UDART wafafanua mgomo wa madereva - MUANGALIZI

Hot

Post Top Ad

Your Ad Spot

Tuesday, June 14, 2016

UDART wafafanua mgomo wa madereva

UONGOZI wa UDART unaoendesha Mradi wa Mabasi Yaendayo Haraka Dar es Salaam (BRT), umetoa ufafanuzi juu ya madereva
waliogoma wakidai kulipa mshahara wa sh. 400,000 badala ya
sh. 800,000 walizodai kukubaliana.

Akizungunza na waandishi wa habari Dar es Salaam jana, Mkurugenzi Mtendaji wa UDART, David Mgwasa, amekiri mikataba ya madereva
hao kutakiwa kulipwa sh. 800,000 kwa mwezi kama wamekidhi
vigezo na masharti waliyokubaliana.

Alisema asilimia 85 ya madereva wote wamesaini mikataba ya kulipwa sh. 800,000 kwa  mwezi na kama watashindwa kukidhi vigezo na masharti yaliyowekwa watalipwa 400,000.

"Kwa mujibu wa mkataba wa dereva waliosaini na Inteligent Transport System (ISP),  mshahara kwa mwezi ni sh. 800,000 uliogawanyika katika sehemu mbili kulingana na mahitaji ya ufanisi wa mradi.

"Kiwango kisichobadilika kwa mwezi ni sh. 400,000, kiasi kilichobaki
kitalipwa kulingana na ufanisi wa kazi na mahitaji ya mradi kwa kila dereva ambayo ni kuanzaa zamu kwa wakati, utunzaji wa muda, uendeshaji wa kujihami, usafi wa mabasi, uendeshaji wa weledi
ili kuwepo na matumizi sahihi ya mafuta," alisema.

Aliongeza kuwa, lengo la kuweka masharti hayo ni kuhakikisha mradi unaendeshwa kwa umakini, weledi ili kutoa uduma bora.

Mgwasa alisema madereva wanadhani kuwa kazi yao ni kubeba abiria wakati kuna vigezo vingi kwani hata akiingia abiria mmoja, wanatakiwa kuondoa basi ili kutunza muda.

"Madereva tulionao ni 280 ambao kati yao, asilimia 85 wamesaini mikatabana, asilimia 15 ndio bado, wengine walipewa mikataba,
kuisoma na kusema hawaiwezi," alisema.

Alisema kulingana na masharti yaliyopo kwenye mkataba, kama dereva atashindwa kuyatimiza, anakatwa asilimia tano hadi 10 ya mshahara wake hivyo hawawezi.

"Mwezi huu, madereva wote watalipwa sh. 800,000 lakini kuanzia
Juni 16, mwaka huu, masharti yataanza kufanya kazi...tunamalizia kufunga mtambo wa kufuatilia mabasi yote ili kuhakikisha madereva wanazingatia muda wa kazi na wakikiuka masharti watakatwa
mishahara yao," alisema.

Aliongeza kuwa, kutokana na mradi huo kuzalisha ajira nyingi, wasimamizi wa wafanyakazi ni UDA Menejimenti Agence ambayo imesajiliwa na  Wakala wa Usajili wa Biashara na Leseni (BRELA)

Alisema kazi ya UDART ni kuhakikisha mabasi yako vizuri, yanatumika saa 16 kila siku.

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Your Ad Spot