![]() |
Waziri wa Fedha wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Philip Mpango |
WAKATI Serikali kupitia Waziri wa Fedha na Mipango Philip Mpango akiwa amewasilisha Bajeti yake mapema wiki iliyopita mjini Dodoma tayari wadau,pamoja nawasomi wanaendelea kujadili Bajeti hio huku wangi wao wakipongeza na kundi lingine likisema Hapa Kazi Tu.
Katika Bajeti hiyo ambayo imeonekana kugusa nyanja mbalimbali na upande mwingine ikionekana kubana moja ya maeneo kama vile kodi za Magari,wabunge kukatwa kodi katika maato yao ya kuinua mgongo cha kulitumikia Bunge kwa miaka mitano.
Pia Bajeti hiyo imegusa katika kwenye eneo lingine la vileo kama Vile Beer pamoja na Pombe kali,Juice za nje na ndani,makato kutokana na kutuma na kupokea pesa kwa kutumia mihara ya tigo pesa,Mpesa,Airtel Money na mitandao mingineyo.
Hatua hizo zote jibu lake ni Serikali imejipanga kutaka kuhakikisha wanakusanya mapato ambapo mwisho wa wasiku wananchi waweze kupata maisha bora na nafuu lakini huku ikiwa ni sehemu ya utekelezaji wa ahadi mbalimbali zilizotolewa na Rais wakati akiomba ridhaa ya kuchaguliwa katika uchaguzi mkuu uliofanyika 2015.
Rais Dkt. John Magufuli katika kampeni zake alihaidi mambo mengi kwa wananchi ,moja ya mambo ambayo aliyahaidi ni kuhakikisha analibadili taifa kuwa nchi ya kujitegemea huku akisisitiza kuepuka kuwa ombaomba kama ilivyozoeleka,nakudai kuwa ili kuondokana na hali hiyo lazima watu wafanye kazi,nakuziba mianya ya upotemvu wa fedha.
Mambo mengine ambayo aliyahimiza ni kwenda kupambana na Rushwa ,pamoja na Mafisadi huku akihaidi kuazisha Mahakama ya mafisadi ambapo sote tumeona katika Bajeti iliyosomwa Mahakama hiyo imetengewa sh.bil 2.5 ili iweze kuazishwa rasmi.
Ahadi kubwa zaidi ilikuwa ni kuhakikisha serikali yake inakusanya kodi ya kutosha kwa kutumia Mamlaka ya Mapato Tanzania TRA ikiwamo kuibua zaidi vyanzo vya mapato kuazia Serikali kuu hadi katika ngazi ya Halmashauri.
Daniel Lukumayi yeye ni Mwenyekiti wa (UWAVIMA)Umoja wa wamiliki wa gereji ya vipuri vya magari, iliyopo Mabibo Manispaa ya Kinondoni,ambapo kwa upande wake akizungumzia Bajeti ya Serikali anasema kuwa kimsingi bajeti hiyo siyo mbaya kwani imejaribu kumulika katika nyanja muhimu na hususani kwenye eneo la vyanzo vya mapato.
Anasema kuwa anajua kuwa Serikali ya awamu ya tano imejipanga katika kuhakikisha inakuwa nchi yenye uchumi wa kati wa kutegemea Viwanda na ukusanyaji kodi wenye tija kwa ajili ya maendeleo ya wananchi wake.
"Binafsi jitihada za Rais Dkt. Magufuli na Serikali yake naunga mkono kwa asilimia zote ila mbali na kumulika katika maeneo kadhaa kwa ajili ya ukusanyaji wa kodi lakini viongozi wake inatakiwa waongeze kasi ya kubaini vyanzo vya mapato na zaidi katika ngazi za Halmashauri za Wilaya mbalimbali nchini."anasema Lukumayi
Anasema kuwa kama halmashauri hazitakuwa na macho ya kuona kama wapi pana vyanzo vya mapato ni wazi kwamba wanaweza kusababisha Serikali isitimize adhima yake ya kufikia katika uchumi unaohitajika kwa ajili ya maslahi mapana ya wananchi wake.
Akitolea mfano umoja wao UWAVIMA anasema kuwa wao biashara yao kubwa ni ya kununua na kuuza vipuri vya magari mbali na hivyo changamoto kubwa wanayokutana nayo ni ufinyu wa eneo la kufanyia shughuli zao.
Anasema kuwa wameshapambana mno,na kuzifikia mamlaka husika ili kupeleka maombi ya kutaka waatafutiwe eneo kubwa ambalo wanaweza wakafanya shughuli zao kwa kujinafasi lakini kila wanapopiga hodi ndani ya Manispaa ya Kinondoni kupitia viongozi wake,kwa Diwani,Ofisi ya Serikali ya Mtaa,hadi Halmashauri kwenyewe lakini hakuna kinachofanyika.
Mwenyekiti huyo anasema kuwa kutokana na uwingi wao na vijana wengi kuweza kujiari katika eneo hilo basi kama Halmashauri ya Kinondoni wangeona na kutilia mkazo wa wao kuweza kupata eneo kubwa bila shaka ingekuwa sehemu ya chanzo kikubwa cha mapato.
"Hapa tunajishughulisha na kazi hizi za Magari kama nilivyotangulia kusema kwa maana kununua, na kutengeneza,na kuuza vipuri vya magari hivyo tumejaribu kufuatilia kwa viongozi wetu ili waweze kututafutia eneo kubwa ili tuwezu kufanyia shughuli zetu ila imeshindikana."anasema Lukumayi
Anasema kuwa hakuna shaka yeyote kama Halmashauri ya Kinondoni wangewatafutua eneo kubwa la kufanyia biashara zao hizo wangekuwa wametengeza chanzo cha mapato kwa maana wangeza kuweka hata mtu wao ili ambaye angekuwa na mashine ya ushuru kwa maana katika kila gari ambalo linaingia hapo lingekuwa linatoa ushuru.
Akitolea mfano eneo wanalofanyia kazi anasema kuwa wanalipa mamilioni ya pesa kwa mtu mmoja lakini kama Manispaa wangeweza kusikiliza ombi lao la kuwapatia eneo kama wanavyofanya katika maeneo mengine inamaana kwamba pesa ambayo wanatoa huko ingekuwa inaingia kwao moja kwa moja.
Anasema kuwa wanatamani kuona siku moja wanaunga juhudi za rais za kuhamasisha kila mtanzania kuona anajukumu kubwa la kulipa kodi kwa muktaza wa ustawi wa taifa lake la maendeleo ya watu wake kama ilivyo katika mataifa mengine.
Lukumayi anaongeza kuwa lazima wamuunge rais mkono kwa kulipa kodi na ili walipe kodi lazima Halmashauri ziongeze ubunifu wa kubainisha vyanzo vya mapato ndani ya manspaa zao na kikubwa zaidi kuacha urasimu na kuendekeza vitendo vya rushwa,kwa maana kwamba huwezi kupewa kitu hadi upate kitu.
"Tupo tayari kulipa kodi na tunatamani kufanya hivyo lakini tutafanyaje hivyo wakati wakubwa hawataki kusikiliza kilio chetu,ndugu mwandishi kabla hatujafika eneo hili ambali umetukuta leo hii,awali tulikuwa Urafiki na kwenyewe tulilazimika kutoka kutokana na eneo hilo kuwa ndogo lakini baadae kulijitokeza changamoto zingine."anasema
Nakuongeza kuwa kuazia hapo kwa maana miaka kadhaa sasa imepita tumekuwa tukihaingaika kwa viongozi kuazia wanasiasa hadi serikali ili waweze kusaidia sisi kama watu wao tupate eneo kubwa lakufanyia shughuli zetu hizi lakini hadi Rais Magufuli anaingia madarakani hakuna eneo wala nini."anaongeza Lukumyi
Chini ya Serikali ya awamu tano.
Lukumayi anasema kuwa kutokana na Serikali ya awamu ya tano ilivyoanza kwa maana umakini wa ufuatiliaji na usimamiaji wa mambo wanamatumaini makubwa kwamba sasa kilio chao kitatuliwa.
Anasema kuwa ili kuthibitisha wanachokisema wanamuomba Mkuu wa Wilaya na Meya wa Manispaa ya Kinondoni, Ndugu Boniface Jacob kuona umuhimu wa kutembelea eneo hilo ili kujonea kwa macho yeye mwenyewe.
Anasema kuwa ikibidi hata Mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam Ndugu Paul Makonda kuzuru eneo hilo nakudai kuwa Makonda yuko mstari wa mbele na ameonesha nia ya kuinua uchumi na kipato cha watu wake hivyo afike na eneo hilo la Gereji ya uuza wa vipuri ambapo wanaamini akifika watapata eneo la kufanyia shuguli zao.
"Tumeona hivi karibu ametembelea eneo la Gereji kule kunduchi hivyo anaonesha ni kwa namna gani alivyokuwa mwepesi katika kushughulikia mambo ya watu wake,tunawaomba kwa moyo wa kipekee viongozi wetu hawa watupatie eneo ili mwisho wasiku tutoe mchango wetu kwa ajili ya maendeleo ya waliowengi."anasema Lukumayi
Lukumayi anamaliza kwa kusema kuwa Umoja wao uliaza mwaka 2014 na walifikia maamuzi hayo baada ya kuona wanaofanya shughuli hizo wapo wengi na walikuwa wametawanyikatawanyika na hadi kufikia leo wapo wanachama zaidi ya 144 mbali na wale wanaoingia na kutoka .
Anasema kuwa kukoseka kwa eneo lao mahususi kuna wanyima hadi fursa kukopa kwenye taasisi mbalimbali za kifedha nakudai kuwa kama halmashauri ya Kinondoni wakiweza kuwapa eneo inamaana watapata fursa ya kukopa na kuongeza mitaji yao.
No comments:
Post a Comment