![]() |
Mwanamuziki wa muziki wa kizazi kipya kutoka WCB Harmonize akiwa na Mpenzi wake Muigizaji maarufu wa Bongo movie Jackline Wolper wakiwa pamoja katika picha(selfie) (picha na mtandao) |
MSANII Harmonize kutoka WCB ambaye kwa sasa anatamba na kibao cha 'Bado', amesema hana tabia ya kuchezea wanawake ovyo, hivyo kama wakikubaliana na mpenzi wake msanii wa bongo muvi Jacqueline Wolper watafunga ndoa.
Muimbaji huyo ambaye ametoka katika familia ya dini ya kiislamu, amebainisha hayo siku chache zilizopita kuwa dini yake haimruhusu kuwachezea watoto wa kike.
Kwa sasa kuweka wazi kama tunakaa pamoja au hatukai siyo kitu kizuri cha kuzungumzia kwa sasa
“Insha’Allah panapo majaliwa tutakaa pamoja kwa sababu mimi sijaumbwa kwa ajili ya kuchezea wanawake alisema Harmonize.
Harmonize alisema akiwa na mwanamke wataandaa 'future' na kukubaliana wakae pamoja ,ambapo amewataka mashabiki wa muziki watuliekwani kuna mambo mazuri yanakuja.
No comments:
Post a Comment