiyo imeamua kutoa zabuni kwa wakandarasi 9 ili kuwezesha kazi hiyo ya madawati kwa wakati na kwa ubora utakaolingana na thamani ya fedha itakayotumika.
"Nawakikishia wananchi wangu wote wa Wilaya hii kuwa manispaa itaendelea kushirikiana na wadau wengine kutatua kero mbalimbali katika sekta ya elimu na sekta nyingine ili kufikia malengo ya kutoa huduma bora kwa wananchi.
No comments:
Post a Comment