Serikali imewatangazia kimbunga
cha moto mawakala wa sukari na wafanyabiashara wa rejareja mkoani Arusha wale
wote watakaoficha bidhaa hiyo baada ya kiwanda cha TPC kuanza uzalishaji wake
Akizungumza na waandishi wa
habari, Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro, Said Mecky Sadiki, alisema sukari
hiyo itakapoingia sokoni, wasambazaji na wafanyabiashara wa rejareja yeyote
atakayeuza tofauti na bei elekezi ya serikali atafikishwa kwenye vyombo vya
sheria.
Sadiki alisema kwa mfanyabiashara yeyote atakayekuwa na sukari kutoka nje
kwenye duka au ghala lake mara baada ya sukari ya TPC kuingia sokoni,
atalazimika kuuza bei elekezi ya serikali bila kujali bidhaa hiyo imetoka wapi.
“Kiwanda
cha TPC kitaanza uzalishaji wa sukari kesho, na watahadharisha mawakala na
wafanyabiashara wa rejareja, kutojiingiza kwenye mchezo mchafu wa kuhodhi
bidhaa hiyo. Hatutaki kusikia kisingizio kuwa sukari inayouzwa bei ya juu
inatoka nje,…tunachotaka sukari iuzwe bei elekezi ya serikali ya shilingi 1800
,” alisema
Sadiki.
Sadiki alisema bei ambayo kiwanda cha TPC itawauzia mawakala inajulikana
na serikali, hivyo kinachotakiwa kwa mawakala hao ni kuongeza asilimia 3.25,
pamoja gharama nyingine kama usafiri na sio vinginevyo, ili wananchi waweze
kuipata kwa bei elekezi ya serikali.
No comments:
Post a Comment