Samia mgeni Rasmi siku ya kuchangia vifaa vya elimu - MUANGALIZI

Hot

Post Top Ad

Your Ad Spot

Tuesday, June 14, 2016

Samia mgeni Rasmi siku ya kuchangia vifaa vya elimu

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Sulihi

MAKAMU wa Rais Samia Suluhu Juni 18 mwaka huu anatarajiwa kuwa mgeni rasmi katika harambee ya kuchangia vifaa vya elimu kwa wanafunzi wanaoishi katika mazingira magumu iliyoandaliwa na Taasisi ya Binti Foundation.

Akizungumza na waandishi wa habari mwishoni mwa wiki,Mkurugenzi wa Taasisi ya Binti Foundation Johari Sadick alisema kuwa,harambee hiyo itaambatana na matembezi ya hiyari yatakayoanzia Viwanja vya Biafra Kinondoni hadi Leaders Club.

Alisema siku hiyo itakuwa ya kipekee kwa watoto kwani itatumika kujadili matatizo mbalimbali ambayo yameendelea kuwa kikwazo kwa watoto kutimiza ndoto zao ikiwamo kukayishwa masomo kutokana na sababu mbalimbali ikiwemo baadhi yao kupata ujauzito wakiwa shule pamoja na kukosa uangalizi wa karibu kutoka kwa wazazi.

''Kutokana na siku ya mtoto wa Afrika kuadhimishwa Juni 16 kila mwaka Binti Foundation Juni 18 tutafanya  matembezi kutoka Viwanja vya Biafra Kinondoni kuelekea Learders Club na matembezi hayo yataongozwa na  Rais wa awamu ya nne Dkt.Jakaya Kikwete ambaye baadaye siku hiyo atatoa zawadi mbalimbali kwa wanafunzi wa Shule za msingi Dar es Salaam ambazo zimekuwa zikifanya vizuri.

Aidha alisema tangu taasisi hiyo ianze rasmi miaka miwili iliyopita tayari imeshasaidia zaidi ya watoto 50  kwa kuwawezesha kupata mahitaji muhimu ikiwemo afya na elimu na kusisitiza lengo kubwa la Binti Foundation ni kuhakikisha watoto wote nchini hususan wa kike wanapata elimu. 

Alisema Taasisi ilifanya utafiti na kubaini kuwa watoto wa kike wamesahaulika katika suala la elimu hivyo jitihada zaidi zinahitajika ili kuhakikisha mtoto binti wa kike anapata elimu sawa na wa kiume ili aweze kutimiza ndoto za kuwa na maisha bora.

Mbunifu wa mavazi ambaye pia ni Mkurugenzi wa Afrika Sana Alliga Jane aliizungumzia siku ya mtoto wa Afrika kwa kuwataka wazazi kuitambua siku hiyo na kuwaendeleza katika tamaduni za kiafrika, huku akiwasisitiza wazazi na walezi kuitumia siku hiyo kuwaangalia watoto walio katika mazingira magumu kwa kuwawezesha kuweza kufikia malengo.

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Your Ad Spot