Balozi wa Oman hapa nchini Saoud Ali Mohamed al Ruqaishi na Rais Magufuli |
Rais John Pombe
Magufuli ameagana na Balozi wa Oman hapa nchini Saoud Ali Mohamed al Ruqaishi
ambaye amemaliza muda wake wa uwakilishi hapa nchini.
Akizungumza na Balozi
huyo, Ikulu Jijini Dar es salaam Rais Magufuli ameishukuru Oman kwa kuendeleza
ushirikiano na uhusiano wa kihistoria na kidugu na Tanzania na ameahidi kuwa
serikali yake ya awamu ya tano ipo tayari kuongeza ushirikiano huo.
Tanzania kwa
kushirikiana na nchi za Oman na China zimekubaliana kutekeleza mradi wa ujenzi
wa Bandari ya Bagamoyo Mkoani Pwani. Rais Magufuli pia amemuomba Balozi
Saoud Ali Mohamed al Ruqaishi kufikisha salamu zake kwa Sultani wa Oman Mtukufu
Qaboos bin Said al Said………
>>>”Naomba
umfikishie salamu zangu za dhati Mtukufu Qaboos bin Said al Said, Sultan wa
Oman na umwambie tunamkaribisha Tanzania na nitafurahi kuona mradi wa uwekezaji
wa Bagamoyo unakuwa kielelezo cha undugu na urafiki wetu uliodumu kwa miaka
mingi”
No comments:
Post a Comment