Zitto Ahojiwa tena - MUANGALIZI

Hot

Post Top Ad

Your Ad Spot

Tuesday, June 14, 2016

Zitto Ahojiwa tena

Kiongozi wa Chama cha ACT Wazalendo na Mbunge wa Kigoma Mjini Ndugu Zitto Kabwe aliitwa na kuhojiwa na Jeshi la Polisi jana Jioni na kuachiwa.

Moja ya Mambo yaliyohojiwa na polisi ni Kongamano letu la kujadili Bajeti lilikuwa lifanyike leo tarehe 14 Juni, 2016 Makao Makuu ya Chama Kijitonyama Dar es Salaam.

Jeshi la Polisi limeendelea Kushikilia msimamo wa kulizuia Kongamano letu kwa madai kuwa linalenga kuchochea uvunjifu wa amani.

Kama inavyofahamika ACT Wazalendo ni Chama kinachoheshimu sheria za nchi na kulinda misingi ya amani kwa maslahi mapana ya Taifa letu. Hili limejidhihirisha wazi kwenye mikutano yetu.

Tunakitafsiri Kitendo cha kuendelea kulizuia Kongamano letu kama mbinu ya kuzima Mjadala wa Bajeti na kuminya demokrasia.

Wanasheria wetu Wanashughulikia kufungua kesi ya kikatiba kupata tafsiri ya kimahakama dhidi ya vitendo hivi vya jeshi la polisi kuzuia Mikutano ya hadhara na Makongamano ambayo ni haki ya kisheria ya vyama vya siasa.

Ado Shaibu, Katibu, Itikadi, Mawasiliano na Uenezi

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Your Ad Spot