Miundombinu ya uhakika ni tatizo TRL - MUANGALIZI

Hot

Post Top Ad

Your Ad Spot

Tuesday, June 14, 2016

Miundombinu ya uhakika ni tatizo TRL

Mafundi wa TRL wakiwa wanachunguza sehemu zilizoharibika za reli hiyo.

KUKOSEKANA kwa miundombinu ya uhakika katika usafiri wa njia ya reli ni moja ya changamoto zinazoikabili sekta ya Uchukuzi na kusababisha Kampuni ya Reli Tanzania (TRL)
kushindwa kuongeza uwezo wa Kampuni kiutendaji ili kutoa mchango katika uchumi.

Pamoja na sekta hiyo kuwa na umuhimu katika suala zima la usafirishaji  wa abiria na mizigo ndani na nje ya nchi bado changamoto ya udhaifu wa njia,upungufu wa vitendea kazi uchakavu wa karakana na uhaba wa wahandisi katika idara zote ni changamoto inayosababisha Kampuni hiyo kushindwa kuongeza uwezo kiutendaji ili kutoa mchango katika uchumi na  kuongeza kipato ili kuweza kujitegemea.

Akizungumza  na waandishi wa habari hali halisi pamoja na mikakati ya Menejimenti ya Kampuni hiyo ambayo imewekwa na Kaimu MKurugenzi wa TRL Masanja Kadogosa ndani ya siku tisini tangu alipoingia rasmi kwenye Kampuni hiyo akitokea
Benki ya Rasilimali (TIB), anasema Kampuni imeandaa mipango ya muda mfupi na mrefu.

Anasema mipango hiyo inaainisha maeneo muhimu ya kuwekeza kwa ajili ya kuiongezea Kampuni  uwezo wa kiutendaji na kutoa mchango katika uchumi sambamba na kuongeza kipato ili iweze kujitegemea.

"Kama Kampuni tunajiandaa kuleta treni mbili za kisasa (DMUs) kwa ajili ya usafiri wa Jiji la Dar es Salaam, treni hizo zitakuwa na uwezo wa kubeba abiria 1,000 kila moja na zitahudumia maeneo ya Ubungo na Pugu likiwemo tawi la kwenda uwanja wa ndege wa Mwl.Julius Nyerere,"anasema.

Anazungumzia mapato ya treni ya Jijini Dar es Salaam maarufu (Treni ya Mwakyembe) inayofanya safari zake kuanzia stesheni hadi Ubungu kuwa,mapato yake yameongezeka  kutoka wastani wa Sh.milioni 1.5 hadi kufikia milioni 3.3 kwa siku ambalo ni ongezeko la asilimia 120.

Anasema kutokana na ongezeko hilo Kampuni imeanza kupeleka michango ya wafanyakazi wake  kwenye Bima za afya na kuimarisha uhusiano wake wa kikazi na Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) kwa kuanza kupeleka kodi za serikali  mara baada ya kufanya makusanyo.

Anaongeza kuwa, mapato ya treni ya masafa marefu (main Train) kwa abiria wa njiani kuwa yameongezeka kutoka sh.milioni 80.8 mwezi Mei 2015 hadi kufikia sh. milioni 155.40 mwezi Mei 2016 sawa na ongezeko la asilimia 92.3.

"Mapato haya yanaenda sambamba na kupungua kwa matumizi ya mafuta ya dizeli kwa vichwa vya treni, kutoka asilimia 56 hadi asilimia 49 na lengo likiwa ni kupunguza matumizi ya mafuta hadi kufikia asilimia 30 na hii inatokana na udhibiti wa mwenendo wa matumizi wa mafuta katika vichwa vya treni",anasema Kadogosa.

Kwa upande wa usafirishaji wa mizigo Kaimu Mkurugenzi anasema Kampuni inaendelea na ushawishi wa wateja wakubwa na hadi kufikia Mei 2016 mteja mkubwa alikuwa ni Tanga Simenti na kwamba katika kipindi cha mwezi Juni Kampuni inategemea kusafirisha mzigo wa Bakhresa wenye uzito wa zaidi ya tani 5000 kwenda Rwanda na Burundi.

Aidha kuhusu maandalizi ya kubadilisha reli Mpiji hadi Soga kilometa 12 yamekamilika na kazi itaanza rasmi Juni 15 mwaka huu na kwa upande wa Mpanda katumba kilomita 162 hadi 176 mataruma 12,800 ya kutosha kilomita 9 yalishapelekwa na reli za kutosha kilomita 2 zenye ratili 56 zilishapelekwa pia sambamba na behewa mbili za vifungo.

Anasema kwa kutumia mafundi mafundi wa kampuni imeweza kufufua mabehewa 24 kwenye karakana ya reli ya Dodoma na juhudi za kufufua mengine ziunaendelea kwa gharama nafuu huku akisisitiza mkakati huu utaendelea kwa karakana za tabora na Dar es Salaam ambapo Kampuni ingenunua mabehewa mapya ingepata gharama kubwa kwa kuwa behewa moja huuzwa kwa sh milioni 230 hivyo kwa mabehewa 24 Sh. bilioni 5.52 zingehitajika.

Kuhusu matengenezo ya ishara na mawasiliano maeneo mbalimbali tayari yamewekewa umeme wa Sola na mitambo ya mawasiliano imewekwa nishati hiyo.

Hata hivyo anatoa wito kwa wadau wote wa reli hususan wananchi wanaoishiu maeneo ya kandokando ya njia ya reli kuilinda miundombinu hiyo kwani ni rasilimali ya Taifa.

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Your Ad Spot