![]() |
Aliyekuwa mwenyekiti wa Chama cha CUF akizungumza na waandishi wa habari(hawapo pichani) katika ofisi za chama hicho |
SIKU moja baada ya aliyekuwa Mwenyekiti wa Chama cha Wananchi CUF Profesa Ibrahim Lipumba kuandika barua ya kutengua uteuzi wa barua aliyomwandikia Katibu mkuu wa Chama hicho Maalif Seif ya kujiuzulu nyifa wake,wasomi na wachambuzi wa masuala ya kisiasa, wamesema kuwa Profesa Ibrahim Lipumba amejimaliza kisiasa mwenyewe.
wakizungumza Dar es Salaam jana kwa njia simu na blog hii wasomi hao walisema kuwa kitendo alichofanya Profesa Lipumba ni sawa na kujimaliza kisiasa mwenyewe nakudai kuwa ameshauriwa vibaya.
Baadhi ya wasomi hao, Dkt. Benson Bana alisema kuwa Profesa Lipumba kimsingi amekosa mshauri na kwamba hakutarajia kama anaweza akachukua maamuzi kama aliyoyachukua hatua hiyo ni ya kujimaliza kisiasa.
"Profesa Lipumba amekosa mshauri kwani kulikuwa hakuna sababu ya yeye kutaka kurudi tena kwenye nafasi hiyo,miaka 20 amekuwa katika nafasi ya mwenyekiti binafsi naona miaka hii imetosha kabisa kwake na kulikuwa hakuna haja tena ya kutaka kurudi.'alisema Dkt. Bana
Aidha Dkt. Bana alihoji kwamba,Profesa Lipumba amezaliwa ndani ya Chama hicho na ndio maana anashindwa kukaa nje ya Chama hicho ?Nakuongeza kuwa kama kurudi basi angerudi akiwa kama mwanachama wa kawaida.
Pia alisema kuwa sababu za awali zilizomsababisha aweze kujiondoa ndani ya Chama hicho anahakika hadi sasa sababu hizo zimatatuliwa au anarudi kwa lipi?
Kwaupande wake Waziri wa Fedha mstaafu Serikali ya awamu ya tatu ya Benjamini William Mkapa,Prosefa Simon Mbilinyi alipoulizwa juu ya maamuzi hayo ya Profesa.Lipumba alisema kuwa yeye hana kometi kwani kama yeye karudi ni haki yake.
Alisema kuwa Profesa Lipumba anahaki ya kutoka na anahaki ya kuingia hivyo kwake haoni kama kuna makosa na kama alikuwa mwenyekiti basi arudi kwa nafasi hiyo hiyo aliyokuwepo.
Naye Mbunge wa Jimbo la Bumbwini CUF Zanzibar Mohamed Amour alipoulizwa kuhusu uamuzi wa Profesa Lipumba kutangaza kurudi tena ndani ya Chama hicho alisema kuwa ni mapema mno kuzungumzia suala hilo lakini muda muafaka utakapofika atazungumza.
Naye Mwanasheria wa Kituo cha sheria na Haki za Binadamu Harold Sungusia alisema mambo hayo ni ya wanasiasa wenyewe yeye hawezi kuzungumzia kwani taratibu zake wenyewe ndio wanajua.
kuelekea uchaguzi mkuu wa mwaka 2015, Profesa Lipumba alitangaza kung'atka huku akitoa sababu mbalimbali ikiwamo ,Umoja wa Katiba ya wananchi UKAWA kushindwa kuenzi Tunu za Taifa katika umoja wao kwa kuwakaribisha watu waliopitisha rasimu iliyochakachuliwa kwenye Bunge Maalumu la katiba.
Profesa Lipumba amekiri kushiriki katika vikao mbalimbali vya Ukawa mpaka hapa walipofikia . lakini akasema . "Nafsi yangu inanisuta kuwa katika maamuzi yetu tumeshindwa kuenzi na kuzingatia Tunu za Taifa za utu, uadilifu, uzalendo, uwajibikaji, umoja na uwazi ".
No comments:
Post a Comment