Na Heriard Mwallow:
Mahakama ya hakimu mkazi Kisutu Jiji Dar es Salaam
imetengua matekeo ya Udiwani Kata ya Saranga
Manispaa ya Kinondoni.
Uamuzi huo ulitolewa jana na Hakimu Lwaliarwange
Lema wa mahakama hiyo na hivyo kutengua matekeo
yaliyokuwa yamempa ushindi Mgombea wa Chadema
Ephrahim Kinyafu dhidi ya mgombea wa CCM Haroni
Mdoe.
Katika hukumu hiyo Lema alisema kuwa sababu kubwa
ya kutengua matekeo hayo ni kutokana na kukiukwa kwa
taratibu mbalimbali za uchaguzi za mwaka 2015.
Akizungumza baada ya hukumu hiyo aliyekuwa diwani
wa Kata hiyo Ephrahim Kinyafu alisema kuwa
hakubaluanai na matokeo hayo na kivyo atakata rufaa
kupitia kwa mawakali wake na anaamini haki itatendeka
mbele ya safari.
"Nimepokea hukumu ya kesi hii iliyo tengua matokeo
yaliyonipa ushindi mimi ila sijaridhishwa na hukumu hii
na nategemea kukata rufaa kupitia kwa mawakili wangu
na naamini huko mbele haki itatendeka kwa kunirudishia
ushindi wangu" alisema Kinyafu.
Kwa upande wake aliyekuwa mgombea wa CCM Harouni
Mdoe alisema kuwa alikuwa na imani atashinda kesi
hiyo maana hakukurupuka kukata rufaa kutokana na
matukio yaliyotokea kwenye kutangaza matokeo.
"Ninamshukuru Mungu kwa kuwana nasi leo na
ninaishukuru mahakama kwa kutenda haki, nilijua
nitashinda maana matukio yaliyotokea wakati wa
kutangaza matokeo yalikuwa wazi" alisema Mdoe.
"Sikukurupuka kufungua kesi, nilishauriana na chama
pamoja na wanasheria kabla ya kufungua kesi, hata
wakikata rufaa ninauhakuka nitashinda tena" alisisitiza
Mdoe.
Kesi hiyo ilifunguliwa na mgombea wa CCM na sasa
mahakama imesema taratibu za taasisi nyingine
zinazohusika zitajua namana ya kuwapatia wanan
Saranga mwakilishi kama ni kurudia uchaguzi au
kumtangaza mgombea wa CCM kama mshindi moja kwa
moja.
No comments:
Post a Comment