Kinondoni wakabidhiwa milioni 19.3 - MUANGALIZI

Hot

Post Top Ad

Your Ad Spot

Tuesday, June 14, 2016

Kinondoni wakabidhiwa milioni 19.3

Mkuu wa wilaya ya Kinondoni Ally Salum

KANISA la The Pool Of Siloam Limetoa fedha kiasi cha sh. Millioni 19.3 kwa Halmashauri ya kinondoni kwa ajili ya kuchangia ununuzi wa Madawati.

Wakikabidhi fedha hizo kwa Mkuu wa wilaya kinondoni, Ally Salum Hapa jijini Dar es salaam jana Kiongozi wa Kanisa hilo Miaka 1000.

Alisema kanisa hilo limepata kibali cha kushiriki  baraka ya kutoa madawati ili kuunga mkono juhudi za serikali ya awamu ya tano za kutoa elimu ya msingi na sekondari bure.

Miaka 1000 alisema fedha hizo zimechangwa na waumini wa kanisa hilo na pia wanaamini kuwa wananchi wengi wasio na uwezo wanaweza kuchagia chini ya uongozi wa wenyekiti au kata na kupata madawati ya kutosha kama walivyofanya kanisa hilo.

"Tulikuwa tunatimiza mstari wa sita peke yake ambao umekuwa unahimiza kuombea jamii iliyotuzunguka lakini tulikuwa atujaanza kutimiza mstari wa saba ambao umekuwa ukiimiza kanisa kuwajibika kwa jamii iliyotuzunguka kwa vitendo uliopo kwenye Isaya 58:6-7"alisema Miaka 1000

Kwa upande wake Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni Ally Salum Hapi alisema ni mara ya kwanza kupata fedha kutoka kwa  Taasisi ya kidini  kujitokeza kutoa fedha hizo kwa ajili ya ununuzi wa madawati.

Alisema kanisa hilo limeonesha upendo wa dhati na linatakiwa kuingwa na taasisi za kidini kwa kujitoa na kuwajibika kwa ajili ya kutatua chagamoto mbalimbali.

"Huu ni mfano mzuri wa kuigwa katika  jamii na ni mara ya kwanza kwa taasisi ya dini kujitokeza na kuwajibika kwa ajili ya jamii kwa kuhakikisha chagamoto mbalimbali zinaweza kutatuliwa"alisema Hapi.

Hapi alisema fedha hizo zitakwenda kama zilivyokusudiwa kwa kuhakikisha wanafunzi wanaweza kusoma katika mazingira mazuri.

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Your Ad Spot