![]() | |
Msanii wa Muziki wa Bongo fleva Ney wa mitego |
MSANII wa muziki wa Bongofalva Ney wa Mitego ameonekana kama kuitupia dongo kimtindo familia ya Wasafi Classic (WCB).
Ney amefunguka kuwa wasanii wachanga wanajisikia ufahari kutoka kimapenzi na mastaa wa kike wenye umri mkubwa kwa kuwa hawawezi kujizuia kwakuwa walikuwa wanawatamani kwa muda mrefu
Mimi siwezi kuwalaumu hao vijana kuwa na uhusiano nao, unajua unaweza kuwa mtaani siku moja ‘unawishi’ kuwa na mtu fulani halafu ghafla ikatokea nafasi kama hiyo, hapo hata upewe ushauri wa dizaini gani mtu ambaye ulikuwa ukimuona kwenye runinga anaingia kwenye 18 zako, siwalaumu ingawa wanatakiwa kuwa makini,” alisema Ney
Pia nyota huyo anayetamba na ngoma nyingi akaweka wazi kuwa wasanii wengi wa kike wamekuwa wakiutumia udhaifu huo ili kutembea na wasanii wachanga.
No comments:
Post a Comment