Wapinzani kukatwa Posho Bungeni - MUANGALIZI

Hot

Post Top Ad

Your Ad Spot

Friday, June 10, 2016

Wapinzani kukatwa Posho Bungeni

Naibu spika wa Bunge la Jamhuri Ya Muungano wa Tanzania Dkt, Akso Tulia akizungumza na wabunge wa jimbo hilo hawapo pichani.
BUNGE la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania limetangaza rasmi kuwakata posho wabunge ambao wanasusia vikao vya Bunge kwa sababu kitendo hicho hakikubaliki.

Uamuzi huo moja kwa moja utawaathiri wabunge wa kambi Rasmi ya Upinzania wanaoendelea kusisia vikao vya Bunge  kutokana na kile wanachodai kutokuwa na imani na Naibu Spika, Dkt. Tulia Akson.

Uamuzi huo ulitangaza mjini Dodoma jana na Dkt. Tulia wakati akijibu mwongozo ulioombwa na Mbunge wa Nkasi Kaskazini kwa tiketi ya CCM,Alli Keissy, mwanzoni mwa wiki hii.

Keissy katika mwongozo wake alisema hakubaliani na kitendo cha wabunge hao kuingia dakika chache bungeni na kusaini fedha kisha kutoka bila kufanyakazi.

“Mheshimiwa Naibu Spika, huu si utumishi hewa? Nataka mwongozo wako katika hili na viongozi wa Serikali wanawaona kama sio kuiibia Serikali ni nini? Je kesho sisi tukija hapa kutia vidole na kutoka tukakuacha wewe na makatibu wako Bunge litaendelea!"Alihoji Kessy.

Akijibu mwongozi huo jana mjini Dodoma,Naibu Spika Dkt.Tulia, alisema ametafakari kwa kina na kubaini kuwa vitendo vya baadhi ya wabunge kutia saini na kuingia ukumbini na kisha kutoka nje jambo havikubaliki. Alisema alifikia hatua hiyo baada ya kupitia maamuzi mengine yaliyowahi kutolea na Bunge.

Alisema wabunge wanapotoka nje wanakuwa wanakiuka masharti ya katiba yanayolipa Bunge majukumu ya kutekeleza shughuli zake ndani ya Bunge hilo.

"Kanuni ya tano fasiri ya kwanza ya kanuni za kudumu za bunge toleo la januari 2016 linaeleza kwamba kipi kinapaswa kuzingatiwa pamoja na mambo mengine maamuzi ya awali yaliyowahi kutolewa na maspika ya bunge yaliyopita katika sula hili,"alisema Dkt. Tulia.

Alisema kuwa amepitia maamuzi mbalimbali yaliyotolewa na baadhi ya maspika waliopita juu ya suala kama hilo hususani vitendo vya wa bunge kususia vikao na kutoka ukumbini bila kutekeleza shughuli za bunge.

Alisema Aprili  8,2008 wabunge wa Chama cha wananchi CUF waliwahi kutoka bungeni na kususia shughuli rasmi za bunge zilizokuwa zimepangwa kutekelezwa kwa siku hiyo katika bunge hilo, hivyo kutokana na kitendo hicho wabunge hao, kiti cha Spika kilitoa uamuzi  wa wabunge waliotoka nje kwa shughuli zisizokuwa rasmi kuwa hawastahili kulipwa posho zinazohusika kwa siku zote ambazo hawakuhudhuria vikao vya bunge.

Alisema kutokana na uamuzi huo wabunge hao hawastahili kulipwa posho.

"Napenda kuwakumbusha wabunge wetu kwa mujibu wa kanuni ya 149 ya fasili ya kwaza ya Bunge kila mbunge anawajibu wa kuhudhuria vikao na kamati zake, hivyo jambo hili linapaswa kuzingatiwa na kila mmoja wetu na kitendo cha baadhi ya wabunge kutoka nje mara kwa mara baada ya kujisajili ni ukiukwaji wa kanuni za bunge letu,"alisisitiza Dkt. Tulia

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Your Ad Spot