TMA yatoa tahadhari ya hali ya hewa nchini - MUANGALIZI

Hot

Post Top Ad

Your Ad Spot

Friday, June 10, 2016

TMA yatoa tahadhari ya hali ya hewa nchini

Na Mwandishi wetu.

MAMLAKA ya Hali ya Hewa Tanzania(TMA) imesema kuwa katika kipindi hichi cha  juni hadi Agosti mwaka huu hali ya hewa  inatarajia kuwa ya joto la wastani hadi juu ya wastani katika maeneo mengi.

Akizungumza Dar es Salaam jana Meneja kitengo kikuu cha utabiri(TMA) Samweli Mbuya,alisema  hali ya  hewa ya joto la chini ya wastani inatarajiwa katika maeneo ya  nyanda za juu Kusini Magharibi.

Pia alisema kutrokana na hali ya hewa katika kipindi hiki hali ya upatikanaji wa malisho ya mjifugo inatarajiwa kupungua na hivyo wafugaji wanashauriwa kuchukua hatua stahiki ili kukabilina na madhara yatokanayo na  uhaba wa malisho.

Vile vile alisema kwa  shughuli zinazotegemea hali ya joto wadau wanashauriwa kuchukua hatua stahiki ili kukabilina na  madhara yanayoweza kutokea kutokana na hali ya hewa inayotarajiwa.

"Mifumo ya hali ya hewa inaonesha uwezekano wa kupungua kwa joto la bahari katika eneo la ukanda wa Tropiki la bahari ya Pasifiki wakati  lile la ukanda wa magharibi wa bahari ya  Hindi  litakuwa la wastani katika kipindi cha juni hadio Agosti,"alisema Mbuya.

 Alisema  joto  katika bahari ya Atlantiki litakuwa chini ya  wastani na hali hiyo inatarajiwa  kusababisha upepo kuvuma kutoka  magharibi ukielekea mashariki katika maeneo ya ukanda wa Ziwa Victoria.

Pia alisema joto la bahari ya juu ya wastanbi linatarajiwa katika eneo la ncha ya kusini ya bara la Afrika hivyo kuathiri msukumo wa upepo wa kusi katika kipindi cha miezi ya juni  hadi Agosti.


Hata hivyo alisema hali hiyo itasababisha hali ya baridi kiasi  katika kipindi hicho, pia  vipindi vifupi vya mvua vinatarajiwa  kujitokeza katika maeneo machache ya Ukanda wa Ziwa Vikitoria na Uknda wa pwani ya Kaskazini  hasa Visiwa vya Unguja na Pemba.

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Your Ad Spot