WAZIRI wa Nchi Ofisi ya
Rais ,Tawala za mikoa na Serikali za Mitaa ,George Simbachawene amesema kuwa pamoja na kuwepo kwa
Sheria, na Mikataba ya uwekezaji baina ya Serikali na Wawekezaji ni lazima
wananchi nao washirikishwe kikamilifu katika
utoaji wa kibali hicho cha uwekezaji ili nao waweze kunufaika.
Akizungumza Dar es Salaam
jana,wakati wa Mdahalo unaohusu masuala ya uwekezaji baina ya
serikali,wawekezaji na wananchi ulioandaliwa na Taasisi ya Uongozi,Simbachawene
alisema licha ya kuwepo kwa mikataba baina ya wawekezaji na Serikali pia
Wananchi wanapaswa kushirikishwa,ikiwa ni sehemu moja wapo ya wao kupata
maendeleo.
Alisema wananchi
wanaozungukwa na rasilimari mbalimbali wanapaswa kuwa sehemu ya maendeleo kutokana na uwekezaji
katika eneo husika na kuona faida kwa uwazi tangu siku ya kwanza muwekezaji
anapoanza kuwekeza.
“Hapa kuna wadau
mbalimbali wamekutana katika mdahalo wa kujadili mambo mbalimbali ya maendeleo
yanayohusu nchi za Afrika katika shughuli
zake ikiwemo katika masuala ya uchimbaji wa madini na mafuta na kuona ni
namna gani jamii inavyofaidika na kunufaika na wawekezaji wanaowekeza katika
maeneo yao,”alisema
Simbachawene alisema wananchi
wanahaki ya kutoa kibali kwa wawekezaji,na
kuwakubalia kufanya shughuli zao katika maeneo yao au la.
Alisema Tanzania ina nguvu
ya kiuchumi kutokana na uwepo wa rasilimali zake ambapo takwimu za mwaka 2015 zinaonyesha hadi sasa ni asilimia 10 tu za
madini nchini zimechimbwa huku asilimia 90 zikiwa bado hazijachimbwa katika
maeneo mbalimbali ya nchi.
Aidha alisema endapo
watanzania watakuwa makini katika kutunza rasiliamari zake itasaidia kuimarisha
uchumi imara katika nchi.
“Serikali na wananchi
tushirikiane kwani fursa tulizonazo ni nyingi mpaka sasa hakuna kilichoharibiwa
inatupasa tutumia elimu ili kurekebisha
makosa tuliyokuwa nayo katika mikataba ya uwekezaji,
Alisema zipo sheria mbalimbali zinazosimamia uchimbaji
na uvunaji wa rasilimali ya madini na Mafuta,ambapo mara nyingi rasiliamri hizi
zinapopatikana kuna tokea na fujo nyingi kutokana na wananchi kutoshirikishwa
juu ya uwekezaji unaofanyika katika maeneo yao.
Aidha alisema rasilimari
zinapovunwa na wawekezaji wananchi wanakuwa wanaachiwa madhara makubwa hivyo
elimu inapaswa kutolewa kwa wananchi pindi mwekezaji anapokuja kuwekeza ili
pawepo na uwazi zaidi.
“Wataalama duniani wamekaa
na kuendelea kufikilia zaidi ya sheria zaidi si kwamba mtu anaweza kuendesha
uvunaji wa rasirimali ya mafuta na Madini kwa kutumia sheria,ni lazma kuwepo
kwa kipengele cha wananchi kuwa na kibali cha makubaliano kati ya wananchi na
muwekezaji,”alisema
Alisema uwekezaji
unaofanywa na wawekezaji wengi unasababisha kuwepo kwa migogoro mingi ambayo
inatokana na kutoingia mikataba rafiki na wananchi wa eneo husika.
No comments:
Post a Comment