Mamia ya wasichana walioko India, Thailand, Oman Saudia kurejeshwa nchini - MUANGALIZI

Hot

Post Top Ad

Your Ad Spot

Tuesday, June 14, 2016

Mamia ya wasichana walioko India, Thailand, Oman Saudia kurejeshwa nchini

SERIKALI ya Tanzania imesema kuwa, itawarudisha nchini mamia ya wasichana raia wa nchi hiyo waliokwama nchini India na mataifa mengine baada ya Taasisi zilizowachukua kwenda kuwatafutia ajira, kukiuka mikataba yao na kuwalazimisha kufanya kazi tofauti ikiwemo ya ukahaba.

Vyombo vya habari vya kimataifa vilimnukuu Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mindi Kasiga wakati akizungumzia matatizo wanayoyapata Watanzania wanaokwenda kufanya kazi nje ya nchi.

Kwa mujibu wa Kasiga,alisema kati ya mwezi Machi hadi Mei mwaka huu, balozi za Tanzania nchini India, Malaysia na nchi kadhaa za Mashariki ya kati, zilipokea maombi ya kutaka kusaidia kuwarejesha nyumbani.

Alisema watanzania hao walipelekwa katika nchi hizo kwa ahadi za kupatiwa ajira ambazo hutolewa na watu wasio waaminifu ambao wengi wao wanashukiwa kujihusisha na mtandao wa magendo ya biashara za binadamu.

Aliongeza kuwa,mtandao huo umekuwa ukiwatafuta wasichana wenye umri kati ya miaka 18 hadi 24 au chini ya umri huo na kuwalaghai kuwa kuna fursa za ajira katika hoteli, migahawa, maduka makubwa au kazi za nyumbani katika nchi za nje ambapo baada ya hapo huwawezesha kupata hati za kusafiria na tiketi za ndege kwa ajili ya kusafiri kwenda nchi husika.
Hata hivyo alikiri kuwa, wasichana wengi huwa wanafahamu mapema kuhusu kazi wanayoenda kuifanya huko ughaibuni na kwamba ugumu wa maisha ndio huwa unawasukuma na kujikuta wanaingia kwenye matatizo makubwa.

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Your Ad Spot