![]() |
Msanii wa Filamu nchiniFaiza Ally |
MSANII wa filamu nchini mwenye kipaji ambaye hivi sasa anaendelea kutambulika kwa vituko vingi Faiza Ally, amesema atafurahi sana endapo atampata mtu wa kumhonga kwa sababu hajawahi kuhongwa hata siku moja.
Faiza amefunguka kuwa ameanzia mbali kutafuta fedha na karibu kila kitu chake anajihudumia mwenyewe.
“Ninatamani ningepata mtu wa kunihonga, mimi kila kitu najifanyia ambapo kwa sasa
hata moja ya mradi wangu nimesimamisha mwenyewe ” alisema.
Msanii huyo ambaye anategemea kuiingiza sokoni filamu yake mpya muda si mrefu, ameweka wazi kuwa amenunua gari ya ndoto yake aina ya Landrover bila kumtegemea mtu na kwamba mafanikio yake ni kutokana na kujiamini kwake katika utafutaji.
"Unajua wanawake wengi hawajiamini katika harakati zao za kutafuta maisha ndio maana wamekuwa wepesi kuhongwa na kudanganywa na wakati fulani hata kuharibu pale ambapo tayari walipatengneza kwa mikono yao,mimi sijawahi lakini natamani atokee huyo wa kunihonga," alisema mwadada huyo mwenye vituko.
No comments:
Post a Comment